Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Shirika la Citizens 4 Change (C4C) pamoja na Women Fund Tanzania Trust(WFT) wameitoisha kikao cha pamoja cha wadau zaidi ya 70 kutoka katika kata 18 za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wanaoshughulikia masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.Wadau hao walipatikana baada ya kutambulishwa na wananchi wenzao zaidi ya 1200 waliohojiwa kuhusu watu wa muhimu katika maisha na mazingira yao.
Kikao hicho kimejumuisha viongozi wa serikali pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya ulinzi na usalama kwa watoto pamoja na wanawake.Kikao kililenga kuwaleta wadau pamoja ili kujadili mchakato bora wa kukomesha ukatili dhidi ya watoto na wanawake unaozingatia uhalisia wa mazingira yao.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale amewaomba wadau hao kushirikiana na serikali katika kukomesha ukatili kwa wanawake na watoto .Kadhalika Bwana Ngwale aliwasisitiza wadau kuhakikisha kuwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga inakuwa mfano wa wilaya zingine katikakutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“Ninyi sasa ni viongozi tunaomba mtatusaidia sana ili Halmashauri yetu iwe mfano katika kutokomeza maswala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.Tunataka viongozi wengine kutoka katika wilaya zingine waje kujifunza kwenu.Naomba mjitahidi kushirikiana na serikali”,alisema
Kwa upande wake Dkt. Kate McAlphine ambaye ni Mkurugenzi na mtafiti kutoka Shirika la citizen for changealisema lengo la Shirika hilo kufika wilaya ya Shinyanga na kushirikiana na wadau wa Shinyanga katika mradi wa kukomesha unyanyasaji dhidi ya watoto na wanawake kutumia ubunifu wa kitafti.Mradi huu unafanywa na Citizen 4 Change kwa kushirikiana na Shirika la Women Fund Tanzania Trust(WFT) pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)

"Nia yetu ni kushirikiana na watu wa wilaya ya Shinyanga ili kuhakikisha ukatili sasa basi.Kadhalika tunataka kutengeneza kwa pamoja na wadau njia nzuri ya kuwalinda watoto na wanawake.Njia ipo mioyoni mwetu"Alisema Dkt.Kate
Shirika la Citizen For Change linatumia njia ya ujumbe mfupi wa simu kuwasiliana na watu wenye nia ya kulinda watoto na wanawake dhidi ya unyanyasaji.Dkt Kate alifafanua kuwa huduma hiyo ya simu ni bure na mtu yeyote mwenye nia ya kulinda watoto na wanawake anaweza kujiunga kwa kupiga*149*46*11#
Kwa upande wake,Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Muhoja amesema baadhi ya maeneo ukatili umepungua ambapo amesema changamoto kubwa ni mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni amewataka wananchi kuacha matendo ya ukatili .
“Katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa sasa hali ya ukatili imepungua lakini changamoto kubwa ni mimba na ndoa za utotoni .Nitoe wito kwa wananchi tuache matendo ya ukatili kwa sababu ukatili hauna faida.Pia pale ukatili unapofanyika,majirani watoe taarifa mapema sehemu husika ili hatua zichukuliwe",amesema.