Na Marco Maduhu, SHINYANGA
LIGI ya Mpira wa miguu ya Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew, imefika tamati leo, ambapo Timu ya Kapine imeibuka na ushindi na kutwaa zawadi ya Jezi na pesa Taslimu Sh.50,000.
Fainali ya Mchezo huo umechezwa kati ya Timu ya Kapine na Kolandoto, ambayo imechezwa kwenye uwanja wa michezo Kolandoto, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mfanyabiashara maarufu mjini Shinyanga Gilitu Makula, na Kapine aliibuka na ushindi wa Goli Mbili kwa moja.
diwani wa kolandoto mussa andrew, alisema alianzisha mashindano hayo, kwa kushirikisha timu Nane za vijana kutoka kwenye Vitongoji vya Kata hiyo, ikiwamo ya Mwasimba, Wame, Mwamala, Kabondo, Luhumbo, Mwanubi, Kapine, pamoja na wenyeji Kolandoto, lengo likiwa ni kuibua vipaji vya vijana.
"Lengo la ligi hii ni kuibua vipaji vya vijana wa Kata hii ya Kolandoto, sababu mpira ni ajira, pamoja na kuimarisha afya zao," alisema Andrew.
"Katika Mashindano haya Mshindi wa kwanza ambaye ni Timu ya Kapine, tumempatia Jezi na Sh.50,000, Mshindi wa Pili Kolandoto tumewapa Mpira na sh.30,000, Mshindi wa Tatu Mwamala tumewapa Sh.30,000," aliongeza.
Aidha, alisema pia wametoa zawadi ya pesa kwa wachezaji ambao waliibuka washindi kwenye ligi hiyo wakiwamo wachezaji bora, na timu yenye nidhamu.
Naye, Mgeni Rasmi Gilitu Makula, alimpongeza Diwani kwa kuanzisha ligi hiyo, ambapo ameona vipaji vingi, na kuahidi kuendelea kumuunga mkono diwani huyo, ili kuendelea kuibua vipaji vya vijana na hata kuunda timu ya Kata.
Kwa upande wake Katibu wa wazazi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Migeyo Ally, alisema kitendo alicho kifanya diwani huyo ni utekelezaji wa ilani ya chama hicho, ambyo ina hamasisha michezo, na kutoa wito kwa madiwani wengine kuiga mfano huo.
Mgeni Rasmi Gilitu Makula, ambaye ni Mfanyabiashara akizungumza kwenye hitimisho la Ligi ya Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew.
Mgeni Rasmi Gilitu Makula, ambaye ni Mfanyabiashara, akitoa Nasaha kwa vijana kabla ya kuanza mchezo wao wa Fainali.
Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew, akielezea madhumuni ya kuanzisha Ligi hiyo ya vijana kwenye Kata yake.
Katibu wa wazazi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Migeyo Ally, akizungumza kwenye Hitimisho la Ligi ya Diwani Kolandoto Mussa Andrew.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, Samweli Jackson, akizungumza kwenye Hitimisho la Ligi hiyo ya Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew.
Awali Mgeni Rasmi Gilitu Makula, akikagua wachezaji wa Timu ya Kapine, kabla ya Fainali kuanza.
Rasmi Gilitu Makula, akikagua wachezaji wa Timu ya Kolandoto, kabla ya Fainali kuanza.
Soka likisakatwa kwenye Fainali ya Ligi ya Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew.
Soka likiemdelea kusakatwa kwenye Fainali ya Ligi ya Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew.
Soka likiemdelea kusakatwa kwenye Fainali ya Ligi ya Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew.
Soka likiemdelea kusakatwa kwenye Fainali ya Ligi ya Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew.
Soka likiemdelea kusakatwa kwenye Fainali ya Ligi ya Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew, ambapo Timu ya Kapine, waliibuka na ushindi wa Goli Mbili kwa Moja dhidi ya wenyeji Kolandoto.
Wananchi wa Kolandoto wakiangalia mchezo wa fainali Ligi ya Diwani wao.
Wananchi wa Kolandoto wakiangalia mchezo wa fainali Ligi ya Diwani wao.
Wananchi wa Kolandoto wakiangalia mchezo wa fainali Ligi ya Diwani wao.
Viongozi mbalimbali wa Kata ya Kolandoto wakiangalia Fainali ya Ligi wa Diwani wa Kata hiyo.
Mashabiki wa Timu ya Kapine wakishangilia Goli la Pili ambalo lilifungwa na Frank Samweli kipidi cha pili na ndiyo lililowapa ushindi.
Ushangiliaji wa Goli ukiendelea.
Mgeni Rasmi Gilitu Makula, kushoto, akiwa na Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew, wakionyesha zawadi ya Jezi.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, Samweli Jackson, kulia, akiwa na viongozi mbalimbali wakionyesha zawadi za Jezi.
Mgeni Rasmi Gilitu Makula, ambaye ni Mfanyabiashara Maarufu Mjini Shinyanga , akitoa Zawadi kwa Timu ya Kapine, mara baadha ya kuibuka na ushindi kwenye Fainali ya Ligi ya Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew, wakwanza kulia, akipokea Zawadi ya Jezi na Pesa Sh.50,000 kiongozi wa Timu hiyo Msweden Rafael.
Mgeni Rasmi Gilitu Makula, kulia, akitoa Zawadi ya Mpira kwa mshindi wa Pili wa mashindano hayo Timu ya Kolandoto na Pesa Sh.30,000.
Katibu wa Wazazi wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Migeyo Ally, akitoa Zawadi kwa washindi wengine katika Ligi hiyo, wakiwamo wachezaji bora, na Timu yenye Nidhamu.
Zawadi zikiendelea kutolewa.
Na Marco Maduhu-SHINYANGA.