Daktari wa watoto ambaye anatibu wa watoto wenye Utapiamlo katika kituo cha Afya Bugisi kilichopo Didia wilayani Shinyanga Zacharia Msumari kushoto, akimweleza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko sababu za watoto wilayani humo kuendelea kupata Utapiamlo.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
DAKTARI wa watoto ambaye anatibu watoto wenye tatizo la Utapiamlo katika kituo cha Afya Bugisi kilichopo Didia wilayani Shinyanga Zacharia Msumari, ametaja sababu za wazazi kutopanga uzazi wa mpango, ndiyo chanzo cha watoto wilayani humo kupata Utapiamlo.
Dk. Msumari akizungumza juzi kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, alipotembelea kwenye kituo hicho kwa ajili ya kutoa elimu kwa akina mama ili kukabiliana na tatizo la utapiamlo kwa watoto.
Alisema tatizo la watoto wilayani Shinyanga, kuendelea kukabiliwa na tatizo la Utapiamlo, linatokana na wazazi kuzaa watoto mfululizo bila ya kufanya uzazi wa mpango, na hivyo kushindwa kuwanyonyesha maziwa ya mama ipasavyo, sababu ya kupata ujauzito mwingine.
“Mkuu wa wilaya ukiangalia baadhi ya watoto ambao wana Utapiamlo, wanasababishwa na wazazi wao kutowanyonyesha maziwa ya mama ipasavyo, ambapo wamekuwa wakiachisha kunyonya wakiwa bado wadogo, kutokana na wazazi wao kubeba ujauzito,”alisema Dk. Msumari.
“Maziwa ya mama kwa mtoto mdogo yana virutubisho mwilini mwake, hivyo mtoto akiyakosa ana kuwa katika hatari kubwa ya kupata Utapiamlo, na ndiyo maana watoto wengi unao waona hapa Hospitalini hawakunyonya maziwa ya mama ipasavyo,”aliongeza.
Aidha, alisema kwa kipindi cha miezi Mitano, kuanzia Februari 15 hadi Agost mwaka huu, walipokea watoto 73 wakiwa na Utapiamlo na waliwapatia matatibu, na mpaka sasa wanawatoto wa Nne tu, ambao wanaedelea kuwa hudumia ili kuimarisha afya zao.
Naye, Ofisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Saidi Mankiligo, alisema hali ya utapiamlo kwa watoto wilayani humo ipo wastani ambapo watoto wenye udumavu ni asilimia 33, ikilinganishwa na takwimu za kitaifa asilimia 36.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, aliwataka wazazi wilayani humo kufuata ushauri wa wataalam wa afya, kwa kunyonyesha watoto wao maziwa ya kutosha, ili kuwaepusha na tatizo hilo la utapiamlo, pamoja na wale waliofikisha miezi ya kuanza kura wawapatie lishe bora yakiwamo na matunda.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia, akiangalia Mtoto ambaye ana tatizo la Utapiamlo ambaye anapatiwa matibabu katika kituo cha Afya Bugisi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akisisitiza wazazi kunyonyesha watoto wao maziwa ya mama ili kuwaepusha na tatizo la Utapiamlo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia, akisisitiza wazazi kunyonyesha watoto wao maziwa ya mama ili kuwaepusha na tatizo la Utapiamlo.