Na Marco Maduhu, SHINYANGA
SERIKALI mkoani Shinyanga, imeyataka mashirika yasiyo ya kiserikali, kuendelea kutoa elimu kwa jamii, ili kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike, ikiwamo kupewa mimba za utotoni, na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi VVU.
Amesema Mkoa wa Shinyanga upo mstari wa mbele kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali, ili kuhakikisha jamii ina mthamini mtoto wa kike na kumpa ulinzi wa kutosha, juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, ambavyo vinaweza kumuingiza kwenye matatizo na kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi VVU.
“Nawapongeza Shirika la Familiy Health International (FHI360) kupitia mradi wa EPIC, chini ya wafadhili shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa USAID na REPFAR, pamoja na asasi za kiraia kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuchangia na kusaidia juhudi za Serikali yetu kupambana na janga la Ukimwi hasa kwa Mabinti katika mkoa wetu wa Shinyanga,”amesema Dk, Sengati.
“Takwimu zinaonyesha hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wasichana balehe na wanawake vijana ni asilimia 15.3, ikilinginishwa na vijana wakiume, ambapo ni asilimia 6.6, kwa mujibu wa Tanzania HIV impact Survey ya mwaka 2016-17, Pia takwimu zinaonyesha asilimia 27 ya wasichana balehe wenye umri miaka 15-19 wamepata watoto au ujauzito,”ameongeza.
Pia, ametaja Takwimu za Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi mkoani humo, kuwa ni asilimia 5.9, ambapo kitaifa ni asilimia 4.9, na kubainisha watahakikisha wanazishusha hadi kufikia asilimia 2.
Kwa upande wake Meneja mradi wa EPIC kutoka Shirika hilo la FHI 360 Dk. Shinje Msuka, amesema mradi huo umejikita kudhibiti janga la virusi vya ukimwi kwa wasichana walio katika rika balehe, na wanawake vijana.
Amesema katika Mkoa wa Shinyanga, mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri Tano, ambazo ni Manispaa ya Shinyanga, Kahama, Ushetu, Msalala, na wilayani Shinyanga, na kubainisha katika mkoa mzima wametoa baiskeli 242 thenye tahamani ya Sh. milio 61.5 ili kutatua changamoto ya usafiri kwa wawezeshaji wasichana kiuchumi, na kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Aidha, amesema tangu mradi huo uanze kutekelezwa mkoani Shinyanga February mwaka jana, kupitia mpango wa Dreams, wameshawafikia wasichana 100,000 na kupatiwa huduma mbalimbali zinazotolewa na mradi, ambapo wasichana 20,000 wameshapewa huduma za uzazi wa mpango, uchunguzi magonjwa ya zinaa, na upimaji wa VVU kwa hiari.
Alisema, mradi huo unatekelezwa kwa kutoa elimu kwa wasichana, juu ya afua za afya ya uzazi wa mpango, kupima VVU, pamoja na kuwapatia elimu ya ujasiriamali ili wajikwamue kiuchumi, na kutojiingiza kwenye makundi mabaya, na kufanya ngono katika umri mdogo na kuambulia Ukimwi.
Nao baadhi ya wawezeshaji hao kiuchumi, akiwamo Rachel Maige, alisema Baiskeli hizo zitakuwa msaada kwao, kufika maeneo mengi na kutoa elimu ya kujitambua kwa wasichana, ili kuepukana na mimba, ndoa za utotoni, na maambukizi ya VVU.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, akizungumza kabla ya kukabidhi baiskeli hizo.
Meneja mradi wa EPIC unaotekelezwa na FHI360 Dk. Shinje Msuka, akielezea namna mradi huo unavyotekelezwa mkoani Shinyanga katika Halmashauri Tano.
Mwezeshaji wasichana kiuchumi Sophia Chamba, akieleza namna baiskeli hizo zitakavyo wasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao.
wajumbe wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya baiskeli kwa wazeshaji wasichana kiuchumi.
wajumbe wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya baiskeli kwa wazeshaji wasichana kiuchumi.
wajumbe wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya baiskeli kwa wazeshaji wasichana kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk, Philemon Sengati, wapili kushoto, akikabidhi baiskeli kwa Mwezeshaji wasichana kiuchumi Rachel Maige, wakwanza kulia, akifuatia na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary na kushoto ni Meneja wa Mradi wa EPIC unaotekelezwa na FHI360 Dk, Shinje Msuka.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, akiendesha baiskeli kabla ya kuzikabidhi.
Zoezi la kukabidhi baiskeli likiendelea.
Wazeshaji wasichana kiuchumi wa rika balehe na wanawake vijana, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kukabidhiwa baiskeli.
Na Marco Maduhu-Shinyanga.