Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mwajuma Magwiza akifungua mafunzo ya Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwa wataalamu wa Sektetarieri za Mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma leo tarehe 11 Desemba, 2021.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sebastian Kitiku akieleza lengo la mafunzo kuhusu Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya mtoto kwa wataalam wa Sektetarieri za mikoa.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya kuhusu programu Jumuishi ya malezi,
makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto kwa wataalamu wa Sektetarieri za
mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma.
Na WAMJW, Dodoma
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Mwajuma
Magwiza amesema changamoto ya ukosefu wa lishe bora ni ukatili kwa
watoto kwani inawasababishia udumavu wa akili na mwili.
Magwiza
ameyasema hayo tarehe 11,desemba,2021 Jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kuhusu
programu Jumuishi ya malezi, makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto kwa
wataalamu wa Sektetarieri za Mikoa nchini yanayofanyika .
Magwiza
ameongeza kuwa, jamii haina budi kufahamishwa namna bora ya malezi kwa
watoto wao katika kila hatua kitaalam zaidi ili kuwajengea watoto
misingi imara ya ukuaji na ujifunzaji.
Amesema
pamoja na kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa watoto vinavyoripotiwa
bado ni vichache lakini pia vitendo hivyo vinasababisha ongezeko la
udumavu.
"Kuanzisha
Kwa programu hii kunawajumuisha wataalamu ikiwemo madaktari ambao wana
Sayansi ya malezi makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto hivyo
watatusaidia katika kuelimisha Jamii,
tunajua
kila mzazi anaamini anatoa malezi kwa usahihi lakini kuna hatua za
malezi za kitaalamu ambazo Jamii zinapaswa kujengewa na washiriki wote
humu kutokana na utaalamu wenu. Huduma za malezi zinatakiwa zimjengee
mtoto Afya, lishe, ujifunzaji na mwitikio" alisema Magwiza.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto Sebastian Kitiku
akieleza lengo la programu hiyo alisema washiriki walioalikwa ni muhimu
sana katika utekelezaji wake wakiwemo Maafisa lishe, Maafisa elimu,
Maafisa Maendeleo na Ustawi wa jamii na Waganga wakuu wa Mikoa.
"Lengo
ni kujenga uelewa wa pamoja kuifahamu programu vizuri ili
itapozinduliwa utekelezaji uanze kwa pamoja wote tukiwa na uelewa"
alisema Bi Mwajuma
Aidha,
vitabu kuhusu programu vimeandaliwa kwa lugha zote mbili lengo pia ni
kutekeleza programu hii kwa ujumuishi wake na Uratibu wa pamoja kwa
kuingiza kwenye mipango yetu ikiwa ni wakati muafaka wa maandalizi ya
bajeti" alisema Kitiku.
Kitiku
aliongeza pia programu hiyo inategemea sana ushiriki wa Serikali kwa
kuweka utekelezaji katika mipango yake na kushirikiana na Wadau
mbalimbali.
Lengo
pia ni kukusanya taarifa Kwa kadri inavyowezekana kulingana na
viashiria vilivyowekwa kwenye kanzidata na wataalam hao watafundishwa
namna ya kukusanya taarifa na kuziingiza kwenye kanzidata hiyo.
Mmoja
wa washiriki wa mafunzo hayo Mwl. Juma Kaponda akizungumza kwa niaba ya
washiriki ameishukuru Serikali kwa kuanzisha programu hiyo ambayo
itasaidia kutoaelimu kwa jamii ili watekekeleze majukumu ya Malezi kwa
watoto.
Kaponda
amesema mafunzo hayo yatawajenga na kuwakumbusha umuhimu wa malezi
sahihi kwa watoto kwani ni muda mrefu wamekuwa kama wamejisahau. Aidha
ameahidi watakwenda kufanya kazi kupitia programu hiyo kwa ufanisi.
Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa
kushirikiana na Wadau wa Maendeleo ya Mtoto imeandaa Programu Jumuishi
ya Kitaifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto
itakayozunduliwa hapo tarehe 13 Desemba, 2021. Programu hii inatekelezwa
kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Ofisi ya
Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais TAMISEMI.
MWISHO
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464