Picha aihusiani na tukio
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
WATU watatu ambao ni wakazi wa Ngofila wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, wamefariki dunia Papo hapo, mara baada ya kugongwa na gari wilayani humo, wakiwa wamebebana mshikaki kwenye bodaboda.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, akitoa taarifa hiyo leo kwa vyombo vya habari, amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 1 asubuhi katika barabara ya Ngofila- Igulumbi Kata ya Ngofila wilayani Kishapu.
Kyando amewataja watu hao kuwa ni Konya Jiloma ambaye ni dereva wa bodaboda, Mipawa Njile na Ndosera Maganga ambao ni abiria waliokuwa wamebebwa mshikaki, ambapo waligongwa na gari aina ya Scania Lor lenye namba za usajili T.550 AJA, na kusababisha vifo vyao papo hapo.
“Chanzo cha Ajali hii ni mwendokasi wa dereva wa pikipiki, ambapo alilivamia gari hilo na kusababisha ajali ambayo imepelekea vifo vyao,”alisema Kyando.
Pia alisema Jeshi linamtafuta dereva wa gari hilo Salimu Abdalla, ambaye alikimbia kusikojulikana mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Aidha Kamanda alitoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani, na kuacha kuendesha mwendokasi, na kusababisha ajali za uzembe ambazo zina gharimu maisha ya watu.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464