PROFESA ASSAD ASISITIZA HAKUONDOLEWA KIHALALI, AKERWA KUITWA MSTAAFU



Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wa zamani, Profesa Mussa Assad amesema hapendi kuitwa Mstaafu na neno hilo linamchukiza, akidai kuwa taratibu za kumwondoa hazikufuatwa.

Profesa Assad ameyasema hayo leo Oktoba 6 jijini Dodoma wakati wa mdahalo juu ya kitabu cha Rai ya Jenerali kinachozungumzia umuhimu wa Katiba Mpya.

Hata hivyo taarifa iliyotolewa na Serikali mwaka 2019 ilieleza kuwa Profesa Assad kipindi chake kilimalizika Novemba 4, 2019

"Sipendi sana kusikia neno mstaafu na kwamba neno hilo linaniudhi linapotamkwa mbele yangu," amesema Profesa Assad.
 
SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464