WAZIRI WA UWEKEZAJI MWAMBE ATEMBELEA KIWANDA CHA JAMBO NA JIELONG, AACHA UJUMBE HUU KWA WATANZANIA HASA WANANCHI WA SHINYANGA…


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Geoffrey Mwambe, (Wanne kutoka Kushoto) akiwa kwenye kiwanda cha Jambo

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Geoffrey Mwambe, ametembelea kiwanda cha Jambo na Jeilong, na kutoa wito kwa Watanzania hasa wakazi wa mkoani Shinyanga kuchangamkia fursa za kulima mazao na kupanda matunda, ambayo yatatumika kwenye viwanda hivyo ambavyo hutumia maligafi hizo kutengeneza bidhaa.

Mwambe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini, alibainisha hayo jana wakati alipotembelea kwenye viwanda hivyo cha Jambo, na Jielong vilivyopo Manispaa ya Shinyanga, ambavyo hutumia maligafi ya mazao na matunda kutengeneza bidhaa zao, yakiwamo Maembe, Ukwaju, Pamba, Alzeti, Soya, na Kalanga.

Amesema, Watanzania wana fursa nyingi sana za kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo cha mazao na matunda, ambapo Serikali imehamasisha wawekezaji wengi kuja hapa nchini wakiwamo na wazawa, kuwekeza viwanda vya kutengeneza bidhaa kwa kutumia maligafi za hapa nyumbani ili wananchi wainuke kiuchumi.

“Nimetembelea kiwanda cha Jambo, nimeona shughuli zao za uzalishaji mali, ambapo wanatumia maligafi za hapa nyumbani kabisa kama vile Maembe na Ukwaju tofauti na viwanda vingine, jambo ambalo nimefurahishwa nalo,”amesema Mwambe.

“Lakini nimetembelea kiwanda cha utengezaji mafuta ya kupitia cha Jielong, nimekutana na changamoto ya upungufu wa maligafi ya utengezaji wa mafuta hayo, hivyo naomba wananchi mchangamkie fursa mlime Pamba kwa wingi, Alzeti, Soya, na Kalanga sababu soko lipo la kutosha,”ameongeza Mwambe.

Katika hatua nyingine Waziri Mwambe, alisema kama tatizo hilo la ukosefu wa Maligafi kwenye viwanda likiendelea, itabidi wafanye utaratibu wa kuingia Mkataba na wakulima kwa kuwakopesha Pembe Jeo za kilimo, ili wakivuna mazao wakauze kwenye viwanda hivyo.

“Tukifanikiwa kupata Maligafi za kutosha kwenye viwanda vyetu hivi, tutakuwa na mafuta ya kutosha na kupunguza matumizi ya mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi, ambapo kwa Tanzania tunatumia mafuta kutoka nje kwa asilimia 84,” alisema Mwambe.

Kwa upande wake Meneja wa kiwanda cha Jielong, Shang- Jie, alisema changamoto kubwa ambayo inawakabili kwenye kiwanda hicho cha utengenezaji wa mafuta ya kupikia, ni upungufu wa maligafi, ambapo kwa sasa wamebakiwa na maligafi ya akiba ambayo nayo ni kidogo, na ikiisha watafunga kiwanda kwa muda.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Geoffrey Mwambe (kulia) akisikiliza maelezo ya uzalishaji bidhaa kwenye kiwanda cha Jambo, kushoto ni Mmiliki wa kiwanda hicho Salum Khamis.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Geoffrey Mwambe (kulia) akitembelea kiwanda cha Jambo, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Geoffrey Mwambe, (kushoto) akiangalia uzalishaji wa Pipi kwenye kiwanda cha Jambo, (wapili kulia) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akifuatiwa na Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Jambo Khamis Salum.
Waziri Mwambe akiendelea kuangalia uzalishaji wa bidhaa kwenye kiwanda cha Jambo.

Muonekano wa uzalishaji wa Maji kwenye kiwanda cha Jambo.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Jambo, wakiendelea na zoezi la upangaji Maembe kwa ajili ya kutengeneza Juice.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Geoffrey Mwambe, (katikati) akiangalia uzalishaji wa bidhaa katika Kiwanda cha uchakataji Mafuta ya kula cha Jielong, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, na kulia ni Meneja wa kiwanda hicho Shang-Jie.
Zoezi la uangaliaji wa bidhaa katika kiwanda cha Jielong likiendelea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Geoffrey Mwambe, (katikati) akiwa katika kiwanda cha Jielong, (kulia) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, na (kushoto) ni Meneja wa Kiwanda hicho Shang-Jie.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Geoffrey Mwambe, (kulia) akiwa katika kiwanda cha Jielong, (katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, na (kushoto) ni Meneja wa Kiwanda hicho Shang-Jie.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.






























Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464