RC MJEMA AFUNGUKA AKITOA HOTUBA, AONYA MATUMIZI MABAYA FEDHA UJENZI MADARASA, KUTOKOMEZA MIMBA ,NDOA ZA UTOTONI.


Mkuu wa Mkoa mpya wa Shinyanga Mhe; Sophia Mjema, (kushoto), akiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Dk, Philemon Sengati, wakikabidhiana nyaraka za Ofisi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa Mpya wa Shinyanga Mhe; Sophia Mjema, ambaye ameteuliwa Oktoba 8 mwaka huu, na Rais Samia Suluhu Hassani na kuapishwa jana, amekabidhiwa Ofisi Rasmi, na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Dk. Philemon Sengati, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Zoezi hilo la Makabidhiziano ya Ofisi, limefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini, Taasisi, na mashirika ya kiraia.

Amesema katika utendaji wake kazi mkoani Shinyanga, anataka kuwepo na mambo matatu kwa watumishi wa umma, ambayo ni Mshikamano, Uwajibikaji, na usimamizi.

Akielezea suala la Mshikamano, amewataka watumishi wote wa umma wafanye kazi kwa pamoja kama Team Work, na siyo kununiana, bali waheshimiane na kushirikiana katika utendaji kazi.

Akizungumzia Suala uwajibikaji, amewataka watumishi wa umma kuanzia ngazi zote, kila mmoja awajibike katika eneo lake la utendaji kazi, ikiwamo kutatua migogoro ya wananchi, na siyo tatizo lipo ngazi ya Kata linashindwa kutatuliwa hasi aende Mkuu wa Wilaya au Mkoa, na kubainisha kuwa kwenye uongozi wake hilo jambo halina nafasi.

Pia, amezungumzia suala la usimamizi wa fedha za Serikali pamoja na miradi ya maendeleo, amewataka watumishi wafanye kazi zao kwa weledi na kuwajibika ipasavyo kwa kusimamia vizuri shughuli zote za Serikali na kutoa huduma kwa wananchi ipasavyo.

“Baada ya kumaliza kuapishwa jana na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani, tulipewa maaagizo ya kujenga mshikamano, kusimamia uwajibikaji na usimamizi wa fedha za umma,”alisema Mh Mjema.

“Kutokana na kuagizwa kusimamia fedha za umma, hivyo nawaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani hapa, fedha ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassani, kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa, nataka zitekeleze ujenzi huo na siyo kutumiwa katika shughuli zingine sababu fedha hizi nizamoto,”aliongeza.

Aidha, aliwataka wakuu wote wa Idara mkoani humo wawe na Kitabu Cha ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, ambacho kinaonyesha vitu wanavyotakiwa kufanya katika idara mbalimbali ikiwamo Afya, Elimu, na Kilimo, na siyo kukaa Ofisini na kusubili wasukumwe na viongozi.

Pia, amewataka wawe na Takwimu kichwani kwa kufahamu masuala yote ya idara zao, ambapo wakipigiwa kuombwa Taarifa wawe wanazitoa kichwani, na kuachana na mambo ya ku-copy na ku-paste taarifa, huku akibainisha kuwa siku wakija viongozi wakubwa wa kitaifa, maswali yote watakuwa wanajibu wao na siyo kuwaachia jukumu hilo viongozi.

“Wakuu wa Idara nawataka mfanye kazi na siyo kukaa maofisi, pamoja na Maofisa ugani, muache kuvaa mawigi, bali ni vipara tu na kuvaa Gambutu kuingia kwa wakulima kutoa elimu ya kilimo cha kisasa na kama mashamba Darasa yamekufa yafufuliwe, nataka wananchi walime kilimo chenye Tija,”alisema Mjema.

Katika hatua nyingine ameeleza kuchukizwa na Tatizo la Mimba na Ndoa za utotoni, ambalo limekuwa kero mkoani humo, na kuonyesha adhima yake ya kutaka kulimaliza tatizo hilo, likiwamo na la Imani Potofu za Kishirikina, huku akiwaomba viongozi wa Dini washirikiane na Serikali kumaliza matatizo hayo.

“Mkoa huu wa Shinyanga una mimba nyingi sana za utotoni nataka kuzimaliza kabisa, na wale wazazi wenye tabia ya kumalizana na watuhumiwa kwa kupewa kitu kidogo na kushindwa kutoa ushahidi tutawakamata na kuwa sweka ndani, lengo langu mimba za utotoni zisiwepo Shinyanga,”alisema Mh Mjema.

Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, alisema Mkoa huo umepata kiongozi Jembe na mtendaji kazi mzuri sababu anafahamu Rekodi zake, na kuwaomba watumishi wa mpatie ushirikiano, ili kuwaletea maendeleo wananchi.

“Namshukuru Rais Samia Suluhu Hassani, kwa kunipatia fursa ya kuwatumikia Watanzania kupitia mkoa huu wa Shinyanga, na sasa nina mwachia mwenzangu na nina amani kabisa na mmepata Mkuu wa Mkoa Jembe sababu Mh Sophia Mjema Rekodi zake zinaonyesha ni mtedaji mzuri,”alisema Sengati.

Nao Wakuu wa Wilaya mkoani Shinyanga, akiwamo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, kwa nyakati Tofauti wakitoa salama, walimkaribisha Mkuu huyo Mkoa Mpya Sophia Mjema, na kuahidi kumpatia ushirikiano katika kuwatumikia wananchi wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa mpya wa Shinyanga Mhe; Sophia Mjema, (kushoto), akiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Dk. Philemon Sengati wakisaini Hati ya makabidhiano ya Ofisi.

Mkuu wa Mkoa mpya wa Shinyanga Mhe; Sophia Mjema, (kushoto), akiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Dk, Philemon Sengati, wakikabidhiana nyaraka za Ofisi.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, akizungumza mara baada ya kumaliza kukabidhi Ofisi Rasmi, kwa Mkuu wa Mkoa mpya wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema.

Mkuu wa Mkoa mpya wa Shinyanga Mhe; Sophia Mjema akizungumza mara baada ya kumaliza kukabidhiwa Ofisi Rasmi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Dk. Philemoni Sengati.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa, akitoa salam kwenye makabidhiano hayo ya Ofisi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye makabidhiano hayo ya Ofisi ya Mkuu mpya wa Mkoa wa Shinyanga Mhe; Sophia Mjema na aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo Dk. Philemon Sengati.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akizungumza kwenye makabidhiano hayo ya Ofisi ya Mkuu mpya wa Mkoa wa Shinyanga Mhe; Sophia Mjema na aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo Dk. Philemon Sengati.

Viongozi wa dini wakishuhudia makabidhiano ya Ofisi kati ya Mkuu wa Mkoa mpya wa Shinyanga Mhe; Sophia Mjema na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Dk. Philemon Sengati.

Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Shinyanga, wakishuhudia makabidhiano ya Ofisi kati ya Mkuu wa Mkoa mpya wa Shinyanga Mhe; Sophia Mjema na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Dk. Philemon Sengati.

wajumbe wakiendelea kushuhudia zoezi la makabidhiano ya Ofisi.

wajumbe wakiendelea kushuhudia zoezi la makabidhiano ya Ofisi.

wajumbe wakiendelea kushuhudia zoezi la makabidhiano ya Ofisi.

wajumbe wakiendelea kushuhudia zoezi la makabidhiano ya Ofisi.

Picha ya Pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa zoezi hilo la Makabidhiano ya Ofisi.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.







































































































































































































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464