Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
UMOJA wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga, umempongeza Rais Samia Suluhu Hassani, kwa utoaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa, vituo vya afya, pamoja na fedha za mikopo asilimia 10 za Halmashauri ambazo zimesaidia kuinua vijana kiuchumi.
Pongezi hizo zimetolewa leo na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, wakati alipoambatana na baadhi ya wajumbe wa umoja huo, kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa, vituo vya afya, pamoja na vikundi vya vijana vya ujasiriamali katika Manispaa ya Shinyanga.
Alisema anampongeza sana Rais Samia kwa ujenzi huo wa vyumba vya Madarasa, ambao utamaliza changamoto ya wanafunzi kusoma katika mazingira yasiyo rafiki, pamoja na ujenzi wa vituo vya afya ambavyo vitaboresha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi na kuokoa afya zao hasa kwa akina mama wajawazito.
“Nimetembelea ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Uhuru na Shule Shikizi ya Mwamagulya, nimeridhishwa na hatua ya ujenzi huo, ambapo majengo yapo kwenye hatua ya upauaji, na imani hadi kufikia Decemba 15 yatakuwa yamekamilika, na mwakani kuanza kutoa huduma kwa wanafunzi,” alisema Shemahonge.
“Nimeona pia ujenzi wa kituo cha Afya Ihapa-Oldshinyanga kipo katika hatua nzuri, na sina budi kumpongeza Rais wetu Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa ambayo anaifanya ya kuleta maendeleo hapa nchini, pamoja na wasaidizi wake wote wakiwamo Mawaziri, Wabunge, Madiwani, Wakuu wa Mikoa na Wilayani, hii ndiyo dhana ya utekelezaji wa ilani ya Chama kwa vitendo,”aliongeza.
Pia, aliwapongeza wananchi kujitoa nguvu kazi katika ujenzi wa vyumba hivyo vya Madarasa, na vituo vya afya, na kubainisha kuwa nchi hua ina jengwa na wananchi wenyewe, na kuwaomba waendelee kuunga juhudi za Rais Samia za kuwaletea maendeleo.
Katika hatua nyingine, Shemahonge alifurahishwa na namna vijana wanavyo changamkia mikopo ya Halmashauri asilimia 10, ambayo Nne kwa vijana na wanawake, Mbili watu wenye ulemavu, kuwa fedha hizo zimekuwa chachu ya vijana kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali za kuwaingiza kipato, ikiwamo ufugaji kuku, na utengenezaji wa Magodoro.
“Nawapongeza vijana ambao mmethubutu kujiunga kwenye vikundi vya Ujasiriamali, na kufanya shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato, na kuacha dhana ya kukaa vijiweni na kulalamika hakuna ajira na wakati kuna fursa nyingi ambazo mtajiajiri wenyewe na kuendesha maisha yenu, natoa wito kwa vijana wengine changamkieni mikopo ya Halmashauri mjikwamue kiuchumi,”alisema Shemahonge
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Elisha Robert ambaye ni Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo, alisema wanajenga vyumba vya Madarasa 44, Sekondari 35 na Msingi Tisa, ambavyo vyote kwa sasa vipo katika hatua nzuri, pamoja na ujenzi wa kituo hicho cha Afya Oldshinyanga.
Naye Afisa vijana wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Charles Luchagula, akizungumzia suala la utoaji mikopo, alisema katika mwaka wa fedha (2020-2021) wametoa kiasi cha fedha Sh. milioni 170 kwa vikundi vyote vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, na wamekuwa wakifuatilia maendeleo yao na kutatua changamoto ambazo zinawakabili.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM, (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (kulia) akizungumza mara baada ya kukagua na kushiriki ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari uhuru, (kushoto) ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM, (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akishiriki ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Sekondari uhuru, (kulia) ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, akiwa amebeba Tofali kushiriki ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa na Ofisi katika Shule ya Sekondari. Uhuru Manispaa ya Shinyanga ,alipofanya ziara kukagua ujenzi wa vyumba hivyo.
Diwani wa Kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga GulaamHafeez Mkadamu, akishiriki ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Uhuru.
Zoezi la kushiriki ujenzi wa vyumba vya Madarasa likiendelea katika Shule ya Sekondari Uhuru.
Muonekano wa ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Uhuru.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) Baraka Shemahonge (kulia), akishiriki ujenzi wa Kituo cha Afya Oldshinyanga, alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo, (kushoto) ni Mwenyekiti wa (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) Baraka Shemahonge (katikati), akiwa katika kituo cha Afya Olshinyanga, alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo, (kulia) ni Mwenyekiti wa (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua na (kushoto) ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Elisha Robert.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM)Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule Shikizi ya Mwamagulya Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, (kushoto) akiangalia mradi wa vijana wa ufugaji kuku katika Kata ya OldShinyanga.
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, (katikati) akiangalia mradi wa vijana wa ufugaji kuku katika Kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga.Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, (wapili kulia) akisikiliza maelezo ya Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha utengenezaji Magodoro Manispaa ya Shinyanga Ally John.
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, (kushoto) akiwa katika kikundi cha vijana cha utengenezaji wa Magodoro Manispaa ya Shinyanga, kulia ni Mwenyekiti wa kikundi hicho Ally John.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (watatu kutoka kulia) akiwa na baadhi ya viongozi na wajumbe wa umoja huo na wataaam wa Manispaa ya Shinyanga, wakiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa , kituo cha Afya na vikundi vya vijana vya ujasiriamali.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.