ASKOFU SANGU AMZUNGUMZIA HAYATI MAGUFULI MKESHA MWAKA MPYA 2022


Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, akibariki waumini wa Kanisa hilo, wakati akiingia Kanisani kuendesha Misa ya kuupokea mwaka mpya 2022, katika Kanisa kuu la Mama mwenye huruma Parokia ya Ngokolo Jimbo la Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, amewataka Watanzania kumtanguliza mwenye Mungu kwa kila jambo, kama alivyokuwa akiwasisitiza Hayati Rais John Magufuli, na kutenda yale yaliyomema machoni pa Mungu na kuacha dhambi.

Amebainisha hayo jana kwenye mkesha wa kuuaga mwaka 2021, na kuupokea mwaka mpya 2022, wakati akiendesha Misa katika Kanisa kuu la Mama mwenye huruma la Romani Katoliki Ngokolo Jimbo la Shinyanga.

Alisema chimbuko la mafanikio katika maisha ya Mwanadamu ni kumtanguliza mwenyezi Mungu kwa kila Jambo, kama alivyokuwa akisisitiza Hayati Rais John Magufuli, pamoja na kuruhusu Roho mtakatifu atawale maisha yao, ambapo watakuwa wakitenda mambo mema na kupata Baraka kutoka kwa Mungu.

“Mungu alimtoa mwanaye Yesu Kristo kuja kufia dhambi zetu na sisi tupate ukombozi, hebu tuishi na sisi kwenye huo ukombozi na kuacha kutenda dhambi, na tumtangulize mwenyezi Mungu kwa kila jambo, ili tuwe na upendo, furaha na amani,”alisema Askofu Sangu.

Pia, aliwasisitiza wanadamu wawe na tabia ya kushukuru kwa kila jambo, hata yale mambo ambayo hawapendezwi nayo na siyo kulaumu, sababu kila kinachofanyika hapa duniani kimepangwa na mwenyezi Mungu, pamoja na kujifunza kuombana msamaha wanapokoseana.

Katika hatua nyingine, alisema ana kemea dhambi ya uharibifu wa mazingira, ambayo binadamu hajui kama nayo hiyo ni dhambi, na imekuwa ikiathiri sana mabadiliko ya tabia nchi na kusababisha mvua kutonyesha.

Aidha, aliwataka pia watanzania waendeleze utamaduni wa kusaidia watu wenye uhitaji, pamoja na kuacha kuwanyanyapaa watu wenye virusi vya ukimwi na ukoma.

Nao baadhi ya waumini waliokuwa kwenye mkesha huo wa kuupokea mwaka mpya, kwa nyakati tofauti walisema, wanamshukuru Mungu kwa kuwavusha salama mwaka uliopita, huku wakiahidi kutenda mema zaidi mwaka huu, na kutimiza malengo ambayo wamejiwekea kwa uwezo wa mwenyezi Mungu.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, akiendesha Misa kwenye Mkesha wa kuupokea Mwaka Mpya 2022, katika Kanisa Kuu la Mama mwenye huruma Parokia ya Ngokolo jimbo la Shinyanga.

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, akiendelea kuendesha ak Misa kwenye Mkesha wa kuupokea Mwaka Mpya 2022, katika Kanisa Kuu la Mama mwenye huruma Parokia ya Ngokolo jimbo la Shinyanga.
Waumini wakiwa kwenye Misa ya mkesha ya kuupokea mwaka mpya 2022.

Waumini wakiwa kwenye Misa ya mkesha ya kuupokea mwaka mpya 2022.

Waumini wakiwa kwenye Misa ya mkesha ya kuupokea mwaka mpya 2022.

Waumini wakiwa kwenye Misa ya mkesha ya kuupokea mwaka mpya 2022.

Waumini wakiwa kwenye Misa ya mkesha ya kuupokea mwaka mpya 2022.

Awali Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, akibariki waumini wa Kanisa hilo, wakati akiingia Kanisani kuendesha Misa ya kuupokea mwaka mpya 2022, katika Kanisa kuu la Mama mwenye huruma Parokia ya Ngokolo Jimbo la Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.












Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464