Diwani wa Songwa wilayani Kishapu Abdul Ngolomole akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani.
Na Suzy Luhende, KISHAPU
Madiwani wa halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga wameiomba serikali itengeneze miundombinu ya barabara, kwani wakati wa masika barabara hazipitiki hali ambayo imekuwa ikisababisha wagonjwa kupelekwa hospitali kwa kutumia mkokoteni wa ng'ombe na kuhatarisha maisha ya wagonjwa.
Hayo wameyasema leo kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, ambapo wamesema hali ya barabara inayotoka Migunga, Mwataga kwenda Isoso wakati wa masika hazipitiki,hivyo anapotokea mgonjwa inabidi awekwe kwenye mkokoteni wa ng'ombe ili apelekwe hospitali.
Diwani wa Kata ya Mwataga halmashauri ya Kishapu Matungwa Daudi na diwani wa Kiloleli wamesema wananchi wanapata shida sana wanapougua ili waweze kuwahi hospitali hali ambayo wengine wanapoteza maisha wakiwa wanapelekwa hospitali kutokana na kukosa usafiri wa gari ama pikipiki ya kuwawahisha kupata matibabu.
'Tunaiomba serikali itusaidie juu ya hili kutokana na barabara kuwa mbovu hazipitiki mwaka juzi kuna mama mmoja alipoteza maisha kutokana na kukosekana kwa barabara, hivyo tunaomba barabara zitengenezwe ili kunusuru afya za wananchi,amesema Daudi.
Diwani kata ya Songwa Abdul Ngolomole amesema barabara za Songwa na Mondo wanalima Sana mazao ya mpunga na dengu ni barabara za kiuchumi lakini nimbovu hivyo Wafanyabiashara wanashindwa kupitisha mazao yao kwa sababu barabara hazipitiki na biashara ya mazao hayo inafanyika Maganzo.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo amesema kero za barabara zinaonekana zipo kila kata hivyo Tarura iliangalie vizuri suala hili kwani wananchi wanahitaji barabara waweze kupata matibabu kwa muda na waweze kusafirisha mazao yao kwa wakati.
Kwa upande wake meneja Tarura wilaya ya Kishapu Samson Pamphili amesema serikali ilikuwa imetenga Sh 800.9 milioni lakini baada ya kuona changamoto za barabara ni nyingi iliongeza fedha ikafika Sh 2.4 Bilioni ambazo zimeelekezwa kuishirikisha halmashauri na mbunge, na fedha hizo zimeelekezwa kwenye barabara ambazo hazipitiki kabisa zipewe kipaumbele.
"Sh 500 milioni zitatengeneza barabara la kata ya Talaga la Nhobola kwenda Muguda kata ya Kiloleli ambalo litakuwa ni kilomita 18 Sh 540 milioni zitatengeneza barabara la kata ya Itilima linalopakana na barabara la manispaa ya Shinyanga Sh 130 milioni zitatengeneza barabara ya Bupigi, Mwamala A na Mwamala B pia Sh 90 milioni zitatengeneza barabara ya Busulwa inayounganishwa na manispaa ya Shinyanga ambayo ni kilomita 4.3.jumla zitatumika Sh 1.5 bilioni na Sh 800 milioni zitatumika kwa ajili ya barabara zilizopitishwa kwa ajili ya kukarabati"amesema Pamphili.

Diwani wa Kilole, akichangia hoja kwenye Baraza la Madiwani Kishapu.
Diwani wa Songwa wilayani Kishapu Abdul Ngolomole akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Anderson Mandia, akiendesha kikao cha baraza la madiwani Kishapu.