Afisa Ardhi wa Manispaa ya Shinyanga Jacob Mwinuka, akizungumza na Wananchi wa Mtaa wa Majengo Mapya Manispaa ya Shinyanga ,
Na Suzy Luhenge, SHINYANGA
WANANCHI wa Mtaa wa Majengo mapya Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga, wameipongeza serikali kwa kuanzisha zoezi la upimaji viwanja kwa gharama nafuu ya Sh 130,000 , kwa ajili ya kuwapatia hati miliki ambayo itawasaidia kukopa fedha kwenye Taasisi mbalimbali za kibenki na kujikwamua kiuchumi.
Wakizungumza kwenye kikao cha elimu ya urathimishaji wa ardhi uliofanyika katika soko la mtaa wa Majengo mapya ,wananchi hao wamesema wanaishukuru serikali kwa kuanzisha utaratibu wa urasimishaji, hivyo mpango huo wameupokea kwa asilimia 100, na gharama za upimaji ambazo ni 130,000 watailipa bila shida.
Daniel Mayenga mkazi wa mtaa wa Majengo na Frola Joseph. wamesema utaratibu ulioletwa ni mzuri. kwani awali walikuwa wakitumia gharama kubwa, hivyo wamepà ta matumaini mapya watapimiwa viwanja vyao, na kupatiwa hati miliki na wataweza kukopa kiurahisi na kufanya biashara ili kujiendeleza kiuchumi.
"Suala hili tumelipokea kwa nguvu zote na kwa furaha sana, kwani tunaamini wananchi wote tutalipia fedha zilizotajwa na afisa mteule wa ardhi na tutaweza kurathimishiwa makazi yetu na kupata hati miliki ambayo itasaidia Mambo mengi yakiwemo ya mikopo na kufanya biashara ili kujiongezea uchumi wetu"amesema Fue Mlindoko mkazi wa mtaa wa Majengo mapya"
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ngokolo Victor Mkwizu. amesema wananchi kujitomeza kwa wingi kwenye kikao hicho, inaonekana walikuwa na kiu kubwa ya kupimiwa makazi yao na kuweza kupatiwa hati miliki, hivyo ni vizuri wananchi wakachangamkia fursa kwa wakati kwani kikomo cha zoezi hilo ni 2021.
"Tatizo hili limekuwa la muda mrefu lilikuwa halijatatuliwa, na hii ni moja ya Mambo tuliyoahidi kwenye mikutano yetu ya kampeni, kwamba tutatatua changamoto zilizopo, hivyo hili tumelitatua na mpango huu utatekelezwa kwa wakati, lakini wale waliopimiwa kwa mda mrefu wanatakiwa kwenda kuhakiki viwanja vyao katika ofisi ya ardhi, kwa sababu watu wengine walitumia majina mawili tofauti na yaliyomo kwenye kadi ya kitambulisho cha Taifa"amesema Mkwizu.
Naye Afisa mteule wa ardhi Manispaa ya Shinyanga Jacob Mwinuka, amesema mpango wa urathimishaji unasimamiwa na wananchi wenyewe, ambapo watalipia Sh 130, 000 kwa ajili ya upimaji, kununulia nondo, kokoto, na kulipa vibarua lakini eneo la kuabudia,kani msikiti hoteli watalipia Sh 500,000 na gharama ya kulipia hati miliki itategemea na ukubwa wa kiwanja chenyewe kiwanja cha 15 kwa 30 haitadhidi sh 150, 000 kwa ajili ya kupatiwa hati miliki.
Mwinuka amesema katika zoezi hilo, hakuna mtu atakayebomolewa na wale wenye hati watabaki na hati zao, hakuna atakayewagusa kwani upimaji upo kisheria, kwenye kupima unapimiwakama ulivyoendeleza kiwanja chako, katika mitaa mingi sehemu kubwa ina upimaji wa ofa, hivyo zoezi hili ni kwa ajili ya kurathimisha na kupatiwa hati miliki.
"Awali ili uipate hati miliki ilikuwa ulipie asilimia mbili 2.5 lakini kwa sasa gharama za hatimiliki zimeshuka ni asilimia 0.05 ya thamani ya ardhi, hivyo fikeni ofisi ya ardhi acheni kutuma vishoka, wengi mnasema gharama ni kubwa kwa sababu mnatumia vishoka hao wanawaibia"amesema Mwinuka.

Diwani wa Kata ya Ngokolo Victor Mkwizu akizungumza na Wananchi wa Mtaa wa Majengo mapya. kwenye zoezi la utoaji elimu ya upimaji wa viwanja.
Wananchi wa Mtaa wa Majengo Mapya, wakiwa kwenye zoezi la upewaji elimu ya upimaji wa viwanja.