Baadhi ya wanachama wa kikundi cha Whatsap Shytown VIP wakikabidhi Mabati kwa Mwanachama Mwenzao Steven Wang'anyi nyumbani kwake maeneo ya Kitangili ( aliyepo nyuma katikati).
Na Josephine Charles
SHINYANGA.
Kikundi cha Whatsapp cha Shinyanga VIP, kimetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi kwa ajili ya kuezeka nyumba ya mwanachama mwenzao Steven Wang’anyi, ambaye pia ni mwandishi wa habari, aliyepata ajali zaidi ya mwaka moja na nusu uliopita.
Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Mwenyekiti wa kikundi hicho Musa Ngangala, amesema vifaa walivyotoa ni Bati Bando 4, misumari kilo 20, na Sink moja la choo zenye thamani ya shilingi Millioni moja laki tano na elfu sitini(1,560,000/=)pamoja na pesa Taslimu shilingi Elfu 50 kwa ajili ya Kujikimu yeye na familia yake.
Ngangala ametumia nafasi hiyo kuwaomba watu wengine waungane na Kikundi cha Shy Town VIP kuweza kumsaidia mwenzao ambaye ameugua kwa kipindi kirefu kutokana na ajali aliyoipata na kusababisha kushindwa kufanya shughuli zake za uzalishaji mali.
Kwa Upande wake Mjumbe wa Kikundi hicho Bi. Neema Chacha, ametoa wito kwa wadau wengine watakaoguswa kumsaidia mwenzao kwa kuwa mahitaji bado ni mengi yakiwemo Simenti,Madirisha na milango kwa kuwa kipindi cha Mvua kimekaribia kuanza.
Naye Steven Wang’anyi ambaye amepokea msaada huo amewashukuru wanachama wenzake wa kikundi cha Shy Town VIP na kuwaombea kwa Mungu Baraka zaidi kwa kumsaidia vifaa vya kuezeka nyumba yake kutokana na matatizo aliyonayo,amesema alihamia kwenye nyumba yake ambayo haikuwa imeezekwa kwa takriban miezi mine kwa sababu alishindwa kulipa kodi ya nyumba aliyokuwa amepanga awali kabla ya kupata ajali ya Pikipiki kwa kuwa alikaa hospitali muda mrefu pasipo kuweza kufanya shughuli zozote za kujipatia kipato.
Aidha kikundi cha Shy town VIP kilianzishwa kwa lengo la kusaidiana katika shida na raha kwa wanachama wake na hadi sasa kina wanachama zaidi ya 250.

Zoezi la ushushaji Mabati likiendelea.
Zoezi la ushushaji Mabati likiendelea.