KLABU YA MAZOEZI PJFCS WAONDOKA NA KOMBE BONANZA LA MICHEZO, RPC KYANDO AONYA UHALIFU

 


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP George Kyando, kulia, akikabidhi Kombe kwa washindi wa Mashindano ya Bonanza la Michezo, Klabu ya Mazoezi ya Mjini Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFCS) baada ya kuwashinda Klabu ya Mazoezi ya Kahama, akipokea Kombe hilo ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Mazoezi Shinyanga Lucas Morn.



Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Klabu ya mazoezi Polisi jamii Fitness Center ya mjini Shinyanga (PJFCS), ambayo inalelewa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, imeshinda kombe kwenye Bonanza la michezo, kati ya klabu ya mazoezi ya Kahama.

Bonanza hilo limefanyika leo Jumamosi Agosti 14, 2021 katika uwanja wa michezo wa Jeshi la Polisi Kambarage Mjini Shinyanga, lililokuwa na lengo la kufahamiana na kujifunza, kati ya klabu ya Mazoezi ya Kahama na wenyeji Shinyanga.

Mwenyekiti wa Klabu ya Mazoezi ya Polisi Jamii Fitness Center ya Mjini Shinyanga Sadick Kibira, amesema wameendesha Bonanza hilo la michezo ili kujenga pia urafiki na klabu ya michezo ya Kahama ambayo bado ni changa.

"Wenzetu hawa wa Kahama, walituomba kuja kwetu kujifunza sisi ambavyo hua tunafanya katika klabu yetu, tukaona tuandae kabisa na Bonanza la michezo ili mshindi aondoke na Kombe,"amesema Kibira.

"Michezo ambayo imechezwa ni, Mpira wa Miguu, kukimbia Mita 100 na 400, Mbio za Vijiti, Magunia, pamoja na kuvuta Kamba, ambapo Shinyanga kati ya michezo yote hiyo, tumeibuka na ushindi wa Points 22 kwa 18, na kuchukua Kombe," ameongeza Kibira.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Mazoezi ya Kahama (Kahama Jogging Club) Hussein Salum, amesema wamejifunza vitu vingi kutoka klabu ya mazoezi ya Shinyanga, ambavyo watakwenda kuvifanyia kazi na kuwajenga zaidi.

"Klabu yetu ya mazoezi ya Kahama ni changa kabisa, ina mwezi mmoja tu, hivyo tukaona ni vyema tuje kujifunza kwa wenzetu hapa Shinyanga, na tumeona vitu vingi sana, na tumekidhi mahitaji kwa asilimia 150," amesema Salum.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP George Kyando, amewataka wanachama wa klabu hizo za mazoezi, kuwa na nidhamu ya hali ya juu, pamoja na kuchukia masuala ya uhalifu.

Amesema, licha ya klabu ya mazoezi ya Kahama kumuomba awe mlezi wao, kama ilivyo ya Shinyanga, amesema endapo akisikia kuna vitendo vya uhalifu, yupo tayari kujitoa pamoja na kuwachukulia hatua, bila ya kujali ni mlezi wa klabu hiyo.

Pia, Kamanda ametoa wito kwa wananchi mkoani Shinyanga, wapende kufanya mazoezi, sababu michezo ni afya, na itawasaidia kupambana na janga la virusi vya Corona.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI👇👇

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP George Kyando, akizungumza na wanachama wa Klabu za mazoezi Kahama na Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, akizungumza kwenye Bonanza hilo la michezo, inayo onekana ni Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Klabu ya Michezo ya Kahama (Kahama Jogging Club).

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, akizungumza kwenye Bonanza hilo la michezo, inayo onekana ni Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Klabu ya Michezo ya Shinyanga (PJFCS).

Mwenyekiti wa Klabu ya Mazoezi ya Polisi Jamii Fitness Center, Sadick Kibira, akielezea madhumuni ya Bonanza hilo la michezo.

Makamu mwenyekiti wa Klabu ya mazoezi ya Polisi Jimii Fitness Center Lucas Morn, akielezea historia ya Klabu hiyo kuwa ilianza mwaka 2014 na ina wanachama 150, ambapo licha ya mazoezi pia wanajishughulisha na shughuli za kijamii, kusaidia wahitaji, pamoja na kutangaza utalii wa ndani.

Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Kahama (Kahama Jongging Klabu) Hussein Salum akitoa historia ya kuanzishwa kwa Klabu hiyo kuwa imeanzishwa Julai mwaka huu.

Awali Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, akifungua rasmi Bonanza hilo la michezo kwa kupiga Penat.

Bonanza hilo la michezo likichezwa kwa kuanza na mpira wa miguu, ambapo wenye Jezi za Njano ni Timu ya Polisi Jamii Fitnes Center ya Mjini Shinyanga wakiwa na Timu ya Klabu ya mazoezi ya Kahama.

Soka liliendelea kuchezwa, ambapo Timu ya Kahama Jogging Klab, waliibuka na ushindi wa Magoli Mawili kwa Sifuri.

Mashindano ya riadha yakiendelea kwa upande wa wanawake Mita 400 na mshindi kutoka Shinyanga, ambapo Mita 100, alitoka Kahama.

Mashindano ya riadha yakiendelea kwa upande wa wanaume, na mshindi kutoka Kahama.

Mashindano ya kukimbia kwa magunia yakiendelea kwa upande wa wanawake na mshindi kutoka Shinyanga.

Mashindano ya kukimbia kwa magunia yakiendelea kwa upande wa wanaume na mshindi kutoka Shinyanga.

Mashindano ya kuvuta Kamba kwa upande wa wanawake yakiendelea ambapo Shinyanga waliibuka washindi

Mashindano ya kuvuta Kamba kwa upande wa wanaume yakiendelea, ambapo Shinyanga waliibuka washindi.

Awali kabla ya mashindano hayo ya michezo, yalianza mazoezi ya viungo.

Mazoezi ya viungo yakiendelea.

Mazoezi ya viungo yakiendelea.

Mazoezi ya viungo yakiendelea.

Mazoezi ya viungo yakiendelea.

Mazoezi ya viungo yakiendelea.

Mazoezi ya viungo yakiendelea.

Jogging katika mitaa mbalimbali ya mjini Shinyanga kutoka Bwalo la Polisi kueleke kwenye uwanja wa michezo vya Jeshi la Polisi Kambarage Mjini Shinyanga, kwa ajili ya Bonanza la michezo.

Jogging ikiendelea katika mitaa mbalimbali ya Mjini Shinyanga.

Jogging ikiendelea katika mitaa mbalimbali ya Mjini Shinyanga.

Jogging ikiendelea katika mitaa mbalimbali ya Mjini Shinyanga.

Jogging ikiendelea katika mitaa mbalimbali ya Mjini Shinyanga.

Jogging ikiendelea katika mitaa mbalimbali ya Mjini Shinyanga.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, kulia, akikabidhi Kombe kwa washindi wa Mashindano ya Bonanza la Michezo, Klabu ya Mazoezi ya Mjini Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFCS) baada ya kuwashinda Klabu ya Mazoezi ya Kahama, akipokea Kombe hilo ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Mazoezi Shinyanga Lucas Morn.

Wanachama wa Klabu ya mazoezi ya Polisi Jamii Fitness Center (PJFC) ya Mjini Shinyanga wakishe elekea ushindi kwa kubeba kombe juu.

Na Marco Maduhu-Shinyanga.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464