MAHAFALI YA 36 CHUO CHA VETA SHINYANGA YAFANA, MKURUGENZI SATURA ATANGAZA NEEMA KWA WAHITIMU

Kaimu Mkuu wa chuo cha Ufundi Stad (VETA) mkoani Shinyanga Magu Mabelele, (kushoto), akimkabidhi Zawadi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura kwenye Mahafali ya 36 chuoni hapo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

CHUO cha ufundi stadi (VETA) Mkoani Shinyanga, kimefanya mahafali ya 36 chuoni hapo, kwa kuwaaga wahimitimu wa mwaka wa pili kutoka fani mbalimbali.
Mahafali hayo yamefanyika chuoni hapo leo, na kuhudhuliwa na viongozi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali, na za kifedha, huku mgeni Rasmi akiwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura.

Akizungumza kwenye Mahafali hayo Kaimu Mkuu wa chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele, amesema chuo hicho kilianzishwa mwaka 1989, ambapo kilikuwa na Fani moja ya ujenzi, lakini mpaka sasa kina Fani 37, mafunzo ya muda mrefu yanafani 10 ya muda mfupi fani 27.

Amesema chuo hicho kina watumishi 42, walimu wa mafunzo 28, na 14 wapo katika shughuli zingine saidizi, huku kikiwa na wanafunzi 416 wa Fani ndefu, na 1,364 Fani Fupi, na kubainisha wanakabiliwa na uhaba wa Hosteli za wanafunzi, ambapo katika Hosteli za chuoni hapo wanauwezo wa kubeba wanafunzi 170 tu.

“Mgeni Rasmi chuo chetu kwa sasa ni kikubwa sana, ila tunakabiliwa na changamoto ya upungufu wa Hosteli, ambapo wanafunzi wengi wamepanga vyumba mitaani, na hivyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali hasa wa kike na kusababisha baadhi yao kushindwa kumaliza mafunzo,”alisema Mabelele.

“Mfano mzuri wanafunzi ambao wamehitimu leo, walianza mafunzo wakiwa 162, lakini wanahitimu 141, na hiyo inatokana na sababu za kuishi kwenye nyumba za kupanga mitaani (Magheto), ambapo wanakosa uangalizi na kujiamulia mambo yao wenyewe, hivyo natumia fursa hii kuita wawekezaji waje Shinyanga kuwekeza Hosteli za wanafunzi,”aliongeza.

Pia, alisema changamoto nyingine ambayo inawakabili chuoni hapo, ni ukosefu wa huduma ya Afya, mfumo wa majitaka ambapo huingia gharama ya kuvuta majitaka kila wiki na hutozwa kiasi cha Sh. 120,000, na kuomba wapunguziwe gharama hizo ili wasiingie hasara, pamoja na kumuomba Mkurugenzi huyo aanzishe usafiri wa umma katika barabara ya Kizumbi, ili wanafunzi wasipate shida ya usafiri.

Katika hatua nyingine alitoa wito kwa wazazi, kuwasaidia watoto wao ambao wanahitimu mafunzo mbalimbali ya ufundi chuoni hapo kwa kuwanunulia vifaa au kuwapatia fedha za mitaji ili wajiajiri wenyewe, kuliko kuwaacha wakilandalanda mitaani na kulalamika hakuna ajira na wakati wanaujuzi wa kutosha.

Aidha Mwanafunzi Elizabeth Philemon akisoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake, alisema changamoto kubwa ambayo inawakabili wahitimu wa mafunzo ya ufundi ni ukosefu wa ajira pale na fedha za mitaji ili wapate kujiajiri wenyewe na ndiyo maana wengi wao huishia mitaani na kukaa bila kazi.

Alisema anaoimba Serikali kupitia Halmashauri zirahisishe masharti ya utoaji mikopo kwa vijana asilimia 4 ili wahitimu hao kutoka VETA wawe wanajiunga kwenye vikundi na kupewa fedha hizo, ambazo zitawasaidia kujiajiri wenyewe na kuacha kutegemea kuajiriwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, aliwatoa wasiwasi wahitimu wa VETA hasa wale ambao wanaishi Manispaa ya Shinyanga ,kuwa hakuna ugumu wowote wa kupata mikopo tena wao wanafursa kubwa sababu wakipata fedha hizo watakwenda kuzitumia vizuri sababu wanaujuzi na hatimaye kujikwamua kimaisha.

Satura alitoa ahadi pia kwa wahitimu wa Fani ya ushonaji na ubunifu wa mavazi kuwa ataangalia namna ya kuwasaidia kwa kuwafungulia ofisi yao ili washone nguo na kujiajiri wenyewe, huku akitoa ahadi kwa wale wa fani za umeme na ujenzi, kuwa watapewa kazi kwenye miradi mbalimbali ya manispaa hiyo ikiwamo ya ujenzi wa vituo vya afya, zahanati,Sekondari ya wasichana, na jengo la ghorofa la utawala la Manispaa.

Akizungumzia suala la usafiri wa umma, alisema Manispaa hiyo hadi kufikia Decemba mwaka huu, wanatarajia kukopesha wafanyabishara Magari Manne aina ya Costa, ambayo moja ya mashariti ni kubeba wanafunzi, ambapo zitakuwa zikipita katika Barabara za Olshinyanga, Kolandoto, Mwawaza, na Kizumbi.

Mkurungenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akizungumza kwenye Mahafali ya 36 katika chuo cha VETA Shinyanga.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele, akitoa taarifa ya chuo hicho.

Mratibu wa mafunzo chuo cha VETA Rashid Ntahigiye akisoma taarifa ya mafunzo ya chuo cha VETA kwenye Mahafali hayo.

Mwanafunzi Elizabeth Philemon, akisoma Risala kwenye Mahafali hayo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akiangalia Fani ya ushonaji na ubunifu wa mavazi chuoni hapo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akiangalia Fani ya ushonaji na ubunifu wa mavazi chuoni hapo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akiangalia Fani ya ushonaji na ubunifu wa mavazi chuoni hapo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akiangalia Fani ya ushonaji na ubunifu wa mavazi chuoni hapo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akiangalia Fani ya ufundi umeme chuoni hapo wakati wa Mahafali ya 36 leo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akiangalia Fani ya ufundi Magari na Mitambo chuoni hapo wakati wa Mahafali ya 36 leo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akiangalia Fani ya uchongaji na ung'arishaji madini ya Vito chuoni hapo.

Wanafunzi wakiendelea na kazi ya ung'arishaji Madini ya Vito chuoni hapo.

Muonekano wa Madini ya Vito.

Wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya 36 ya wanafunzi chuo cha VETA Shinyanga.

Wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya 36 ya wanafunzi chuo cha VETA Shinyanga.

Wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya 36 ya wanafunzi chuo cha VETA Shinyanga.

Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali yao.

Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali yao.

Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali yao.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akitoa vyeti kwa Wahitimu.

Zoezi la utoaji Vyeti likiendelea.

Kaimu Mkuu wa chuo cha Ufundi Stad (VETA) mkoani Shinyanga Magu Mabelele, (kushoto), akimkabidhi Zawadi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura kwenye Mahafali ya 36 chuoni hapo.

Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Ufundi Stadi VETA mkoani Shinyanga Magu Mabelele, akionyesha zawadi ya Picha ambayo amechorwa sura yake na mwanafunzi wa chuo hicho Kassimu Maxmiliam.

Awali Mgeni Rasmi katika Mahafali hao ya VETA Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura (kushoto) akiwasili chuoni hapo, (katikati) ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Veta Magu Mabelele na kulia ni Mratibu wa Mafunzo chuoni hapo Rashid Ntahigiye.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.



















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464