Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuandikwa vibaya na gazeti la chama la Uhuru.
"Tunamuomba radhi Rais kwa kumlisha maneno, ukifuatilia mahojiano yoyote BBC hakuna sehemu amezungumza na muungwana ni vitendo. Tayari bodi imewasimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji, Ernest Sungura, Mhariri mtendaji na Rashid Zahoro ambaye alikuwa msimamizi gazeti;
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za chama zilizopo Lumumba mkoani Dar es Salaam.
Pia ndugu Chongolo ametangaza kusimamisha uchapwaji wa gazeti la Uhuru kwa siku saba kuanzia leo Jumatano kwa kuandika habari ya kupotosha juu ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Kupitia gazeti hilo nakala ya leo lilionekana kumlisha maneno Mwenyekiti huyo wa chama Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464