Mkurugenzi wa Shirika la Global Network Of Religion For Children (GNRC) Tanzania Joyce Mdachi, akielezea madhumuni ya kuja mkoani Shinyanga na kuunganisha nguvu na Shrika la Agape kufanya Kampeni ya kutokomeza matukio ya kingono dhidi ya watoto wadogo, likiwemo tatizo la mimba na ndoa za utotoni.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
SHIRIKA la Agape na GNRC wameunganisha nguvu ya pamoja katika kuendeleza mapambano ya kutokomeza matukio ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto wadogo zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.
Mashirika hayo mawili shughuli zao kubwa ambazo wanazifanya ni kutetea haki za watoto, pamoja na kuzuia matukio ya kingono dhidi ya watoto wadogo ili watimize ndoto zao.
Mkurugenzi wa Shirika la Global Network Of Religion for Children (GNRC) Tanzania Joyce Mdachi, anabainisha hayo leo Decemba 11,2021, wakati walipokutana na makundi mbalimbali wakiwamo viongozi wa dini, wazazi, dawati la jinsia, viongozi wa Kata, Maofisa Maendeleo na Ustawi wa jamii Manispaa ya Shinyanga, kujadili namna ya kutokomeza matukio ya kingono dhidi ya watoto.
Alisema baada ya kusikia kazi za Shirika la Agape ambazo wanazifanya za kupigania haki za watoto likiwamo suala la mimba na ndoa za utotoni, ndipo wakaona ni vyema kuunganisha nguvu za pamoja na Shirika hilo, ili kutokomeza matukio hayo ya kingono dhidi ya watoto wadogo.
“Baada ya kuunganisha nguvu na Shirika hili la Agape, tukaona sasa ni vyema tukutane na watu ambao wanashirikiana nao katika mapambano haya ya kupinga ukatili dhidi ya watoto wadogo ili tupange mpango mkakati wa kuendeleza mapambano haya na watoto wetu waisha salama na kutimiza ndoto zao,”alisema Mdachi.
“Matarajio yetu kama Shirika la GNRC baada ya kuunganisha nguvu za pamoja na Shirika la Agape na nyie wadau mkiwamo viongozi wa dini, ni kubadilisha mitazamo na tamaduni mbalimbali ambazo zinaleta madhara kwa watoto, kuwa na vitega uchumi mbadala kwa wazazi na siyo kutegemea kuozesha watoto ndoa za utotoni, pamoja na mitazamo ya kisera na sheria,”aliongeza.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola, alisema matukio ya ukatili mkoani humo bado yapo, ambapo wadau, mashirika, jamii, na viongozi wa dini wanapaswa kuunganisha nguvu ya pamoja kupaza sauti, juu ya kutokomeza vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto.
Ametaja baadhi ya vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto wadogo kuwa ni ubakaji, vipigo, matusi, kuozesha wanafunzi ndoa za utotoni, pamoja na kuwapatia ujauzito na kuzima ndoto zao.
Nao baadhi ya washiriki warsha hiyo akiwamo kiongozi wa dini Sheikh Hamisi Nkingo kutoka Msikiti wa Mabambase Ngokolo Manispaa ya Shinyanga, walisema wazazi wanapaswa kubadilika na kujikita kwenye malezi bora ya watoto wao, pamoja na kufuatilia mienendo yao na kuwa nao karibu, ili kubaini kama wanafanyiwa vitendo vichafu na kuchukua hatua mapema kabla ya kupata madhara.

Mkurugenzi wa Shirika la Global Network Of Religion For Children (GNRC) Tanzania Joyce Mdachi, akielezea madhumuni ya kuja mkoani Shinyanga na kuunganisha nguvu na Shrika la Agape kufanya Kampeni ya kutokomeza matukio ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto wadogo, likiwemo tatizo la mimba na ndoa za utotoni.
Mkurugenzi wa Shirika la Global Network Of Religion For Children (GNRC) Tanzania Joyce Mdachi, akizungumza kwenye Warsha hiyo na kuelezea madhara ya matukio ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto.
Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola akizungumza kwenye Warsha hiyo na kuelezea namna wanavyofanya kazi ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya watoto wadogo, zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.
Afisa Program kutoka Shirika la (GNRC) Venance Tem, akizungumza kwenye Warsha hiyo.
Mratibu wa dawati la jinsia kutoka Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga Brightoni Rutajama, akizungumza kwenye Warsha hiyo.
Sheikh Hamis Nkingo kutoka msikiti wa Mabambase Ngokolo Manispaa ya Shinyanga, akichangia kwenye Warsha hiyo.
Washiriki wakiwa kwenye Warsha hiyo.
Washiriki wakiwa kwenye Warsha hiyo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo kwa vitendo.

Washiriki wakiwa kwenye mpango kazi namna ya kutokomeza matukio ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto wadogo mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.