MTUMISHI UHAMIAJI SHINYANGA ANUSURIKA KIFO NYUMBA IKITEKETEA MOTO


Muonekano wa nyumba ikiwaka Moto

Na Marco Maduhu, SHINYANGA


FAMILIA ya Mtumishi idara ya uhamiaji mkoani Shinyanga Mwinji Nyombo ambayo ina watu Nane, wamenusurika Kifo mara baada ya nyumba ambayo wamepanga ya Mstaafu aliyekuwa Afisa Elimu mkoani Shinyanga Mohamed Kahundi, katika Mtaa wa Viwanja vya Mwadui Ndembezi Manispaa ya Shinyanga kuteketea kwa Moto.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 2 usiku, wakati wanafamilia hao wakiwa wote nyumbani, baadhi wakila chakula sebuleni, wengine wakiwa vyumbani, huku Mtumishi huyo wa Uhamiaji akifanya mazoezi chumbani kwake.

Nyombo akizungumza na Mwandishi wa Taarifa hii, alisema wakati akiendelea kufanya mazoezi, gafla akasikia kelele za mdogo wake akisema watoke nje haraka nyumba yao inawaka Moto, ndipo wote wakakimbilia nje na kunusurika kifo.

"Moto huu umeanza kuwaka kwenye chumba cha wavulana, na baada ya kutoka nje tukaanza kuomba msaada kwa majirani kuuzima, na jinsi ulivyokuwa kuuzima kwa maji na mchanga usingewezekana, ndipo tukaanza taratibu za kuomba msaada Jeshi la Zimamoto, lakini wamechelewa kufika na nyumba imeteketea yote, ila tuna shukuru wote tupo wazima," alisema Nyombo.

Kwa upande wake Afisa Oparesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga Inspekta Edward Lukuba, alisema walichelewa kufika eneo la tukio sababu gari lao la kuzimia Moto ni bovu, na wanagari moja tu, ambapo ili bidi waazime kutoka Jeshi la Wananchi Kambi ya Kizumbi, ndipo wakafika na kuuzima Moto huo.

Aidha, alisema chanzo cha Moto huo ni hitilafu ya mfumo wa umeme ndani ya nyumba hiyo, sababu ya waya zake kutokuwa katika mfumo mzuri, na kubainisha kuwa hakuna madhara kwa binadamu zaidi ya mali nyingi kuteketea.


Muonekano wa nyumba ikiwaka Moto.

Muonekano wa nyumba ikiwaka Moto.
Muonekano wa nyumba ikiwaka Moto.

Muonekano wa nyumba ikiwaka Moto.




















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464