RC MJEMA AZINDUA BODI MPYA YA USHAURI HOSPITALI YA RUFAA MKOANI SHINYANGA, ATAKA SHINYANGA KUWA KITUO CHA COSMETIC SURGERY


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (wapili kushoto), akikata utepe kuzindua Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga, (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Frank Samweli, (kushoto) Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga Dk. Luzila John, (katikati) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amezindua Rasmi Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali ya Rufani mkoani humo, na kuitaka ifanye kazi kwa ufanisi na kutoa ushauri mzuri, ili kuboresha huduma za Afya katika Hospitali hiyo.

Mjema amezindua Bodi hiyo leo, kufautia bodi iliyopita kumaliza muda wake mwaka jana, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano katika Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga, na kuhudhuliwa pia na mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Dk. Anjelina Sijaona.

Alisema, Bodi ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, ni chombo muhimu sana katika uendeshaji wa huduma za Afya za Hospitali za Mkoa, na ndiyo kiunganishi kikubwa cha wananchi na Serikali yao ngazi ya Hospitali ya Rufaa, katika utoaji wa huduma za matibabu.

“Bodi hii ina wakilisha wananchi katika kufanya maamuzi juu ya utoaji wa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, na bodi inaweza kufananishwa na kioo ambacho Menejimenti ya Hospitali ina kitumia kupata mrejesho wa namna wanavyotoa huduma za matibabu kwa wananchi,”alisema Mjema.

“Bodi hii teule, imeteuliwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto Dk. Dorothy Gwajima tangu june 18 mwaka huu, na itahudumia hadi June 16, 2024, naomba mkafanye kazi kwa uaminifu mkubwa, kama milivyoaminiwa na Waziri, na muishauri na kuisimamia vizuri Menejimenti ya hospitali katika utekelezaji wa majukumu yake,”aliongeza.

Aidha, alisema Matarajio ya Serikali kwa bodi hiyo, ni kuona huduma za Afya zinaboreshwa zaidi katika Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga, pamoja na kubuni kutafuta misaada mbalimbali kupitia wadau, ili kuhakikisha upatikanaji wa Vifaa Tiba zinakuwepo vya kutosha na kuendesha Hospitali.

Akizungumzia suala la upungufu wa watumishi katika Hospitali hiyo ya Rufani mkoani Shinyanga, alisema watalifikisha kwenye sehemu husika, ili wakati wa uzalishaji wa Madaktari na wauguzi wapate mgao mkoani humo, wakiwamo Madaktari wa upasuaji.

Pia, alisema anatamani bodi hiyo mpya ifanye ubunifu wa hali ya juu kwa kufikilia mambo makubwa zaidi, na hata kuifanya Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga kuwa kituo cha Hospitali ya utalii, na kituo maalumu cha kuboresha muonekano wa maumbile (Cosmetic Surgery) na watu kuja Shinyanga kupata huduma na kuongeza Mapato ya Hospitali, na kuacha kwenda Afrika Kusini.

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga Frank Samweli, alimwahidi Mkuu huyo wa Mkoa, kuwa maelekezo yote ambayo ameyatoa watayafanyia kazi, ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Awali Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga Dk. Luzila John, akisoma taarifa ya hospitali hiyo, alisema wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi wa Afya asilimia 65, ambapo wanawatumishi 241 na upungufu 689.

Pia amesema hospitali hiyo kupitia fedha za IMF imetengewa kiasi cha Sh. bilioni 4.5 kwa ajili ya kujenga chumba cha uangalizi wa karibu (ICU), chumba cha CT-SCAN, EMG, na kununua mashine ya CT-SCAN, ili kuondoa changamoto ya wagonjwa kupewa Rufaa kwenda Bugando Jijini Mwanza, sababu ya ukosefu wa huduma hizo.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dk. Faustine Mulyutu, alisema Hospitali hiyo pia inatarajia kukopa Mashine ya kuchujia Figo kutoka Bohari ya Madawa MSD, ili kuendelea kuboresha huduma za matibabu katika Hospitali hiyo ya Rufaa Mkoani Shinyanga.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (wapili kushoto), akikata utepe kuzindua Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga, (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Frank Samweli, (kushoto) Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga Dk. Luzila John, katika ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk, Faustine Mulyutu, akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga Dk, John Luzila, akitoa taarifa ya Hospitali hiyo kwenye uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri katika Hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga Frank Samweli, akitoa neno la Shukrani mara baada ya bodi hiyo kuzinduliwa.

Mwakilishi kutoa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk.Anjelina Sijaona.

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga.

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga.

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga.

Wajumbe wa Bodi ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga , wakipiga picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Picha ya pamoja ikiendelea kupigwa.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) akiwasili kwenye Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga kuzindua Bodi ya ushauri ya Hospitali hiyo, kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dk. John Luzila.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.










Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464