JESHI LA POLISI SHINYANGA LATOA ANGALIZO KWA MADEREVA NA WAFANYABIASHARA

 Maderava Boda boda watahadharishwa kuzingatia sheria za usalama barabarani sikukuu za mwisho wa mwaka.


 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando

 Na mwandishi wetu

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga lawataka madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajili kipindi hiki cha kusherekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya, Hayo yameelezwa leo Alhamisi 23, Desemba 2021 na Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akizungumza na vyombo vya habari.

Kamanda Kyando amesema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limejipanga vizuri kwa kuweka ukaguzi wa askari kanzu na askari wenye sare kwa kila maeneo ya barabara za mkoa wa Shinyanga ili kuweza kuwathibiti madereva wa vyombo vya moto wanaokiuka taratibu na kuleta ajali kwa abiria na mali zao.

Akiongea na vyombo vya habari Kamanda Kyando alisema kuwa kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka kumekuwa na hali ya ajali za vyombo vya moto kwa madereva kukiuka sheria za usalama barabarani kutokana na ulevi wa pombe na uzembe.

 Alisisitiza kuwa kipindi hiki madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani watakamatwa kuwekwa mahabusu   na kisha kupelekwa magereza hadi sikukuu za mwisho wa mwaka zitakapo kwisha.

Madereva wa vyombo vya moto wanaokiuka sheria za usalama barabarani watakamatwa, Jeshi la polisi limeweka doria maeneo yote ya barabarani ili kuwalinda abiria na mali zao na nimemwagiza RTO mkoa wa Shinyanga afanye vipimo kwa madereva wote wanaotumia vilevi barabarani ili tuwakamate na kuwachulika hatua za kisheria” Amesema Kyando

Aidha, Kamanda aliwatakia wafanyabiashara wa huduma za kubadilisha fedha mkoa wa Shinyanga kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao kwa kipindi hiki kwa kuwatumia askari wenye mafunzo ya kijeshi kutoka mgambo, JWT na askari wastafuu ili kuweza kulinda mali zao na wateja.

“Maduka makubwa na watoa huduma za fedha wanatakiwa kuwa na walinzi wenye uwezo wa kulinda  si kutumia wazee wasioweza hata kujilinda na kutumia silaha, Kipindi hiki wahalifu kutumia nguvu kubwa kutafuta fedha” Alisema Kyando.

Jeshi hilo limetoa vibali kwa makanisa yaliyo omba kufanya ibada za usku kwa waumini wao na kuwapa ulinzi wa askari watakuwepo katika nyumba za ibada nyakati za usku kwa ajili ya usalama na ulinzi.

Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Shinyanga, Wameshukuru jeshi hilo kwa kuweka nguvu zaidi katika doria ya kusimamia madereva wa vyombo ya moto na kushauri ni vema boda boda wote wenye sifa njema watambuliwe na wenye viti wa mitaa kwa kushirikiana na jeshi la polisi ili waweze kutoa huduma zenye usalama kwa kipindi chote cha mwaka kuliko kuweka nguvu nyakati za sherehe za mwisho wa mwaka tu.

MWISHO.

 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464