MADIWANI KISHAPU WALIA UBOVU MIUNDOMBINU YA BARABARA

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Wiliam Jijimya akiendesha Baraza la Madiwani.

Na Suzy Luhende, KISHAPU

Madiwani wa Halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga wamesema miundombinu ya barabara iliyopo mingi ni mibovu, ambayo inasababisha sehemu zingine wanafunzi kushindwa kwenda shule na kina mama kujifungulia njiani hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya wanafunzi na kina mama wajawazito.

Hayo wameyasema jana kwenye kikao cha Baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo ambapo madiwa walidai miundombini ya ya barabara iliyopo hazipitiki wakati wa masika, hivyo wameimba serikali iwatengenezee barabara ili waweze kunusuru maisha ya watoto na kina mama wajawazito.

Baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo Thabitha Mmbando wa kata ya Mwakipoya amesema hali ya barabara katika kata yake ni mbaya na huu ni wakati wa mvua kama hazitatengenezwa hazitapitika tena hivyo ameiomba serikali umsaidie ili waweze kuzitengeneza barabara hizo Wananchi wake waweze kupita na kuweza kufanya kazi za maendeleo.

Diwani wa kata ya Somagedi Nyama Kisinza amesema hali ya barabara ni mbaya sana katika kata ya Somagedi kina mama wajawazito wanapata shida sana wakati wanaenda kujifungua kwani kutokana na barabara kuwa mbovu wamekuwa wakijifungulia njiani na kuhatarisha maisha yao na watoto wao kwa sababu njiani hakuna mtaalamu au Mganga wa kuwasaidia.

"Mimi ni diwani wa kata ya Mwakipoya ambaye ni mwanamke ambaye nimekuwa nikitoa taarifa hii kila wakati lakini naona haifanyiwi kazi, hivyo naomba mnisaidie kwa hilo, wananchi wangu wanapata shida sana hivyo naomba kabisa serikali unisaidie Wananchi wangu wanalima mazao ya Biashara lakini wanashindwa kusafirisha kwa sababu hakuna Njia za kupitisha na hatuingizi mapato kutokana na Njia kuwa mbovu"alisema Thabisa

Michael Hillya ambaye no diwani wa kata ya Shagihilu amesema katika kata yake pia barabara hazipitiki hivyo inapokuja bajeti ya maendeleo na kata take ikumbukwe iwekwe kwenye bajeti.

Madiwani wengine James Kasomi wa kata ya Bubiki, Francis Manyanda diwani wa kata ya Mwadui Lohumbo na Fednand Mpogomi wamesema kweli barabara ni za muhimu katika maeneo yao kwani ndiyo yanasababisha kuongeza uchumi na kuongeza mapato ya ndani hivyo no vizuri serikali ikaliangalia hili kwa macho mawili.

Diwani wa kata ya Songwa Abdul Ngolomole amesema kwenye kata yake na kata zingine barabara zimetengenezwa lakini zimeishi njiani, hivyo aliomba ile bajeti ya ndani iliyokuwa imepitishwa 100 milioni imalizie kuchonga barabara hizo.

Baadhi ya Madiwani Edward Manyama diwani wa kata ya Kiloleli amesema yeye alikuwa na changamoto ya muda mrefu barabara lilikuwa halipitiki lakini anaishukuru Tarura barabara yake inaendelea kutengenezwa ili iweze kupitika vizuri lakini alisisitiza barabara za kata zingine zitengenezwe kwa wakati katika wakati huu wa masika ziweze kupitika

Meneja wa Tarura wilaya ya Kishapu Richard Kachwele amesema katika eneo lake Tarura inaendelea kufanya kila jitihada ili kutatua changamoto ya barabara zote zilizoharibika, awali walikuwa na mtandao mdogo lakini kwa Sasa wameongeza mtandao mkubwa wameziingiza kwenye mfumo ambazo ni kilomita 1024 .6.

"Barabara hizo zote zipo kwenye ramani,Tarura tumejipanga vizuri japo tu wachache tunafanya kazi hatulali niwaombeni tu waheshimiwa muwe subira, tutaendelea kufanya kazi katika maeneo yote ya wilaya hii"amesema Kachwele.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo William Jijimya ambaye ni diwani wa kata ya Mondo amesema kwa ujumla barabara nyingi haziko vizuri zinahitaji kutengenezwa kwani Kuna sehemu nyingine wakati wa masika wanafunzi inabidi wavushwe hawana pa kupita kina mama wajawazito wanajifungua njiani, hivyo no vizuri barabara zikatengenezwa kwa wakati.

Madiwani wakiwa kwenye Baraza.


Madiwani wakiwa kwenye Baraza.








Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464