RC MJEMA AKAGUA UJENZI VYUMBA MADARASA USHETU, VIJANA WAMPOGEZA RAIS SAMIA KUTOA AJIRA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

Na Marco Maduhu, KAHAMA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ameendelea na ziara ya ukaguzi ujenzi wa vyumba vya Madarasa mkoani humo, ambapo amehitimisha ziara hiyo katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa vyumba hivyo vya Madarasa.
Mjema amehitimisha ziara hiyo leo, akiwa ameambatana na viongozi wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kamati ya ulinzi na usalama , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Linno Mwageni, pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Halmashauri hiyo ya Ushetu, amepongeza kasi ya ujenzi huo, ambapo maboma mengi yapo kwenye hatua ya Renta, na upauaji, huku akitaka kasi iongozeke zaidi, na ifikapo Novemba 20 wawe wamesha mkabidhi Madarasa hayo.

“Nawapongeza Halmashauri ya Ushetu kwa hatua nzuri mliyofikia ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa, mpo katika hatua ya Renta, na Madarasa mengine mmeshaanza kupaua, mnastahili Pongezi,”alisema Mjema.

“Nimekagua Madarasa haya vizuri, nimeona pia yana ubora wa hali ya juu, yani mmekwenda na kasi nzuri pamoja na kuzingatia ubora wa majengo, kwa kweli mmefanya kazi nzuri,”aliongeza Mjema.

Nao baadhi ya vijana walimshukuru Rais Samia, kwa kutoa fedha za ujenzi wa vyumba vya Madarasa nchi nzima, ambapo wamepata ajira ya muda mfupi na kujipatia kipato na kuendesha maisha yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama Linno Mwageni, alisema Halmashauri hiyo imepokea fedha za ujenzi wa vyumba vya Madarasa Sh. bilioni 1.5 huku akiahidi kuendelea kusimamia ujenzi huo ili ukamilike kwa wakati.

Aidha, Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, alisema katika wilaya hiyo wamepokea fedha za ujenzi wa vyumba vya Madarasa kiasi cha Sh.bilioni 5,5 kwa ajili ya kujenga Madarasa 247, ambapo yote yapo kwenye hatua nzuri za ukamilishaji.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza kwenye ukaguzi wa vyumba vya Madarasa Halmashauri ya Ushetu, na kupongeza kasi ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kahama Thomas Myonga akizungumza kwenye ukaguzi wa vyumba vya Madarasa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

Vijana wakimpongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha za ujenzi wa vyumba vya Madarasa ambapo wamepata ajira na kujipatia kipato na kuendesha maisha yao.

Mwanamke Magret Peter akiponda kokoto kwenye ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Uyogo Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama na kujipatia Kipato, huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa utoaji wa fedha za ujenzi wa vyumba vya Madarasa.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Dakama Halmashauri ya Ushetu.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiwa kwenye ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Dakama Halmashauri ya Ushetu.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Kisuke Halmashauri ya ushetu.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Kisuke.

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Kisuke.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (katikati) akishiriki kushusha Saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Kisuke, (kulia) ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Uyogo Halmashauri ya Ushetu.

Muonekano wa ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Uyogo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akikangalia mbao ambazo zinatumika kutengeneza Kenchi katika ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Uyogo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Msingi Shikizi ya Senai Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

Muonekano wa ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Msingi Shikizi ya Senai.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiangalia Kenchi ambazo zinatarajiwa kuwekwa kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule Shikizi ya Senai.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (katikati) akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa Halmashauri ya Ushetu, (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga.

Na Marco Maduhu- KAHAMA.

















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464