BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA MADAWATI, VIFAA UJENZI WA SHULE VYA MILIONI 24 MASWA

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse (wa tatu kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge viti na meza kwa ajili ya shule wilayani Maswa.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya NMB Kanda ya Magharibi imetoa msaada wa madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka 2021.

Hafla fupi ya Makabidhiano ya vifaa hivyo imefanyika leo Jumatano  Oktoba 6,2021 katika shule ya Msingi Mwawayi wilayani Maswa ambapo Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse kukabidhi vifaa kwa Mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse amezitaja shule hizo kuwa ni shule ya Msingi Mwawayi iliyopo katika kata ya Nyalikungu ambayo imepata mabati 120 na vifaa vingine vya ujenzi vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 5.5 na shule ya msingi Inenwa iliyopo katika kata ya Buchamu ambayo wameipatia madawati 70 yenye thamani ya shilingi milioni 5.

Zingine ni shule ya Sekondari Mwabayanda ambayo wameipatia meza 50 na viti 50 vyenye thamani ya shilingi Milioni 5, shule ya Sekondari Bushashi imepata mabati zaidi ya 60,mbao na vifaa vingine vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 4.5 na shule ya Sekondari Itule ambayo wameipatia mabati 60,mbao na vifaa vingine vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 4.

“Mheshimiwa Mkuu wa wilaya leo tunakabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 24 kwa ajili ya kusaidia shule 5 wilayani Maswa na kukomboa michango ambayo ingepaswa kutolewa na wazazi. Tumetoa vifaa hivi ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka 2021 ikiwa na kauli mbiu ya Nguvu katika huduma ‘ The Power of service’”,amesema Magesse.

“Mwezi huu Oktoba dunia nzima inasheherekea Wiki ya Huduma kwa wateja ikiwa na kauli mbiu ya ‘Nguvu ya huduma’ The Power of service. Hivyo Mwaka huu sisi NMB tumeona ni vyema kusherehekea nanyi kama wateja wetu, ambao bila nyinyi kutuamini nan a fedh zenu, Benki ya NMB isingepata haya mafanikio tuliyonayo sasa hivi.

Kwa hiyo tumeamua kuchangia vifaa hivi nyenye thamani ya jumla ya shilingi Milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano. Tunatambua kuwa ni kupitia jamii ndipo wateja wengi wanapotoka,kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni sehemu ya utamaduni wetu”,ameongeza Magesse.

Amesema changamoto za sekta ya elimu Tanzania kwa NMB ni jambo la kipaumbele kutokana na ukweli kwamba suala la elimu ni nguzo kuu ya maendeleo kwa taifa lolote duniani huku akibainisha kuwa licha ya kwamba Serikali inafanya jitihada kubwa za kusaidia elimu kwa nguvu zote lakini NMB kama wadau wana wajibu wa kuunga mkono juhudi hizo za maendeleo kwa kusaidia jamii.

“Kupitia jamii hii tunayoisaidia, ndiyo imeifanya Benki ya NMB kuwa hapa ilipo na kubwa kuliko Benki yoyote hapa nchini tukiwa na Matawi zaidi ya 226,ATM zaidi ya 800 nchi nzima,NMB Wakala zaidi ya 9000 pamoja idadi ya wateja zaidi ya milioni 4 ambayo ni hazina kubwa ukilinganisha nyingine zote nchini. Pia tumezifikia wilaya zote nchini kwa asilimia 100”,ameeleza Magesse.

Amesema miaka kadhaa sasa Benki ya NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita zaidi kwenye miradi elimu (madawati, vifaa vya kuezeka), afya (vitanda na magodoro yake) na kusaidia majanga yanayoikumba nchi ya Tanzania.

Magesse amesema Benki ya NMB inaendelea kuboresha huduma za kibenki kwa njia ya mitandao ili kufikisha huduma za kibenki kwa wananchi wengi zaidi.

"Ili kuendelea kuwa mbele kwenye utoaj huduma kwa wateja wetu,mapema wiki hii tumezindua Hati ya kiapo cha huduma kwa mteja (Customer service charter) kuonyesha kwa vitendo nguvu ya huduma kwa wateja wetu. Ndani ya kiapo hicho tunatoa kiapo cha kutekeleza upatikanaji wa huduma ya uhakika,usikivu,uhakika wa kuaminika, weledi na nidhamu, na usalama wa taarifa za mteja",amesema.

Aidha amewaomba wananchi kuendelea kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki ya NMB ikiwemo Bima na Mikopo huku akieleza kuwa NMB itaendelea kuunga mkono juhudi za wadau wake wakubwa katika kuhakikisha kuwa changamoto za jamii zinapatiwa ufumbuzi katika kujenga afya bora na elimu bora kwa jamii ya Kitanzania.

Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada wa vifaa hivyo na kuahidi kuwa watavitumia kujenga miundo mbinu ya shule kama ilivyokusudiwa ili kuboresha mazingira ya kujifunzia shuleni.

“Tunawapongeza na kuwashukuru Benki ya NMB,wamekuwa wadau wakubwa katika sekta ya elimu na afya wilayani Maswa. Hizi shilingi milioni 24 mlizotoa siyo haba, zitasaidia kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo shuleni”,amesema Kaminyoge.

Mkuu huyo wa wilaya ameiomba Benki yaNMB kutochoka kusaidia jamii huku akiwaomba wazazi kuchangia nguvu zao kwenye ujenzi wa maboma ili serikali isaidie katika kuyapaua akieleza kuwa serikali pekee haiwezi kumaliza changamoto zote katika shule zote.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa, Paul Simon Maige amesema Benki ya NMB imeonesha mfano wa kuigwa katika kuondoa vikwazo vya maendeleo katika jamii na kuwaomba wananchi kutumia huduma zinazotolewa na Benki hiyo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge akizungumza wakati Benki ya NMB Kanda ya Magharibi ikitoa msaada wa madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu katika shule ya msingi Mwawayi kata ya Nyalikungu wilayani Maswa leo Jumatano Oktoba 6,2021. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa, Paul Simon Maige, kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge akizungumza wakati Benki ya NMB Kanda ya Magharibi ikitoa msaada wa madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu 
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse akizungumza wakati akikabidhi madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu 
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse akizungumza wakati akikabidhi madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu 
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse akizungumza wakati akikabidhi madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu 
akizungumza wakati Benki ya NMB Kanda ya Magharibi ikitoa msaada wa madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu 
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse (wa tatu kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge viti na meza kwa ajili ya shule wilayani Maswa.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse na Mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge (kulia) wakiwa wamekaa kwenye viti na meza vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya shule wilayani Maswa.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge ( wa pili kulia) madawati kwa ajili ya shule wilayani Maswa.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse, wanafunzi na Mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya shule wilayani Maswa.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse (aliyevaa tai) akimkabidhi mabati Mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge (wa pili kulia) yaliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule wilayani Maswa.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mwawayi wilayani Maswa akifuatilia matukio wakati Benki ya NMB ikikabidhi madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu 
Wanafunzi wa shule ya msingi Mwawayi wilayani Maswa akifuatilia matukio wakati Benki ya NMB ikikabidhi madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu 
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mwawayi. Bi Gaudencia Makolo akisoma risala ambapo amezitaja changamoto zinazoikabili shule hiyo kuwa ni pamoja na uhaba wa madarasa, matundu ya vyoo, kutokuwa na huduma ya maji, umeme na barabara.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Njile Magesse na Meneja wa Benki ya NMB tawi la Maswa, Hezron Okore wakiangalia kitu wakati wa hafla fupi ya NMB kukabidhi madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu. Kulia ni Meneja Mahusiano Serikali na Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Bi. Vivian Nkhangaa.
Wazazi wakifuatilia matukio wakati Benki ya NMB ikikabidhi madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu 
Wazazi wakifuatilia matukio wakati Benki ya NMB ikikabidhi madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu 
Wadau na Walimu kutoka shule mbalimbali wilayani Maswa wakifuatilia matukio wakati Benki ya NMB ikikabidhi madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu 
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Maswa,Hezron Okore (kushoto) na  Meneja Mahusiano Serikali na Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Bi. Vivian Nkhangaa wakiwa kwenye hafla fupi ya NMB kukabidhi madawati na vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati 240 na mbao 584 vyenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi wa shule tano wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464