Mwanasiasa Mkongwe na Waziri wa zamani wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka ameendelea kusititiza kuwa Chato haina vigezo vya kupandishwa hadhi kuwa Mkoa kama inavyopigiwa debe na baadhi ya viongozi.
Profesa Tibaijuka ambaye amekuwa na msimamo huo tangu muda mrefu aliongeza kuwa hata hayati Dkt John Magufuli hakuwai kuzungumzia Chato kuwa Mkoa na kwamba analishwa maneno na baadhi ya watu wenye ajenda zao binafsi.
"Kama Mkoa unaundwa kwa vigezo, Chato hakuna vigezo siyo kwa sababu mimi ni mtu wa Muleba, lakini kwa sababu pia napafahamu Chato, Kama una vigezo kwanini wanamega Muleba ,kwanini wanamega Biharamulo kumega kwenyewe ndiyo ishara tosha kwamba hakuna vigezo sasa kama vigezo vipo kwanini unamega ? Wewe unataka kuwa Mkoa lakini hauwezi kuwa Mkoa mpaka umege vya wenzako ".
"Mimi nyumbani kwangu Muleba ni kilomita 100 tu kutoka Chato kwa hiyo nazungumza kama Mwenyeji wa maeneo yale nayajua, Sisi katika uhai wake hatukuwahi kumsikia Rais Magufuli akizungumzia Mkoa wa Chato kama ni kupaendeleza Chato kweli alikuwa anapaendeleza lakini mambo ya Mkoa tumekuja kuyasikia kwenye Msiba

SOMA ZAIDI HAPA ;CHANZO NIPASHE