Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga limeshauriwa
kufikiria madhara ya kudumu yanayompata mhanga wa ukatili wa kijinsia ambapo limelaumiwa kwa kuwa sehemu ya kukwamisha mapambano ya ukatili kwa
kutokukutoa ushirikiano dhidi ya matukio ya ukatili kwa watoto hayataisha.
Katibu wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wanawake na Watoto ya Mkoa wa Shinyanga Bw. Thedson Ngwale amesema hayo kwenye kikao cha asasi za kiraia zilizokuwa zimefadhiliwa na shirika la Firelight Foundation la nchini Marekani ambacho kimefanyika kuanzia 03 November hadi 05 November 2021.
Amesema baadhi ya matukio
yanashindwa kufanyiwa kazi kwa wakati na wananchi kuripoti matukio mengi lakini
yanayofanyiwa kazi ni machache hiyo ni kwa sababu sheria ya ushahidi inaruhusu
kesi kama hizo za jinai lakini zina dhamana,hivyo mtu akipata dhamana anaenda
kwenye mahakama ya familia kati ya familia ya mhanga na mtuhumiwa kwa mantiki
hiyo wanaenda kumtengeneza mhanga afiche ukweli kwa kuahidiwa au kupewa kitu na
familia ya mtuhumiwa.
Ngwale ambaye pia ni Afisa maendeleo ya jamii Mkoa
wa Shinyanga pia amewaomba viongozi wengine wa ngazi ya Taifa kwamba kuna sheria
zinahitaji mabadiliko na kesi zisiondolewe mahakamani kama ushahidi haueleweki
ili mkemia mkuu wa Serikali athibitishe kupitia vipimo vya Vina saba(DNA) baada
ya mtoto kuzaliwa ili kugundua mthumiwa ni yupi ili huo mchezo wa kupikwa kwa
ushaidi ukome.
Mmoja wa washiriki wa kikao hicho Mkurugenzi wa shirika la Agape Aids Control Program Bw.John Myola amemwomba Kamanda wa jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga atengeneze utaratibu kuawapata askari wa dawati la
Jinsia weye maadili na wasikae zaidi ya miezi sita bali
angalau miezi mitatu halafu wawekwe wengine kwa sababu kesi za ukatili
zinazowafikia wanazigeuza kuwa fursa kwa kuwa kuna mazingira ya rushwa na
kuharibu kesi za mimba na ndoa za utotoni.
Akitolea mfano wa kesi ambayo walienda mkamata baba mtu mzima aliyekutwa na binti wa miaka 14 wa darasa la tano mwenye mimba ya miezi mitano na humo ndani alikuwa na mdogo wake mwenye umri wa miaka tisa ambapo mtoto huyo ni mtoto wake wa Kambo maana yake Mama mzazi wa huyo mtoto ameolewa na huyo baba na wakati wameenda kumkamata mama yake alikuwa amesafiri kwa muda wa miezi miwili maana yake huyo baba alikuwa anamtumia mama na mtoto kama wake zake.
Ameendelea kueleza kuwa mtuhumiwa huyo alikaa polisi
wiki mbili bila kwenda mahakamani ingawa alikamatwa na vielelezo vyote,matokeo
yake amepewa dhamana na baadae wanaambiwa mtuhumiwa ametoroka,hivyo ameshauri
polisi waliopo dawati la jinsia wawe wanabadilishwa wasikae pale kimazoea kwani
kwa kuna mazingira ya rushwa kutokana na kesi zinavyoyeyuka.
Amesema wao kama mashirika yanayopinga mimba na ndoa
za utotoni wanavunjika moyo kutokana na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya
maafisa wa Jeshi la Polisi waliopo dawati la jinsia kutengeneza mazingira ya
kupoteza ushahidi.
Kwa upande wake Afisa Miradi wa ulinzi na haki za
watoto kutoka Firelight Foundation bi. Tomaida Banda amesema wao kama shirika
walifanya utafiti wa mimba na ndoa za utotoni nchini Tanzania wakagundua kwamba
Shinyanga ni mmoja wa mkoa unaokabiliwa na changamoto hiyo na yapo mashirika
mengi yanahusika na kupinga vitendo hivyo ndipo wakaamua kuwa wafadhili kwa
mashirika hayo takribani 12 ili kuwawezesha kupambana na janga hilo na amesema
kwa kuwa mradi umeisha na wameukabidhi kwa Serikali,baada ya kikao cha tathmini
watafanya utafiti mwingine ndipo waje kuwekeza tena.
Akijibu malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya asasi hizo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema kama wana uthibitisho wa hizo tuhuma waende ofisini wazungumze na wampe taarifa zenye uthibitisho au viashiria vyovyote vyenye mianya ya rushwa ili achukue hatua kwa watakaobainika.
"Askari wetu ni weledi na wamepitia mafunzo, kama kuna tabia kama hizo na zimethibitika tutawachukulia hatua maana huenda siyo wote wapo safi katika kazi",amesema
Aidha mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ya mkaoni
Shinyanga yaliyokuwa yamefadhiliwa na shirika la Firelight Foundation kwa ajili
ya kupinga mimba na ndoa za utotoni ni pamoja na OPE,AGAPE,WEADO,ICS,TVMC,MKOMBOZI,TAI,CHIDEPA,RAFIKI
SDO,YWL NA PWWCO.
Washiriki kutoka baadhi ya asasi za Kiraia zinazoshughulika na mradi wa kupinga mimba na ndoa za utotoni wakiwa wanafuatilia uwasilishwaji wa mradi ulivyotekelezwa kwa kila shirika.
Washiriki kutoka baadhi ya asasi za Kiraia zinazoshughulika na mradi wa kupinga mimba na ndoa za utotoni wakiwa wanafuatilia uwasilishwaji wa mradi ulivyotekelezwa kwa kila shirika.