HABARI ZA USHIRIKA KUNOGESHA TUZO ZA EJAT MWAKANI

Afisa Program kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) Paul Mallimbo, akielezea uingizwaji wa kundi jipya la habari za Ushirika kuwania Tuzo za EJAT mwakani

Na Marco Maduhu, TANGA

BARAZA la Habari Tanzania (MCT), limeongeza kundi la habari za Ushirika, ambalo litashindaniwa mwakani kwenye Tuzo za umahiri za uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) ambazo hutolewa na baraza hilo.

Afisa Program kutoka Baraza hilo la Habari Paul Mallimbo, amebainisha hayo leo Decemba 14.2021 kwenye mafunzo ya waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbalia, ambayo yanafanyika Jijini Tanga namna ya kuandika habari bora ambazo zitakuwa zikishindaniwa kwenye utoaji wa Tuzo hizo za EJAT, mafunzo yaliyofadhiliwa na Taasisi ya utawala wa maliasili (Natural Resources Governance Institute).

Alisema Baraza hilo limeongeza kundi la habari za ushirika, ambazo zitaanza kushindaniwa mwakani, kufuatia ombi ambalo liliombwa na Tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania (TCDC), kuingiza kundi hilo kwenye kinyang’anyilo cha Tuzo za EJAT.

“Baraza la habari Tanzania (MCT) katika utoaji wa Tuzo za umahiri za uandishi wa Habari mwakani, tumeongeza kundi la habari za ushirika, ambapo wakati wa mashindano litatazamwa katika vigezo vile vile vinavyotumika kwenye makundi mengi ambayo yanashindaniwa,”alisema Mallimbo.

“Baada ya kuongeza kundi hili la habari za ushirika, hivyo kutafanya makundi yanayoshindaniwa kwenye Tuzo za EJAT kufika 19, ambapo makundi mengine ni habari za uchumi, biashara, fedha, michezo, utamaduni, kilimo, elimu, utalii, uhifadhi, uchunguzi, data, haki za binadamu na utawala bora, jinsia na watoto,”aliongeza.

Aidha, alitaja Tuzo zingine kuwa ni habari za Gesi, mafuta, madini, walemavu, afya, sayansi na Teknolojia, hedhi salama, mpiga picha bora, mchora katuni, pamoja na kundi la wazi.

Kwa upande wake Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Tanga Henjewele John, alisema kundi hilo kuingizwa kuwaniwa katika Tuzo za habari EJAT, itasaidia kwa kiasi kikubwa kutangaza kazi za Ushirika na kuongeza chachu ya kuhudumia wakulima na kuwainua kiuchumi.

Alisema vyama vya ushirika, vina mchango mkubwa sana hapa nchini katika kuinua uchumi mkulima, pamoja na kuongeza mapato ya Serikali, ambapo humsaidia mkulima kapata dhana bora za kilimo, Pembejeo, na utafutaji wa masoko ya mazao yao.
Afisa Program kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) Paul Mallimbo, akielezea uingizwaji wa kundi jipya la habari za Ushirika kuwania Tuzo za EJAT mwakani.

Mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Tanga Henjewele John, akielezea umuhimu wa Habari za Ushirika kuingia kwenye Tuzo za EJAT.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Na Marco Maduhu-TANGA

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464