UWT SHINYANGA MJINI WASIKITISHWA UCHAKAVU MIUNDOMBINU SHULE YA MSINGI BUGWETO, WATOA MATOFALI 200

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Mwajuma Rabi, (kulia), akimkabidhi Matofali 200 Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugweto Kulwa Robert, (katikati) kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa katika shule ya Msingi Bugweto, wapili kushoto ni Diwani wa Viti maalum Manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama cha Mapinduzi CCM (UWT) wilaya ya Shinyanga Mjini, wamesikitishwa na uchakavu miundombinu shule ya Msingi Bugweto Manispaa ya Shinyanga na kusababisha wanafunzi kusoma katika mazingira mabovu.

Wanawake hao wamebainisha hayo leo, wakati walipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuadhimisha siku ya wanawake UWT duniani, ambayo huadhimishwa kuanzia Septemba 28, na kuhitimishwa Oktoba 4, na kujionea uchakavu wa miundombinu ya shule hiyo.

Akizungumza Shuleni hapo,Mgeni Rasmi Mwajuma Rabia, ambaye ni Mjumbe kamati ya utekelezaji UWT wilaya ya Shinyanga Mjini, amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele kuchangia Shughuli za maendeleo, ili watoto wa shule hiyo wasome katika mazingira mazuri.

Alisema, Diwani wa Viti maalumu Manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri, alifika kwenye kamati yao ya utekelezaji UWT, na kueleza changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya Shule hiyo ya Msingi Bugweto  na kuamua kumuunga mkono ili kuikarabati na kujenga Madarasa mapya.

"Sisi kama UWT wilaya ya Shinyanga Mjini, tunampongeza Diwani wa Vitimaalum Zuhura Waziri, kwa kuguswa na uchakavu wa miundo mbinu ya shule hii ya msingi Bugweto, na kutoa mifuko ya Saruji 25, ambapo na sisi tumemuunga mkono na kutoa tofali 200", alisema Rabia.

"Wanawake wenzangu, watoto wanaosoma hapa shuleni ni wa kwetu, na kilio kina wenyewe, Diwani wetu wa Vitimaalum amelia, na sisi tumuunge mkono kuikarabati shule hii, na kujenga madarasa, ili watoto wasome katika mazingira mazuri na kutimiza ndoto zao," aliongeza.

Naye Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Lucy Enock, alisema wakati wa siasa umeshapita, na sasa ni kuchapa kazi kuchangia shughuli za maendeleo, na kuwataka akina mama wa bugweto waikarabati shule hiyo wenyewe na kuonyesha mfano.

"Siku nafika hapa shuleni kukabidhi mifuko ya Saruji iliyotolewa na Diwani wa Viti maalum Zuhuru Waziri, niliguswa sana na watoto wetu hapa shuleni, kuona wanasoma katika madarasa yana nyufa, hakuna sakafu chini, ndipo nikaona sisi kama UWT lazima tufanye kitu hapa shuleni na leo tumefanya kitu,"alisema Enock.

Kwa upande wake Diwani wa Viti maalum Zuhura Waziri, alisema shule hiyo ya Bugweto ipo katika hali mbaya, ndipo akaona afanye jambo, na kutoa Mifuko ya Saruji 25, pamoja na kushirikisha Jumuiya ya UWT wilaya ya Shinyanga Mjini, ili kusaidia kukarabati shule hiyo kwa kushirikiana pia na wanawake wa Bugweto.

Aidha katika harambee ambayo imeendeshwa shuleni hapo, kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na kukarabati miundombinu ya shule hiyo, zimechangwa Sh. 244,500, Mifuko ya Saruji 32 na Matofali 81, huku zoezi la uchangiaji likiwa endelevu, hadi kuhakikisha shule hiyo ina kuwa katika mazingira mazuri.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Mwajuma Rabi, akizungumza kwenye katika shule ya Msingi Bugweto.

Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Lucy Enock, akizungumza katika Shule ya Msingi Bugweto

Diwani wa Vitimaalum Zuhura Waziri akizungumza shuleni hapo na kueleza namna alivyoguswa na uchakavu wa miundombinu ya shule hiyo na kuamua kufanya jambo ili kuiboresha.

Diwani wa Vitimaalum Zuhura Waziri akizungumza shuleni hapo na kueleza namna alivyoguswa na uchakavu wa miundombinu ya shule hiyo na kuamua kufanya jambo ili kuiboresha.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugweto 'B' Kulwa Robert, akimpongeza Zuhura Waziri na Jumuiya hiyo ya Wanawake UWT wilaya ya Shinyanga mjini kwa kujitoa kusaidia kuikarabati shule hiyo.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Mwajuma Rabi, (kulia), akimkabidhi Matofali 200 Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugweto Kulwa Robert, (katikati) kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Bugweto, wa pili kushoto ni Diwani wa Viti maalum Manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri.

Muonekano wa Matofali yaliyokabidhiwa na UWT wilaya ya Shinyanga Mjini katika shule ya Msingi Bugweto.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Mwajuma Rabi,, akimkabidhi Miti 275 Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugweto 'B' Kulwa Robert, kwa ajili ya kutunza Mazingira ya shule hiyo.

Ukaguzi wa miundombinu ya Madarasa shuleni hapo ukifanyika na kuonyesha ubovu wa Madarasa.

Diwani wa Viti maalum Manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri, kulia, akionyesha Tundu kwenye Ubao katika Shule ya Msingi Bugweto, kushoto ni Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Lucy Enock.

Diwani wa Vitimaalum Manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri, (kushoto), akionyesha tundu kwenye ukuta wa darasa katika Shule ya Msingi Bugweto, (kulia) ni Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Lucy Enock.

Muonekano wa nyufa katika moja ya madarasa katika Shule ya Msingi Bugweto.

Ukuta wa choo shuleni hapo ukiwa umedondoka.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugweto 'B' Kulwa Robert akionyesha nyufa katika choo cha Shule hiyo.

Akina mama wa Bugweto wakiwa kwenye mkutano wa UWT kuchangia ujenzi wa madarasa na ukarabati wa Shule hiyo.

Akina mama wa Bugweto wakiwa kwenye mkutano wa UWT kuchangia ujenzi wa Madarasa na ukarabati wa Shule hiyo.

Akina mama wa Bugweto wakiwa kwenye mkutano wa UWT kuchangia ujenzi wa madarasa na ukarabati wa shule hiyo.

Akina mama wa Bugweto wakiwa kwenye mkutano wa UWT kuchangia ujenzi wa Madarasa na ukarabati wa Shule hiyo.

Uchangiaji wa ukarabati na ujenzi wa Madarasa katika Shule ya Msingi Bugweto ukiendelea.

Uchangiaji ukiendelea.

Awali Mgeni Rasmi Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Mwajuma Rabi, kulia, akiwa na Diwani wa Vitimaalum Zuhura Waziri (katikati) na Katibu wa UWT Lucy Enock, kushoto, wakiwa katika ukaguzi wa miundombinu ya Shule ya Msingi Bugweto.

wanawake wa UWT wakiwa katika Shule ya Msingi Bugweto.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464