WAKAZI SHINYANGA WAJITOKEZA KUPATA VIPIMO NA MATIBABU YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA.

Mwananchi akiendelea kupata vipimo vya awali vya Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo Presha na Suakri.

;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;
Picha na Michael  Solomon-Shinyanga Press Club Blog.

Wakazi wa Manispaa na Mkoa wa Shinyanga wamejitokeza kupata huduma za Matibabu ya Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, huduma iliyokuwa ikitolewa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo kwa muda wa siku mbili.

Mratibu wa huduma za  lishe hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni mratibu wa  Magonjwa yasiyoambukiza Mkoa,na Mwenyekiti wa Chama Cha Magonjwa yasiyoambukiza Kanda ya Ziwa  Bi. Lucy Kanoni amesema kuwa jamii ya Mkoa huo na kanda ya ziwa haina utaratibu wa kupima afya mara kwa mara, hivyo hujikuta wamefikia hatua mbaya zaidi  za ugonjwa ikiwemo Sukari, Shinikizo la damu na  Moyo.

Lucy amesema kuwa wameamua kutoa elimu  ili waelewe magonjwa hayo na kuwawezesha kuchukua tahadhari pamoja na kufanya vipimo kwa wnanachi mbalimbali ili kubaini viashiria vya magonjwa  na kuchukua tahadhari zaidi.

Jukumu letu ni kuhakikisha, tunatoa elimu ya kutosha kwa umma juu ya magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza ili wananchi wachukue hatua za kujilinda na kujikinga dhdi yake alisema Bi Lucy Kanoni.

Lucy ameongeza kwa kusema kuwa lengo la hospitali na Mkoa ni kuona mwananchi yeyote haingii kwenye  magonjwa  hayo sababu akiingia huko si rahisi kutoka, hivyo jamii inapswa kubadilika ikiwemo mwenendo. 

 Magonjwa haya ni hatari sana  mfano Presha,Moyo na Mishipa ya damu, Kishukari na baadhi ya Kansa, Pumu, Figo na Selimundu(Sicocell) ambapo tunapomubaini mtu kuwa amepatwa na magonjwa haya huwa tunawaanzishaia huduma na matibabu Alisema Lucy ."

Katika hatua nyingine Lucy amesema kuwa Moa wa Shinyanga umeendelea kuwa na ongezeko kubwa  la wagonjwa wanaotokana na Magonjwa yasiyoambukiza ambapo kwa wiki moja wagonjwa wa presha na moyo  wapatao 10 ubainik.

“Kliniki zetu huwa tunafanya siku ya Jumanne tu kwa wiki moja, lakini uwa tunakuwa na wagonjwa wengi sana hivyo huwa tunakuwa na wagonjwa wapatao 60 hadi 80  ambao wanakuja kliniki na kwa upande wa sukari kila wiki tunapata wagonjwa wanne, hii inatokana na Magonjwa haya kutokuwa na dalili za wazi ambazo mgonjwa anaweza kuona na kuelewa haraka"Alisema Lucy .

Katika hatua nyingine Lucy ameeleza, kuwa mitindo ya Maisha ambayo watu wanaishi kwa sasa ndiyo unachangia watu wengi kukutwa na magonjwa hayo ambapo amezitaja baadhi ya sababu zinazochangia  magonjwa ya sukari moyo ikiwemo ulaji usiozingatia utaratibu, kutofanya mazoezi,matumizi ya tumbaku na matumizi makubwa ya pombe.

Kwa upande wake Muuguzi  katika hospitali  ya rufaa Mkoa wa Shinyaga ambaye ni miongoni mwa watoa huduma waliokuwa wakitoa huduma  kwa wananchi mbalimbali Bi Christina Jacob Kulima amesema kuwa zoezi hilo limekwenda vizuri na zaidi ya wakazi 110 wamefikiwa na huduma hiyo kwa muda wa siku mbili ambazo walikuwa wakitoa huduma na kupatiwa vipimo pamoja  na Ushauri na Nasaha  

Hata hivyo Christina amesema kuwa kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na wizara ya afya mwaka 2012 zilibainisha kuwa katika watu 100  wenye umri wa miaka 25 na kuendelea watu 9 wana kisukari, watu 26 wana shinikizo la juu la damu na watu 25 wana mafuta mengi kwenye damu huku 34 wakiwa na uzito uliopitiliza.

Selemani Omary  ni mkazi wa Ibinzamata  ameishukuru hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa kutoa huduma ya vipimo  vya magonjwa yasiyoambukiza bure  kwa wananchi na kuwataka vijana na makundi mengine kujenga tabia ya kupima mara kwa mara ili kubaini afya zao hali itakaowasaidia kuchukua tahadhari mapema 

 Omary ameongeza kuwa jamii kubwa ya kitanzania haina utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara hali inayochangia kukumbwa na magonjwa hayo  ambayo huwa hayaonyeshi dalili zake mapema.

Naye  Bi Nemetua Petro Mkazi wa Ngokolo ameishukuru hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa kutoa huduma bure kwa wananchi kwa kuwa wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

Tazama Picha katika Matukio.

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wakiendelea kupata Vipimo na ushauri wa Magonjwa yasiyoambukiza.
Zoezi la utaoji huduma na matibabu kwa wakazi waliofika  kupata huduma Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga 
Zoezi la utoaji wa huduma likiendelea 
Wananchi wakienedelea kusubiri kupata matibabu na vipimo vya magonjwa ya kisukari na presha.
Zoezi la upimaji wa urefu na uzito kwa wananchi waliofika kupata vipimo na matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga. 
Mratibu wa huduma za  lishe hospitali ya Mkoa wa Shinyanga na  Magonjwa yasiyo ya kuambukiza Mkoa wa Shinyanga Lucy Kanoni akizungumzia juu ya ongezeko la Magonjwa yasiyo ya kuambukiza  









Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464