Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
kamisaa wa Sensa ya watu na makazi Mhe.Anne Makinda akibonyeza kitufe
kuzindua matumizi ya mfumo wa anwani za makazi jana Jijini Mwanza.Kulia
kwake ni Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Mhe.Dkt.Ashatu kijaji na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mhe.Robert Gabriel
Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kamisaa wa
Sensa ya watu na makazi Mhe.Anne Makinda akimkabidhi Mkuu wa WIlaya ya
Nyamagana Bi.Amina Makilagi kibao chenya anwani za makazi jana katika
uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa anwani za makazi jijini Mwanza
Wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Mwanza wakiwa katika viwanja vya Shule ya Msingi Buhongwa kwa ajili ya uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa anwani za makazi.
Na Daudi Manongi, WHMTH, Mwanza
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Mhe. Anne
Makinda amesema Mfumo wa anwani za makazi utaisaidia Serikali kupanga
mipango ya Maendeleo, kuimarisha usalama, kuongeza ajira na Mapato ya
Serikali.
Mhe. Makinda ameyasema hayo leo wakati akizindua mfumo
huo katika viwanja vya shule ya msingi Buhongwa B kata ya Mkolani Wilaya
ya Nyamagana Jijini Mwanza.
“Nazipongeza Wizara ya Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, TAMISEMI, Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi na wadau wote kwa ushirikiano wao na jitihada
walizoweka ili kuhakikisha mfumo wa anwani za makazi unatekelezwa katika
nchi nzima”, amesema
Aidha, amesema mfumo huo utaendana na
programu tumizi (mobile application) ya mfumo wa anwani za makazi ambayo
itakayorahisisha matumizi na utekelezaji wa mfumo kwa kuzingatia kwamba
itatumika katika kukusanya taarifa za Barabara, wakazi, makazi pamoja
na kutoa anwani za makazi ya wananchi,kaya, ofisi na eneo la biashara.
“NImeelezwa
kwamba programu tumizi imetengenezwa na wazawa,nitumie fuarsa hii
kuwapongeza wataalamu wetu walioshiriki kuunda programu hii,hongereni
sana vijana wetu,hili ni jambo la kujivunia sana kwani lengo la Serikali
ni kuhakikisha wanatumika katika kuleta maendeleo ya taifa letu”
ameongeza.
Kwa upande mwingine Mhe. Makinda amesema kwa kutumia
utaratibu huu wa anwani za makazi, mpango shirikishi ulioandaliwa baina
ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Ofisi ya Taifa
ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar wa kutekeleza zoezi
hili utasaidia sensa ya watu na makazi ya mwakani kufanyika vizuri
sana kwa sababu pia itaonyesha wananchi wanapokaa na wanafanya kazi
gani.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia
ya Habari Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema mfumo huu wa anwani za makati
ni mfuo mama wa mifumo mingi ya utambuzi.
Watanzania wamekuwa
wakilalamika kuwa na mifumo mingi midogo midogo ambao inayowataka
kujisajili na hivyo mfumo huu tumeweza kuunganisha na mifumo mingine
kama ya afya, NIDA, mfumo wa Mamlka ya Mapato Tanzania kwenye TIN namba,
kusajili makampuni BRELA na mfumo wa usimamizi wa viwanja.
“Kama
Wizara inayosimamia mifumo yote ya Mawasiliano tumekuja na mfumo huu
ili turahisishe maisha ya watanzania kwenye kuyaendea maendeleo ya
mapinduzi ya nne ya viwanda, lengo kuu ni kuondoa usumbufu na malalamiko
ya watanzania”, amesema.
Ameongeza kuwa mwaka huu ni dhamira ya
Wizara kila mwananchi anakuwa na anwani yake ya makazi katika eneo
analoishi, eneo la ajira au eneo la biashara.
Aidha, ametoa wito
kwa watendaji, viongozi na wataalamu hususani wa kata na mitaa kujengewa
uwezo wa kutosha ili waweze kuwa na uelewa wa pamoja,waweze kuratibu,
kusimamia na kutekeleza mfumo huu.
Naye Naibu Waziri wa Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula amesema katika
utekelezaji wa mfumo huu wa anwani za makazi Wizara yake ni mdau mkubwa
katika kuandaa ramani za kidijitali ambazo zinatumika kama ramami za
msingi katika utekelezaji wa anwani za makazi
Bila kuwa na anwani
hizi za kidijitali utekelezaji wake unaweza usiwe rahisi sana kwa
sababu tunawatambua watu wetu na maeneo yao kwa kufuata mfumo huu nitoe
taarifa kuwa ni halmashauri tisa ziko tayari ambazo maandalizi ya ramani
husika yamekamilika, amesema
Naye Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mhandisi Robert Gabriel amesema hadi kukamilika kwa mradi huo kwa
upande wa Halmshauri ya Wilaya ya Nyamagana mradi huo huo umegharimu
kiasi cha shilingi bilioni moja milioni mia sita hamsini na tano fedha
ambazo kwa kiasi kikubwa ziilitolewa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari.
Hivi karibuni wakati Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan wakati akizindua mkakati
wa uelimishaji wa pensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 uwanja wa
Jamhuri jijini Dodoma alisema licha ya uwepo wa tozo za makazi lakini
lengo la Serikali ni kujua anunani za makazi, idadi ya makazi na aina ya
nyumba zilizopo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464