DED MANISPAA SHY: TOZO ZA TAKA ZIPO KISHERIA, WANANCHI WAPATIWE ELIMU.


 Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Jomaary Satura akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo Ijumaa Desemba 3,2021 kuhusu mabadiliko ya tozo za taka katika Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Jomaary Satura akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo Ijumaa Desemba 3,2021 kuhusu tozo taka  katika Manispaa ya Shinyanga.
 
 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Jomaary Satura akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Desemba 3,2021 .

Na Mwandishi wetu-Shinyanga.

Mabadiliko ya Tozo za taka zilizopelekwa na Halmashauri ya Manspaa ya Shinyanga kwa jamii na kuibua hali ya mijadala mbalimbali mwanzo mwa mwezi Desemba,2021 kwa wakazi wa mansipaa ya Shinyanga zimeelezwa kuwa ni sheria ya mazingira na usafi ya mwaka 2014 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2019.
 
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Jomaary M. Satura ameeleza hayo desemba 3,2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari mkoani Shinyanga alipokuwa akitoa ufafanuzi wa tozo hizo mpya za taka kwa wakazi wa manispaa ya Shinyanga kutokana na malalamiko mengi ya wananchi kuhusu tozo hizo.
 
Satura alisema kuwa tozo hizo ni mujibu wa sheria ya usafi na mazingira ya mwaka 2014 na iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 kwa kushirikisha jamii na kuidhinishwa na Waziri wa Tamisemi.Sheria inaelekeza jamii kuwajibika kwa nafasi yao kwa kukusanya taka walizozalisha na manispaa inawajibika kwa uteketezaji wa taka hizo.
 
Satura alieza kuwa awali zoezi la ukusanyaji wa taka kwa jamii lilikuwa linatekelezwa kwa vikundi maalum kutoka ndani ya jamii vilivyokuwa vinatambuliwa na manispaa ya Shinyanga kwa tozo walizoweka wana vikundi na kutakiwa kuwasilisha sehemu ya makusanyo ya asilima kwa ajili ya gharama za uteketezaji wa taka hizo.
 
Halmashauri ya Mansipaa ya Shinyanga ilikuwa inatumia Shs.million 30 kila mwezi kwa shughuli ya kukusanya na uteketeza taka ili kuweka mji safi baada ya vikundi maalum kushidwa kufanya zoezi hilo kwa ufanisi zaidi, Nia yetu ni kuweza kutumia Shs.million 30 kwa maendeleo mengine ya jamii kwa manufaa ya wananchi na hii gharama iliyokuwa kwetu inarudishwa kwa jamii kupitia mkandarasi aliyeingia na mikataba na manispaa’ Alisema Satura.
 
Tutawasisitiza viongozi wa mitaa kuweza kutumia mikutano mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu zaidi kwa wananchi kufahamu sheria hizi juu ya tozo za taka na pia kutumia vyombo vya habari” Alisema Satura
 
Afisa usafi na mazingira wa Manispaa ya Shinyanga, Bwana Kuchibanda.K. Snatus alisema kuwa taka zinazozalishwa manispaa ya Shinyanga ni tani 106 kwa mwezi na uwezo wa manispaa ni kukusanya asilimia 60 ya taka zote kwa manispaa ya Shinyanga.
 
"Mkandarasi anayehusika na kukusanya taka ni kampuni ya  Networking Youth Group ambaye kwa sasa atahusika na kata ya ngokolo,ibinzamata, mjini, Kambarage na dembezi kuanzia mwezi desemba ,2021"Alisema Kuchibanda
 
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464