Mwanafunzi John Malasi kutoka Shule ya Little Treasures, kulia (mwenye nguo nyekundu), akimkabidhi msaada wa vitu mbalimbali Mtoto Mwenzake Mwenye Ualbino Lukas Magali kwa niaba ya wenzake ambao wanalelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Na Marco Maduhu, Shinyanga.
Wanafunzi wa shule msingi na sekondari Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga wametoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulea watoto wenye ulemavu kilichopo Buhangija Mjini Shinyanga.
Msaada huo umetolewa leo Alhamisi Septemba 30,2021 na wanafunzi wa Shule hiyo, wakiwa wameambatana na Mkuu wa Shule ya Sekondari Little Treasures Charles Mwita.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mwita alisema wameamua kusaidia watoto hao wenye ulemavu, ili kuonyesha wanafunzi wao namna ya kusaidia watoto au watu wenye uhitaji.
“Vitu ambavyo tumetoa kwa watoto hawa wenye ulemavu ni nguo, viatu, sabuni za kufulia, majora ya nguo, mchele kilo zaidi ya 50, na maharage kilo 40,” alisema Mwita.
Pia, aliwaasa watoto hao wenye ulemavu wasome kwa bidii, ili wapate ufaulu mzuri na kutimiza ndoto zao.
Nao watoto hao wenye ulemavu akiwemo Paulo Bundala, wameishukuru Shule hiyo kwa kuwapatia msaada huo, na kutoa wito kwa wadau wengine wajitokeze kuendelea kuwasaidia na kukidhi mahitaji yao.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Little Treasures Charles Mwita, akizungumza na watoto wenye ulemavu katika kituo cha Buhangija, wakati walipofika kuwapatia msaada.
Mwanafunzi wa Little Treasures Flaviana Felix, akizungumza kwenye kituo hicho cha kulea watoto wenye ulemavu Buhangija.
Mwalimu wa Little Treasures Jackline Mbwambom akizungumza na watoto wenye ulemavu katika kituo cha Buhangija.
Mwalimu Mlezi wa kituo cha kulea watoto wenye ulemavu Buhangija Stanley Wagala, akitoa shukrani ya kupata msaada huo.
Mwanafunzi John Malasi kutoka Shule Binafsi ya Little Treasures, kulia (mwenye nguo nyekundu), akimkabidhi msaada wa vitu mbalimbali Mtoto Mwenzake Mwenye Ualbino Lukasi Magali kwa niaba ya wenzake ambao wanalelewa katika kituo cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Little Treasures Charles Mwita, kushoto, akikabidhi Msaada kwa Mwalimu Mlezi wa kituo hicho cha kulea watoto wenye ulemavu mbalimbali cha Buhangija Stanley Wagala.
zoezi la makabidhiano likiendelea, ambapo kulia ni Mwalimu wa Shule ya Little Treasure Jackline Mbwambo.
Wanafunzi wa Little Treasure, wakiwa na msaada wa vitu vyao katika kituo cha kulea watoto wenye ulemavu Buhangija.
Wanafunzi wa Little Treasure, wakiwa na msaada wa vitu vyao katika kituo cha kulea watoto wenye ulemavu Buhangija.
Wanafunzi wa Little Treasure wakiwa wamechangamana na watoto wenye ulemavu, ili kuonyesha upendo kwao.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464
Na Marco Maduhu- Shinyanga.