ASKOFU SANGU AKEMEA MATUKIO YA UKATILI WA KIJINSIA, MAUAJI YA WATU WASIOKUWA NA HATIA


Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, akibariki waumini wa Kanisa hilo wakati akiingia kuendesha Misa katika mkesha wa Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa kuu la Mama mwenye huruma Parokia ya Ngokolo Jimbo la Shinyanga.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, amekemea wananchi kuendekeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, pamoja na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

Amebainisha hayo jana kwenye Mkesha wa Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa la Romani Katoliki la Mama mwenye huruma Parokia ya Ngokolo jimbo la Shinyanga.

Alisema Watanzania wengi sasa hivi upendo wao umepungua, na kusababisha kuendelea kuwepo kwa matukio ya ukatili wa kijinsia, pamoja na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia, wakiwamo watoto wadogo ambao bado wapo tumboni hawajazaliwa.

“Upendo katika dunia umepungua, na ndiyo maana kumekuwepo na matukio mengi ya ajabu katika nchi yetu, yakiwemo na ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, pamoja na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia,”alisema Askofu Sangu.

“Leo tuna sheherekea upendo wa mungu kwa kumtoa mwanae Yesu Kristo kuja kutukomboa kwa ajili ya dhambi zetu, hivyo naombeni Watanzania tuishi kwa upendo huo wa Mungu na kuacha kutenda mambo maovu,”aliongeza.

Katika hatua nyingine Askofu Sangu, aliwataka Watanzania kila mmoja kwa imani yake, kuombea hali ya hewa ili mvua zinyeshe kwa wingi, na kusijetokea baa la njaa hapo baadae, ili wananchi walime mazao na kupata chakula.

Pia aliwataka wananchi na waumini wa Kanisa hilo, katika kusheherekea sikukuu ya Christmas na Mwaka Mpya wawe majumbani mwao, na siyo kwenda kufanya mambo ya anasa, huku akitamani kwenye sherehe hizo mvua zinyesha kutwa nzima ili watu wasitoke out (kula starehe).

Aidha, alilipongeza pia Jeshi la Polisi kwa kuzuia disko toto, ambayo imekuwa ikihatarisha usalama wao, na kuwataka wazazi wazuie watoto wao kuzurura hovyo mitaani, bali washinde nao majumbuni na kusheherekea sikukuu pamoja.

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akitoa salamu za Serikali, aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuombea amani ya nchi pamoja na mvua, huku akiwahakikishia wananchi katika sherehe za mwisho wa mwaka wataendelea kudumisha amani na utulivu.

Mboneko alikazia pia kauli ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, kuwa kwa wale walevi na waliojipanga kufanya fujo katika sikukuu hizo, Serikali itawashughulikia na watakula sikukuu wakiwa Mahabusu.


Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, akiendesha Misa kwenye mkesha wa Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa la Mama mwenye huruma Parokia ya Ngokolo.

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, akibariki waumini wa Kanisa hilo wakati akiingia kuendesha Misa katika mkesha wa Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa kuu la Mama mwenye huruma Parokia ya Ngokolo Jimbo la Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akitoa salamu za Serikali kwenye Misa ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi katika Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Ngokolo jimbo la Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (wapili kushoto) akiwa na familia yake, pamoja na waumini wengine wakisali kwenye Misa ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, pamoja na waumini wengine wakiendelea kusali kwenye Misa ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko,akiendelea na Ibada kanisani hapo.
Ibada ikiendelea Kanisani hapo.

Waumini wakiendelea kusali kwenye Misa ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi Kanisani hapo.
Waumini wakiendelea kusali kwenye Misa ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi Kanisani hapo.

Waumini wakiendelea kusali kwenye Misa ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi Kanisani hapo.

Waumini wakiendelea kusali kwenye Misa ya mkesha ya sikukuu ya Krismasi Kanisani hapo.
Ibada ikiendelea.

Ibada ikiendelea.

Ibada ikiendelea.

Wanakwaya wakiingia Kanisani kwa ajili ya Misa ya mkesha ya sikukuu ya Krismasi Kanisani hapo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464