KATAMBI ATOA VITABU VYA SAYANSI NA KOPYUTA SHULE ZA SEKONDARI ,, AONYA MATUMIZI DAWA ZA KULEVYA KWA WANAFUNZI.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Patrobasi Katambi, kushoto, akimkabidhi Kopyuta Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Malale Sawaka, kati ya Kopyuta Tano na Printer Moja ambazo ametoa shuleni hapo.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA.



NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, ametoa vitabu vya Sayansi na Kopyuta kwa shule za Sekondari Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza leo wakati wa kubidhi vitabu hivyo na Kopyuta, akiwa katika Shule ya Sekondari Chamaguha na Ngokolo, amesema ametoa vifaa hivyo vya masomo ili kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi.

Amesema kipindi cha Kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2020, aliahidi kutatua changamoto mbalimbali katika jimbo hilo la Shinyanga Mjini, ikiwamo Sekta ya Afya, miundombinu ya barabara pamoja na Elimu, ambapo kwa sasa ameanza utekelezaji wa ahadi zake kwa kila sekta, na kutoa vifaa hivyo vya masomo ya Sayansi.

“Kipindi cha kampeni tulikuwa tuna ahidi, na sasa tunatekeleza yale yote tuiyokuwa tukinadi kwenye ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi CCM yenye kurasa 303, na tutatekeleza ahadi zote kwa wananchi,”alisema Katambi.

“Nimetoa vitabu vya masomo ya Sayansi 324 na vitabu vya miongozi ya walimu, kwa shule za Sekondari Nne za Manispaa ya Shinyanga, ambazo ni Chamaguha, Oldshinyanga, Mwamalili na Ibadakuli, vitabu 81 kwa kila shule, na katika shule hii ya Sekondari Ngokolo ninatoa Kopyuta Tano, na Printer Moja,”aliongeza.

Aidha alisema ametoa vitabu hivyo, ili kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi, na kuiona Shinyanga inapata wataalam wake wa baadae na kuwaletea maendeleo, huku akiwataka wanafunzi wakijike kwenye masomo, yao na kuacha kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na ngono katika umri mdogo.

Naye, Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Malale Sawaka, na Mkuu wa Shule ya Sekondari Chamaguha Mwesa Martini, kwa nyakati tofauti walimpongeza Mbunge huyo kwa kuwapatia vitabu hivyo pamoja na Kopyuta, vifaa ambavyo zitachochea ukuaji wa elimu na kufaulisha wanafunzi wengi wa masomo ya Sayansi.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Patrobas Katambi, akizungumza kwenye Hafla ya kugawa Kopyuta katika Shule ya Sekondari Ngokolo na kueleza kuwa anatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo yenye kurasa 303.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune, akizungumza kwenye zoezi la Katambi la kukabidhi Vitabu na Kopyuta kwa shule za Sekondari Manispaa ya Shinyanga.

Diwani wa Ngokolo Victor Mkwizu, akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya Kopyuta katika shule ya Sekondari Ngokolo kutoka kwa Mbunge Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Malale Sawaka, akishukuru kupewa Kopyuta hizo.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Chamaguha Mwesa Martini, akishukuru kupewa vitabu 81 vya Masomo ya Sayansi.

Katambi, mkono wa kulia ,akikabidhi Vitabu 81 vya Masomo ya Sayansi kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Chamaguha Mwesa Martini.

Katambi, kushoto, akikabidhi Kopyuta kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Malale Sawaka.

Katambi, akikabidhi Printer kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Ngokolo.

Katambi akipiga picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo, huku wakishikilia Kopyuta, kulia ni Diwani wa Ngokolo Victor Mkwizu.

Katambi akiwasihi Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo, kusoma kwa bidii na kutojiingiza kwenye Madawa ya Kulevya na Mapenzi katika umri mdogo bali wasome ili watimize malengo yao.

Awali Katambi, akijionea na kusikiliza namna wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Jinsi wanavyosoma Masomo ya Sayansi kwa vitendo.

Masomo ya Sayansi kwa vitendo yakiendelea.

Katambi akipiga picha ya Pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo, ambao walifanya vizuri kwenye mashindano ya masomo ya Sayansi na kubeba Tuzo, yaliyofanyika katika shule ya Savanna mwaka huu.

Awali vijana wa Skauti katika Shule ya Sekondari Ngokolo, wakimvalisha Katambi Skafu, alipowasili Shuleni hapo kukabidhi Kopyuta Tano na Printer Moja.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.





















































































































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464