EWURA CCC YAENDESHA SEMINA KWA MADIWANI,WENYEVITI SERIKALI ZA MITAA NA WATENDAJI KATA ZA MANISPAA YA SHINYANGA

Diwani wa kata ya Kambarage Mhe. Hassan Mwendapole akiongoza semina ya Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata 17 za Manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Mwenyekiti wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Kudely Sokoine, kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga limeendesha Semina kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata 17 za Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu haki na wajibu wa watumiaji wa  maji na nishati.

Semina hiyo iliyoandaliwa na EWURA Consumer Consultative Council (EWURA CCC) ambayo kazi yake ni kutetea watumiaji wa maji na nishati ili kuelewa haki zao imefanyika Jumatatu Novemba 22,2021 katika ukumbi wa Liga Hotel Mjini Shinyanga kikihudhuriwa pia na Afisa Uelimishaji na Uhamasishaji EWURA CCC,Stella Lupimo.

Akizungumza katika semina hiyo, Mwenyekiti wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga Kudely Sokoine amesema wameamua kukutana na viongozi hao ili kuwajengea uwezo kuhusu haki na wajibu wa watumiaji wa  maji na nishati.

Amesema huduma zinazodhibitiwa na EWURA ni Maji,bidhaa zitokanazo na petrol (petroli,mafuta ya taa na mafuta mazito), umeme na gesi asilia.

Sokoine amezitaja baadhi ya haki za mtumiaji wa maji na nishati kuwa ni kupata huduma ya msingi,usalama na faragha,kupata taarifa,kuchagua huduma kwa kuzingatia bei na ubora,kulalamika,kufidiwa,kuelimishwa, kusikilizwa na kuwakilishwa.

Amefafanua kuwa Wajibu wa mtumiaji wa nishati za maji ni pamoja na Kulipa Ankara kwa wakati,matumizi halali ya huduma,kutunza miundo mbinu,kutoa taarifa ama ufafanuzi,wajibu wa utambuzi,kutumia huduma kwa usalama na kulalamikia huduma mbovu.

Kwa upande wake Katibu Zezema Nyangaki  Shilungushela amesema EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga wamefungua Ofisi Mjini Shinyanga katika jengo la NSSF Ghorofa ya pili na ofisi hiyo itaanza kufanya kazi rasmi kuanzia Desemba 1,2021 hivyo kuwakaribisha wananchi akisema  ni haki yao kupeleka malalamiko yao kuhusu huduma za maji na nishati ili wazishughulikie na kwamba hakuna gharama yoyote ya kuandika malalamiko.

Ameyataja baadhi ya majukumu ya EWURA CCC kuwa ni pamoja na kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za maji na maji zinazodhibitiwa na EWURA na kupokea na kusambaza taarifa kuhusu maslahi ya watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA.

Amesema miongoni mwa mifano ya malalamiko ya watumiaji wa huduma za maji na nishati ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wateja ni ongezeko la bili za umeme na maji, kuunguliwa vyombo vya umeme na makazi,migogoro ya usomaji mita, Makampuni kushindwa kutengeneza miundombinu inayopitisha huduma na uharibifu unaotokea majumbani kutokana na maji machafu na hitilafu za umeme. 

Malalamiko mengine ni pamoja na ucheleweshaji wa kuunganishwa kwenye huduma husika kwa watumia huduma wapya wanaotaka kuunganishwa na huduma za umeme na maji, Watoa huduma kushindwa kutoa mwitikio wa kuridhisha kwa maswali au malalamiko kutoka kwa watumiaji/wateja na maswali kuhusu namna bili zisizo na mita zinavyoandaliwa na ukadiriaji viwango vyake.

Kwa upande wao washiriki wa semina hiyo,wameishukuru EWURA CCC kuandaa semina hiyo na kuomba elimu zaidi iendelee kutolewa kwa wananchi ili kujua haki na wajibu wao katika huduma za maji na nishati huku wakiipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa namna inayojitahidi katika utoaji huduma na kujali wateja.

Madiwani, wenyeviti wa serikali na na maafisa watendaji hao pia wameeleza kukerwa na utoaji huduma wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga kwa kutoshughulikia malalamiko ya wateja ikiwemo kutounganishiwa huduma ya umeme kwa wakati pamoja na kitengo cha dharura kutoshughulikia malalamiko ya wateja mbaya zaidi hawapokei simu za dharura ‘Emergency’ , kuchelewa kufika eneo la tukio wanapopigiwa simu za dharura na kukata kata umeme bila taarifa na umeme kuunguza vifaa.

Afisa Uelimishaji na Uhamasishaji EWURA CCC, Stella Lupimo amelielekeza Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga wafuatilie na wapate majibu ya malalamiko ya watumiaji wa huduma za maji na nishati ya umeme ili kuhakikisha yanatatuliwa.

Viongozi wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga wakijitambulisha kwenye Semina kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata 17 za Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu haki na wajibu wa watumiaji wa  maji na nishati. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Uelimishaji na Uhamasishaji EWURA CCC,Stella Lupimo (kulia) akijitambulisha kwenye Semina ya Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata 17 za Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu haki na wajibu wa watumiaji wa  maji na nishati.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Esther Makune akizungumza kwenye semina ya Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata 17 za Manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga.
Diwani wa kata ya Kambarage Mhe. Hassan Mwendapole akizungumza kwenye semina ya Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata 17 za Manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Kudely Sokoine akizungumza kwenye semina ya Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata 17 za Manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga.

Katibu wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Zezema Nyangaki Shilungushela akizunguza kwenye semina ya Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata 17 za Manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga.

Afisa Uelimishaji na Uhamasishaji EWURA CCC,Stella Lupimo akizungumza kwenye semina ya Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata 17 za Manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga.
Mweka Hazina wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Joseph Ndatala akitoa mada kwenye semina ya Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata 17 za Manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga.
Mjumbe wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Jonathan Manyama akitoa mada kwenye semina ya Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata 17 za Manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa SHUWASA, Masaka Kambesha akizungumza kwenye semina ya Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata 17 za Manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Msaidizi Huduma kwa Wateja na Utawala EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Leone Bizimana akizungumza kwenye semina ya Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata 17 za Manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga.
Wenyeviti wa serikali za mitaa, Madiwani na maafisa watendaji wa kata za Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga.

Semina inaendelea

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464