MADIWANI KASULU WASHUHUDIA UVAMIZI ENEO LA HIFADHI YA MAKERE FOREST KATIKA IKOLOJIA MOYOWASI-MALAGARASI



Meneja wa kitalu cha uwindaji cha Makere na eneo la wazi uvinza , Shadrack Kagoma akionesha watu walivyovamia eneo la hifadhi na kulima Mpunga.

Mwandishi wetu, Kasulu.
 
 Madiwani wa halmashauri ya Kasulu Mkoa wa Kigoma pamoja na viongozi wa halmashauri hiyo wametembelea eneo la hifadhi ya Makere na eneo la wazi la ardhi oevu ambalo limevamiwa na Idadi kubwa ya wafugaji na wakulima.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Elia Charles Kagoma akiwa pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Joseph Rwiza wakizungumza baada ya kutembelea eneo Hilo Jana wameeleza kusikitishwa na uvamizi unaoendelea.

Kagoma alitaka hatua za haraka kuchukuliwa na Mamlaka husika kuweka mipaka eneo hilo kutenga eneo la hifadhi na eneo la vijiji ili iwe rahisi kuwaondoa wavamizi wote.

"Lazima kuwepo alama maalum kuzunguka eneo hili ambalo ni kitaku Cha uwindaji ili kuhakikisha uvamizi unakomeshwa"alisema

Kwa upande wake Rwiza alitaka kuwepo na ushirikiano wa kupambana na wanaojihusisha na vitendo vya ujangili katika eneo Hilo ambalo ni muhimu Kwa maslahi ya Taifa.

Akizungumza na viongozi hao wa halmashauri,Meneja wa kitalu Cha uwindaji ncha Makere na eneo la wazi uvinza,Shadrack Kagoma amesema eneo hilo Sasa Kuna ujangili kutokana na uvamizi wa watu.

"Tuna wageni wa kimataifa wa uwindaji katika eneo hili lakini shida wakifika wanakuta kitalu chetu Kuna uvamizi wa Mifugo,kilimo na majangili"amesema

Amesema wavamizi wakiwepo kutoka nchi jirani wanaingia Mifugo eneo la hifadhi na kulima na baadhi wanaojihusisha na ujangili.

Madiwani wa Kasulu mkoani Kigoma wakiwa kwenye ziara eneo la hifadhi Makere
 
Baadhi ya watuhumiwa wa ujangili waliokamatwa katika eneo hili









Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464