Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Steven Samandari (25) Mkazi wa Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambaye ni mlinzi wa nyumba ya kulala wageni (Guest house), amedaiwa kuuawa kwa kuchomwa na kisu tumboni, na mtu ambaye alidaiwa kumkamata wakati aliporuka uzio wa nyumba hiyo ya kulala wageni, kwa ajili ya kufuatilia wanawake kufanya nao mapenzi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, akitoa taarifa hiyo leo kwa vyombo vya habari, alisema tukio hilo limetokea Septemba11 mwaka huu Majira ya saa 8 usiku katika Mtaa huo wa Nyanhanga wilayani Kahama.
Alisema mtu huyo ambaye bado hajafahamika, alikamatwa na Mlinzi huyo wakati aliporuka uzio wa Gesti, wakati alipokuwa akifuatilia wahudumu wa bar kwenye Gesti hiyo ambayo Kamanda hakuitaja, kwa lengo la kufanya nao mapenzi, ndipo alipochomoa kisu na kumchoma tumboni na kusababisha mauaji.
“Katika eneo la tumekuta kisu kikiwa tumbo kwa mlizi huyo, ambaye kwa sasa ni marehemu,”alisema Kyando.
Aidha, alisema Jeshi hilo linamshikilia Mhudumu wa Bar Fatuma Charles (22), kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo, na kumbaini mhusika wa mauaji hayo, ili hatua kali za kisheria zipate kuchukuliwa dhidi yake.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464