TAKUKURU SHINYANGA YAONDOA MIANYA YA RUSHWA MIRADI YA BILIONI 3.7

Mkuu wa TAKUKURU mkoani Shinyanga Hussein Mussa, akizungumza na vyombo vya habari.

Na Estormine Henry, SHINYANGA.

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa( Takukuru) mkoa wa Shinyanga imefanikisha kuthibiti mianya ya rushwa katika miradi ya maendeleo yenye thamani ya Sh. bilion 3.7 katika mkoa wa Shinyanga.

Haya yameelezwa leo Novemba 2, 2021 Mkuu wa TAKUKURU mkoani Shinyanga Husein M.Mussa , wakati akitoa taarifa ya taasisi hiyo kwa vyombo vya Habari mkoani humo kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022( Julai- Septemba,2021).
Alisema kuwa ofisi yake ilifuatilia miradi ya maendeleo 10 ambayo inatekelezwa mkoa wa Shinyanga yenye thamani ya Sh. bilion 3.7 katika sekta ya kilimo,afya, na miundo mbinu ya barabara.
Alifafanua kuwa katika hiyo 10 ambayo waliifuatilia na kutoa ushauri ifanyiwe marekebisho, miradi 6 imekamilika na miradi minne(4) inaendelea kutekelezwa na ipo katika hatua za utekelezaji.

Aidha, Takukuru Mkoa wa Shinyanga ilifanya uchambuzi katika mfumo wa halmashauri 3 katika mkoa wa Shinyanga na kubaini kuwepo kwa mianya ya rushwa

" Uchambuzi umebaini kuwepo mapungufu ya uwepo wa mianya ya rushwa katika mapato ya stendi ya mabasi maganzo,ukusanyaji wa ada za maegesho ya vyombo vya usafiri manspaa Shinyanga na mfumo wa usimamizi wa mitihani chuo cha VETA shinyanga na Kahama"

Takukuru katika utekekezaji wa shughuli zake katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2021/2022 imepokea malalamiko 46 ikiwa ni serikali mitaa 15,elimu 6,ardhi 4,madini 4,ujenzi 3,afya 2,siasa 2,fedha 2,biashara 2,mahaka 2,kazi 2,maliasili 1 na barabara 1.


Mkuu wa TAKUKURU mkoani Shinyanga Hussein Mussa, akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464