SABABU MSHITAKIWA KESI YA SABAYA AOMBA KUJITOA

Mshtakiwa namba tatu katika kesi ya unyang’anyi wakutumia silaha, Daniel Mbura ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imuachie huru arudi mtaani akapambane na majukumu ya kujenga taifa kwa kuwa taarifa zote za hati ya mashitaka katika kesi hiyo sio zake. 

Mbura anashitakiwa pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya pamoja na mshirika mwingine Sylvester Nyengu.

Mbura ameiambia Mahakama Agosti 23 kuwa yeye anaitwa Daniel Laurent Mbura (31), Mkulima, Mdigo, Mkazi wa Shamsi nakwamba hati ya mashitaka imekosea kuanzia majina yake, umri, kabila, shughuli anayofanya na sehemu anayokaa.

Katika hati ya Mashtaka ya kesi ya jinai namba 105 ya mwaka huu imemtambulisha yeye kama Daniel Gabriel Mbura (38), Mburu, Mfanyabiashara, mkazi wa Boma Ng’ombe Hai. Mbura amesema kesi hiyo ni ya uongo na imetengenezwa. Hakusema kwa nini imetengenezwa na kwanini awe yeye, lakini ametaka mahakama iitupilie mbali kesi hiyo.

“Kwa heshima kubwa naomba mahakama ifute mashtaka haya dhidi yangu kwa kuwa ni uongo. Naomba mahakama iniachie niende nikapambane na majukumu ya kujenga taifa,” alisema.

Kesi Inandelea kwa mshtakiwa huyo kutoa utetezi

Awali mawakili wa utetezi walipinga kesi hiyo kwa madai kwamba hati ya mashitaka ya mshitakiwa namba moja Lengai Ole Sabaya ilikuwa imekosewa. Mawakili wa Jamhuri waliiomba mahakama kubadili hati ya mashitaka baada ya kubaini ilikuwa imeandikwa Lengai Ole Sayaba. Hata hivyo baada ya mvutano baina ya mawakili wa pande zote mbili kudumu kwa zaidi ya saa mbili Mahakama iliridhia ombi la Jamhuri la kubadili majina katika hati ya mashitaka.
 
SOMA ZAIDI HAPA  CHANZO HABARI LEO






Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464