Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Wiliam Jijimya akienesha kikao cha Baraza la Madiwani.
Suzy Luhende,Shinyanga
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wameiomba serikali kuu iwasikie kilio chao cha uhaba wa watumishi sekta ya afya ambapo Zahanati nyingi na Vituo vya afya hazina watumishi wa kutosha kuhudumia wagonjwa.
Hayo wameyasema leo kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, ambapo wamesema wanaupungufu mkubwa wa watumishi wa idara mbalimbali lakini wameiomba serikali iwape kipaumbele zaidi kwa kuwaletea watumishi wa sekta ya afya kwani wananchi wanapata shida sana wanapoenda zahanati na kukuta mtumishi mmoja pekee.
Baadhi ya madiwani hao Ferdinand Mpogomi wa kata ya Seke bugolo na Edward Manyama wa kata ya Kiloleli wamesema hali ni mbaya katika sekta ya afya wagonjwa wakiwemo kina mama waja wazito wanapoenda kujifungua katika kituo cha afya ama zahanati wanasubiliana hali ambayo inahatarisha maisha kwa kuchekeweshwa kupatiwa huduma kwa wakati.
"Tunaiomba serikali ya mama yetu mama Samia Suluhu itusikie kwa hiki kilio chetu ituhurumie na iwahurumie wagonjwa na kina mama wanaojifungua itupe upendeleo kwani kila zahanati iliyopo au kituo Cha afya Kuna upungufu wa watumishi angalau wakiwepo watatu kila zahanati ama kituo Cha afya itasaidia lakini unaweza ukakuta mtumishi mmoja tu mzigo unawelemea na kulalamikiwa hahudumii wagonjwa"amesema Mpogomi.
Diwani wa kata ya mwakipoya Thabisa Sadiki amesema serikali iwasaidie kuwapelekea watumishi kwani kina mama wajawazito wanapokutana wengi katika vituo vya afya na kukuta mtumishi mmoja wanapata shida sana wakati mwingine wanaojifungua kwa wakati mmja hivyo mtumishi anashindwa kuwahudumia kwa wakati mmoja.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Underson Mandia amesema kweli hali ni mbaya watumishi hawatoshi katika sekta za kilimo mifugo walimu wa kile na watendaji wa vijiji kila diwani wa kata anainuka na kuomba watumi serika isikie kilio cha madiwani iweke kipaumbele angalau waletwe watumishi wa sekta ya afya ili kuokoa wananchi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Sabinus Chaula ambaye ni afisa mifugo wa wilaya hiyo amesema tatizo la upungufu wa watumishi ni la nchi nzima hivyo serikali inalifuatilia suala hili ili iweze kuajili watumishi, hivyo aliwaomba wawe na uvumilivu.

Diwani viti maalumu wa halmashauri ya Kishapu Helena Baraza akichangia hoja kwenye baraza hilo.
Diwani wa kata ya Seke bugolo Ferdinand Mpogomi akichangia Hoja kwenye Baraza hilo.