Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akisikiliza kero za wananchi Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama na kuzitafutia ufumbuzi.
Na Marco Maduhu, KAHAMA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amefanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi katika Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkutano huo umefanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Segese na kuhudhuliwa pia na viongozi mbalimbali wa Serikali, wakuu wa idara wa Halmashauri ya Msalala, vongozi wa chama cha Mapinduzi CCM, Diwani wa Kata hiyo Joseph Manyara, Mkurugenzi wa Msalala Charles Fussi, pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga.
Mjema akizungunza na wananchi hao, amesema Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassani, ipo pamoja na wananchi wake kwa kusikiliza kero zao pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
“Mimi nilikuwa kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, lakini nikaona ni siishie tu kukagua madarasa hayo, bali nizungumze na wananchi kusikiliza kero zenu na kuzitafutia ufumbuzi,” alisema Mjema.
“Kabla ya kuanza kusikiliza kero zenu, naomba wananchi muendelee kumuunga Mkono Rais wetu Samia Suluhu Hassani katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,”aliongeza.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa, aliwataka wananchi kwenye msimu huu wa kilimo (2021-2022) wajikite zaidi kulima mazao ya muda mfupi ambayo yanastahimili ukame, ilikuendana na hali ya hewa ya mwaka huu, kuwa kutakuwa na mvua chache, hivyo ni vyema wakalima mazao hayo ambayo yatawakomboa kwenye baa la njaa hapo baadae.
Aidha wananchi hao wa Segese wakitoa kero zao kwa Mkuu wa Mkoa, walilalamikia suala la kuchelewa kufungiwa Mita za umeme kwenye nyumba zao, ambapo kila wakifuatilia wamekuwa wakizungushwa, pamoja na kutopelekewa umeme kwenye machimbo ya migodi ya madini ya dhahabu.
Kero zingine ni ukosefu wa wodi kwa ajili ya kujifungua akina mama wajawazito, upandaji wa bei za pembejeo za kilimo hasa mbolea, ambayo imepanda kutoka kuuzwa Sh. 58,000 kwa mfuko wa kilo 50, hadi kufikia Sh. 120,000, ubovu wa miundombinu ya barabara, pamoja na utitiri wa kodi kwenye madini.
Akitafuta ufumbuzi wa kero hizo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ilibidi awapigie simu watu wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na Ofisi ya Madini, ambao hawakuwepo kwenye mkutano huo, na kutoa majibu kwa wananchi na kuahidi kuzishughulikia kero hizo..
Katika utatuzi wa kero zingine, zilijibiwa na wakuu wa idara ya Halmashauri ya Msalala, na zingine kuzielekeza kwenye menejimenti ya Halmashauri hiyo ili zifanyiwe kazi, ambapo yeye atafanya ziara tena kuona utekelezaji wake.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Charles Fussi, pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, walisema maelekezo yote ambayo ameyatoa Mkuu huyo juu ya ufumbuzi wa kero hizo za wananchi watazifanyia kazi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara.
Diwani wa Kata ya Segese Joseph Manyara, akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara.
Wananchi wa Segese wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Mwananchi wa Segese Mastaigo akitoa kero yake kwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga kwenye mkutano huo wa hadhara.
Wananchi wa Segese wakiendelea kutoa kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akisalimia na viongozi mbalimbali alipofika kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Na Marco Maduhu- KAHAMA.
Na Marco Maduhu- KAHAMA.