Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana na Ajira) Mhe.Patrobas Katambi, amewashukia viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wanaodai Katiba mpya, akisema madai hayo ni uchu wa vyeo na hayalengi maslahi ya taifa.
Amesema anashangazwa kuona wanaodai katiba mpya sasa ndiyo waliosusia vikao vya bunge la Katiba wakati wa serikali ya awamu ya nne na kuongeza kuwa, walifanya hivyo baada ya kuona ya kwao hayajafanikiwa.
Katambi aliyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, wakati wa mkutano wake na wandishi wa habari, uliolenga kutoa ujumbe wa serikali kwa vijana nchini.
Alisema madai hayo ya katiba mpya yanalenga watu fulani kufanikisha kuingiza mambo yao ndani yake ili yawasaidie kupata vyeo na kushinda uchaguzi wala si maslahi ya taifa.
“Wanaodai katiba mpya leo ndiyo hao waliokimbia vikao vya bunge la katiba wakati wa serikali ya awamu ya nne, kwa sababu walitaka yao yaingie waliposhindwa wakaamua kuvuruga mchakato,” alisema.
Katambi ambaye wakati huo alikuwa kiongozi wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), kabla ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alifafanua kuwa mchakato wa katiba mpya wa awali uliigharimu serikali zaidi ya sh. bilioni 200 bila mafanikio.
Alieleza kwa sababu watu fulani walitaka ndani ya katiba hiyo, kuhusishwe mambo yao badala ya maslahi ya taifa, iliposhindikana walikimbia bunge na kubadili mtazamo.
“Wakati huo sisi tulikuwa wanasheria na wanaharakati wa mambo hayo, baada ya kukimbia bunge la katiba wanayoidai sasa wakaamua kujiunga na kutengeneza UKAWA ambao ulihusisha muunganiko wa vyama kadhaa vya upinzani,” alisema.
Alifafanua katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, muungano huo walikubaliana kutoa mgombea mmoja wa urais na wakati wakivutana, kuna chama kilikuwa na mgombea wake mfukoni na hivyo baadaye alipendekezwa.
Alibainisha kuwa kabla ya uchaguzi na baada ya kumpendekeza mgombea wa urais ndani ya UKAWA kulikuwa na mvutano mkali wa kuunda Baraza la Mawaziri, ambapo kila chama kilitaka Waziri atoke ndani yake.
“Angalia mgogoro wa kugombea vyeo ulianza kabla ya ushindi, vyama viligombana nani awe Waziri Mkuu kila chama kikihitaji atoke kwake, viligombea wizara mbalimbali na baada ya mvutano mkali Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR Mageuzi vilijitoa na vingine kufuata”.
Aliongeza, “Sasa fikiria hawa waliogombea maslahi na vyeo ndiyo leo wanadai katiba mpya unadhani wanalenga maslahi ya nani, wanachohitaji ni kwamba Katiba iguse mambo yao sio masuala ya kitaifa”.
Alieleza kuwa hitaji la katiba mpya..............

SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MICHUZI BLOG
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana na Ajira) Mhe.Patrobas Katambi akizungumza masuala ya vijana na mwelekeo wa Serikali katika kushughulikia masuala yanayohusu vijana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Agosti 14, 2021 katika Ofisi za PSSSF Jijini Dar es Salaam.kulia Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Habari Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Bw.Jumanne Isango (Picha Zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana na Ajira) Mhe.Patrobas Katambi,Akionyesha ilani ya CCM,Kulia ni Mkurugenzi Uhamasishaji wa Habari Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Bw.Jumanne Isango, kushoto Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiendelea na kazi kama inavyoonekana ichani (Picha Zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
Afisakazi Mwandamizi (TAHESA)Peter Ugata akitoa maelezo ya mipango ya Serikali katika kutoa mafunzo tarajali kwa vijana ilivyotoa msaada wa kutatua changamoto za ajira nchini.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda (kulia) akizungumza kuhusu masuala ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi wakati wa mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam.kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana na Ajira) Mhe.Patrobas Katambi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464