RC MJEMA AHAMASISHA WANANCHI KULIMA MAZAO YA MUDA MFUPI, KUKABILIANA NA BAA LA NJAA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza na wananchi wilayani Kishapu.

Na Marco Maduhu, KISHAPU

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amewataka wananchi mkoani Shinyanga, katika msimu wa kilimo 2021-2022, walime mazao ya muda mfupi ambayo yanastahimili ukame, ili wapate mavuno mengi na kukabiliana na baa la njaa hapo baadae.

Mjema amebainisha hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa wilaya Kishapu kwenye mkutano wa hadhara, mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa miundombinu ya vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Kishapu.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassani, ameleta Tani 100 za Begu za Mahindi na Alizeti za muda mfupi, na kuwataka wakulima mkoani humo walime mazao hayo, ambayo yatawapatia mavuno mengi kwa kupata chakula, pamoja na kuuza Alizeti na kujipatia kipato.

“Nawasihi wananchi wa Kishapu na Mkoa wote wa Shinyanga, katika Msimu wa kilimo mwaka huu jikiteni kulima mazao ya muda mfupi ambayo yanastahimili ukame, ili kukabiliana na tatizo la njaa hapo baadae, pamoja na kulima kisasa,” alisema Mjema.

“Mbegu hizi ambazo tumeletewa na Mhe; Rais Samia, Alizeti inachukua muda wa miezi Minne, na Mahindi Mitatu zinakuwa zimekomaa, na wananchi tayari kupata mavuno, hivyo sitarajii kuja kusikia kuna mahali katika Mkoa huu wa Shinyanga eti wanalia na njaa, na wakati mbegu zipo za kutosha,”aliongeza.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa, alimwagiza Afisa Kilimo wilayani Kishapu George Kessy, kuhakikisha wanatoa elimu ya kilimo cha kisasa kwa wananchi. pamoja na kulima mazao hayo ya muda mfupi kwa kuwatembelea katika maeneo yao.

Katika hatua nyingine alimtaka Afisa kilimo huyo, kumsaidia mwekezaji wa kiwanda cha kukoboa mpunga na kuupa viwango Mchele (Grade) Mabera Ilumba, kupata kibali cha ubora wa bidhaa zake kwenye Shirika la viwango Tanzania (TBS), ili auze mchele huo kiwango cha kimataifa na kukua kiuchumi.

Awali Mwekezaji wa kiwanda hicho cha kukoboa zao la Mpunga Mabera Ilumba, alilamika kuwa amekuwa wakisotea kupata kibali cha ubora (TBS) zaidi ya miaka mitatu sasa, na hivyo kumkwamisha kuuza Mchele huo katika Soko la kimataifa na kubaki kudumaa kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza na wananchi wilayani Kishapu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza na wananchi wilayani Kishapu.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiwa kwenye kiwanda cha kukoboa zao la Mpunga na kuupa viwango mchele (Grade) katika kiwanda cha bwana Mabera Ilumba

Mashine za kukoboa zao la mpunga.

Zao la Mpunga likiwa katika magunia ndani ya kiwanda hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiwa ndani ya kiwanda cha kutengeneza Mafuta kwa kutumia Malighafi ya zao la Karanga na Alizeti.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiwa kwenye ziara wilayani Kishapu.

Na Marco Maduhu- KISHAPU.




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464