Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosis ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Usharika wa Makedonia Holyness Mkaro, akisoma Risala kwa niaba ya wenzake kwenye sikukuu ya Mikael na watoto Kanisani hapo.
Na Marco Maduhu, Shinyanga
Watoto wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Usharika wa Makedonia Lubaga Manispaa ya Shinyanga, wamesherehekea Sikukuu ya Mikael na watoto Kanisani hapo na kukemea matukio ya ukatili dhidi ya watoto.
Sherehe hizo zimefanyika Kanisani hapo leo zikiambatana na mafungu ya kukariri, maigizo, na nyimbo mbalimbali zenye ujumbe wa kulinda haki za watoto na kuwatimizia mahitaji yao, ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Mhasibu wa Shirika la AGPAHI Ester Ulomi.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Kanisani hapo Holyness Mkaro, akisoma Risala kwa niaba ya wenzake, alikemea kuendelea kuwepo kwa matukio ya ukatili dhidi ya watoto mkoani Shinyanga, ikiwemo ubakaji, vipigo, ulawiti, utelekezaji watoto, mimba na ndoa za utotoni.
Alisema kuendelea kwa matukio hayo ya ukatili mkoani Shinyanga imekuwa ni kero kwao kwani yamekuwa yakiwaathiri kisaikolojia na hata kushindwa kutimiza ndoto zao.
"Matukio ya ukatili kuendelea kuwapo hapa mkoani kwetu, yanatuathiri sana sisi watoto, hivyo tunaomba Serikali kwa kushirikiana na Mashirika, wayamalize kabisa ili tuishi kwa amani na kutimiza malengo yetu," alisema Mkaro.
Aidha aliwaomba pia wazazi, waache tabia ya kumaliza kesi kimya kimya dhidi ya watuhumiwa wa matukio ya ukatili, na hata kushindwa kwenda kutoa ushahidi mahakamani na watuhumiwa kuachiwa huru, jambo ambalo linachochea matukio hayo kuendelea kuwepo.
Katika hatua nyingine ,aliwataka wazazi na walezi mkoani Shinyanga kuwalea watoto wao katika maadili mema na misingi ya kiroho, kuwatimizia mahitaji yao yote na kuacha kuwatelekeza.
Naye Mgeni rasmi Ester Ulomi ambaye ni Mhasibu wa Shirika la AGPAHI aliwataka wazazi kuwasimamia watoto kutimiza ndoto zao, pamoja na kuwalinda dhidi ya matukio ya ukatili.

Mchungaji wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Harold Mkaro, akizungumza kwenye sikukuu ya Mikael na watoto.
Mtoto Christopher Matemu, akiongoza maombi kwenye sikukuu ya Mikael na watoto kanisani hapo.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Usharika wa Makedonia Holyness Mkaro, akisoma Risala kwa niaba ya wenzake kwenye sikukuu ya Mikael na watoto kanisani hapo.
Mgeni rasmi Ester Ulomi, akitoa neno kwenye sikukuu ya Mikael na watoto kanisani hapo.
Watoto wakionyesha uwezo wa kukariri Mafungu ya kwenye Biblia.

watoto wakionyesha maigizo yenye ujumbe wa kuonyesha watoto wa kike na kiume wote wanahaki sawa.
Watoto wakiimba Nyimbo Kanisani hapo.
Watoto wakimlisha keki mgeni rasmi Ester Ulomi ambaye ni Mhasibu wa Shirika la Agpahi.
Mtoto Gian Kweka ,akimvalisha Skafu mgeni rasmi Ester Ulomi, mara baada ya kuwasili Kanisani hapo kwenye Sikukuu ya Mikael na Watoto.
John Eddy, akitoa matangazo ya Kanisa.
Watoto wa Kanisa la (KKKT) Makedonia, wakiwa na Familia ya mgeni rasmi kwenye sikukuu ya Mikael na watoto kanisani hapo.
Waumini wa Kanisa la (KKKT) Makedonia wakiwa kwenye sikukuu ya Mikael na watoto kanisani hapo.

Wanakwaya wa Kanisa la (KKKT) Makedonia wakiwa kwenye sikukuu ya Mikael na watoto Kanisani hapo.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.