MAHAFALI YA KWANZA CHUO CHA VETA MATANDA YAFANYIKA...SISTA LUCINDER ATAKA WATUMIE TAALUMA WALIYOIPATA KUBADILI MAISHA YAO


Wahitimu Saba wa Fani mbalimbali katika chuo cha ufundi Stadi Matanda VTC Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho tangu kifunguliwe mwaka 2018.

Na Mwandishi wetu.

Wahitimu katika chuo cha ufundi cha kikatoliki Veta Matanda kilichopo kata ya Chamaguha halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wameaswa kwenda kuitumia vyema taaluma waliyopata katika chuo hico kubadili maisha yao na jamii kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa Novemba 20 ,2021 na Sista Lucinder Mologai wakati wa Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ufundi Veta Matanda Shinyanga wakati akizugumza na wanafuzni wahitimu katika chuo hicho

Amesema kuwa elimu waliyoipata katika mafunzo hayo ikawe msaada kwao kwa kukabiliana na changamoto za kimaisha ikiwemo ajira nchini kwa kufanya kazi kwa kujituma, bidii na nidhamu ya hali ya juu itakayowafanya kufikia malengo yao.

“Fanyeni kazi zenu kwa bidii kama mtakatifu Joseph alivyofanya katika maisha yake na leo hii amebaki katika historia ya maisha yetu nanyi mkawe mfano wa kuigwa”,alisema Sista Lucinder

Sista Lucinder ameongeza kuwa jukumu lao kwa sasa ni kufanya mabadiliko kwa jamii kwa kuonesha uwezo wao katika kubuni miradi midogo ambayo baadae itakuwa mikubwa na kuajiri vijana wengine huku akisisitiza kuwa wavumilivu katika kazi zao.

“Changamoto za ajira ni mojawapo ya kikwazo kwa vijana niwatake tu mkakabiliane nazo badala ya kuzikimbia akitolea mfano wa changamoto hizo kuwa ni njaa, uchumi, magonjwa na fedha hivyo jambo kubwa ni uvumilivu", alisema Sista Lucinder.

Mratibu wa mafunzo chuo cha ufundi Matanda-VTC Sista Maria Elgebet Maasi amewataka wahitimu kuonesha upendo na moyo wa huruma kwa wengine kwa kufanya kazi zao kwa uaminifu pale watakapopata ajira au kujiajiri wenyewe

“Niwaombe mkawe watu wa mfano wa kuigwa kwenye jamii kwa kufanya mema ikiwemo kutangaza chuo chetu vizuri huko mtakakokwenda najua mmejifuza mengi na mazuri ikiwemo ufundi wa magari, umeme, ushonaji hivyo hakikisheni vinakuwa taa yenu”,amesema

Naye Mkuu wa Chuo hicho Joasinta Kisanko amewasihi wahitimu hao kuwa mfano bora kwa kuhakikisha wanafikia ndoto zao kwa kufanya kazi kwa bidii baada ya elimu waliyoapata chuoni hapo kwa muda wa miaka miwili

Kisanko amesema kuwa chuo hicho kilianzishwa mwaka 1989 na kanisa katoliki jimbo la Shinyanga na baadae mwaka 2010 kilifungwa kwa kukosa baadhi ya sifa ambapo uongozi wa jimbo umefanya taratibu zote na kuanza tena mwaka 2018

“Haya mahafali yetu ya kwanza tangu chuo kianze kutoa huduma zake upya mwaka 2018 baada ya kufungiwa na mamlaka zinazosiamamia taaluma",amesema

Kisanko ameongeza kuwa miaka miwili si haba kwa mtoto au mwanafunzi kuwa chuoni hivyo kukaa kwao hapo chuoni isiwe wamepoteza gharama za bure bali iwe ishara kuu ya mafanikio yao muhimu

Awali wakisoma risala kwa mgeni rasmi wanafunzi hao wamesema kuwa zipo baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwemo uboreshwaji wa Mabweni, vifaa vya kujifunzia na kufundishia.
Wahitimu wa chuo cha ufundi Veta Madanta wakiwa kwenye maandamano kuelekea mahafali yao ya kuhitimisha safari yao ya maomo kwa kipindi cha miaka miwili.Picha ya pamoja kati ya wahitimu Mkuu wa chuo hicho Joasita Kisanka wa kwanza Kushoto akifuatiwa na Sista Maria Maasi na Mgeni rasmi Sista Lucinder Mologai ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Buhangija Sista Lucinder Mologai akimvisha taji mhitimu wa kozi ya Umeme Matanda VTC.Mkuu wa chuo cha Veta Matanda Joasita Kisanka akitoa taarifa ya wanafunzi wahitimu wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho.Sista Lucinder Mologai akimpatia cheti mhitimu wa kozi ya Umeme Matanda VTCSista Lucinder Mologai Mgeni Rasi katka mahafali ya kwanza ya chuo cha Veta Matanda akizungumza na wahitimu Matanda VTC.Sista Maria Maasi Mratibu wa Mafunzo Matanda VTC.Mkuu wa chuo hicho Joasita Kisanka wa kwanza Kushoto akifuatiwa na Sista Maria Maasi na Mgeni rasmi Sista Lucinder Mologai
Wahitimu wa Veta Matanda wakisoma risala kwa mgeni rasmi

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464