MAHAFALI YA KWANZA SHULE YA AWALI NA MSINGI SAMUU YAFANYIKA SHINYANGA...TAZAMA PICHA HAPA


Wahitimu wa darasa la saba mwaka 2021 katika shule ya Msingi SAMUU wakiandamana kuelekea ukumbini wakati wa mahafali yao  Ijumaa Oktoba 8,2021.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’ yamefanyika ambapo jumla ya wanafunzi 15 wamehitimu darasa la saba huku wanafunzi 44 wakihitimu shule ya awali ‘Nursery’ tayari kabisa kuanza masomo ya darasa la kwanza mwaka 2022.

Mahafali hayo yamefanyika Ijumaa Oktoba 8,2021 katika shule ya Msingi Samuu (Samuu English Medium Pre and Primary School) iliyopo katika kijiji cha Mwagala kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Akisoma Risala, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi SAMUU, Moses Josiah amesema shule hiyo imeanzishwa Julai 13,2013 ikiwa na mwanafunzi mmoja na mwalimu mmoja ikiwa na madarasa mawili katika eneo la Ushirika Mjini Shinyanga na mwaka huu wanafunzi 15 wamehitimu elimu ya darasa la saba kati yao Wavulana ni 9 wasichana ni 6.

“Kuanzia mwaka 2013 shule ya Samuu imekuwa ikifanya vizuri sana kitaaluma kwa kufanya vizuri kwenye mitihani ngazi ya mkoa na kitaifa na imefanikiwa kukuza vipaji mbalimbali vya watoto na sasa tuna jumla ya wanafunzi 230 Tuna matarajio na mategemeo makubwa ya kufanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba tuliofanya mwaka huu..Tuendelee kuombeana ili matokeo yawe mazuri sana kama tulivyotarajia”,amesema Josiah.

Hata hivyo amesema shule ya Msingi SAMUU inakabiliwa na ukosefu wa umeme pamoja na barabara mbovu ya kutoka Bugweto hadi Mwagala hasa nyakati za masika kwa kuwa na utelezi na matope mengi hivyo kukwamisha maendeleo ya shule kutokana na .

“Ubovu huu wa barabara unasababisha magari kukwama na kuharibika na mbaya zaidi hali hiyo inahatarisha maisha ya wanafunzi na walimu wao kwa kuwa wakati mwingine imekuwa ikijaa maji kwenye maeneo korofi kama mvua ikinyesha kubwa kiasi cha magari kushindwa kupita”, amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Samuu English Medium Pre and Primary School, Bi. Salome Samaytu amesema Shule hiyo kwa sasa inaendelea na mkakati wa kujenga uzio/ukuta katika eneo la shule ya Msingi SAMUU kituo cha Mwagala ili kuboresha hali ya usalama.

Amesema pia wanaendelea kukamilisha ujenzi wa bweni la watoto wa shule ya msingi ambayo inatarajia kuanza Januari mwaka 2022.

“Shule ya Msingi SAMUU ina mkakati wa kuanza kufundisha masomo ya lugha ya Kifaransa, Kichina na Kijerumani ili kuipandisha hadhi ya kuwa ya kimataifa (International school). Pia tuna mpango wa kuongeza safari za kimasomo ‘Study tour’ ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujifunza kwa vitendo”,ameongeza.

Aidha amesema, katika kuwapa motisha wafanyakazi wake, wamewapatia zawadi ya mabati 20 kila mmoja wafanyakazi watatu (Mwalimu Linus Theobald na Grace Kasanga (mpishi) na Justine John ambaye ni dereva) ambao wamekuwa na ushirikiano mkubwa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2013 ikiwa na mwanafunzi mmoja pekee.

Mmiliki na Mkurugenzi wa SAMUU English Medium Pre and Primary School, Bw. Jonas Samaytu amewashukuru wazazi kwa kuiamini shule hiyo na kupeleka watoto wao na kulipa ada huku akiwahimiza wazazi kulipa ada kwa wakati.

Aidha amesema shule ipo kwenye mazingira na mandhari bora na wanafunzi hao waliohitimu elimu ya darasa saba wamewafundisha vizuri na wanaamini watafaulu vizuri katika mtihani wao wa taifa.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Ibadakuli Msabila Mabula ambaye alikuwa Mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo amesema serikali inatambua changamoto ya barabara na umeme katika shule hiyo na hivi karibuni itaanza kutatua changamoto hiyo.

Mabula ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi na walezi kulinda watoto na kuwapatia mahitaji yao muhimu na kutowaruhusu kuzurura hovyo mtaani.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Muonekano wa sehemu ya majengo ya shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wahitimu wa darasa la saba mwaka 2021 shule ya Msingi SAMUU wakiandamana kuelekea ukumbini wakati wa mahafali yao 
Wahitimu wa darasa la saba mwaka 2021 shule ya Msingi SAMUU wakiandamana kuelekea ukumbini wakati wa mahafali yao 
Wahitimu wa shule ya awali mwaka 2021 katika shule ya Awali na Msingi SAMUU wakiandamana kuelekea ukumbini wakati wa mahafali yao 
Katikati ni Mgeni rasmi wakati wa Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’ diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Mabula akiwasili katika shule hiyo. Wa pili kushoto ni Mmiliki na Mkurugenzi wa SAMUU English Medium Pre and Primary School, Bw. Jonas Samaytu. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Samuu English Medium Pre and Primary School, Bi. Salome Samaytu
Mmiliki na Mkurugenzi wa SAMUU English Medium Pre and Primary School, Bw. Jonas Samaytu akizungumza kwenye Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School.
Mkurugenzi Mtendaji wa Samuu English Medium Pre and Primary School, Bi. Salome Samaytu akizungumza kwenye Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi SAMUU, Moses Josiah akisoma risala  kwenye Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’
Wahitimu darasa la saba wakisoma risala kwenye Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’
  Mgeni rasmi , Diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Mabula akizungumza kwenye Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’
Mgeni rasmi , Diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Mabula na Mmiliki na Mkurugenzi wa SAMUU English Medium Pre and Primary School, Bw. Jonas Samaytu (kulia) wakikata keki kwenye Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’
Mgeni rasmi , Diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Mabula na Mmiliki na Mkurugenzi wa SAMUU English Medium Pre and Primary School, Bw. Jonas Samaytu akimlisha keki mhitimu wa shule ya awali kwenye Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’
Wanafunzi wakitoa burudani ya ngoma za asili kwenye Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’
Mgeni rasmi , Diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Mabula akiendelea na zoezi la kugawa vyeti kwa wahitimu wa shule ya awali kwenye Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’
Mgeni rasmi , Diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Mabula akiendelea na zoezi la kugawa vyeti kwa wahitimu wa darasa la saba kwenye Mahafali ya Kwanza katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464