KANISA LA KKT SHINYANGA LINAVYOWAINUA MABINTI WENYE UALBINO KIUCHUMI

Mgeni Rasmi Beda Chamatata, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akigawa vyeti kwa wahitimu wa Mafunzo ya Ushonaji nguo na Ujasiriamali kwa Mabinti wenye Ualbino, ambapo mafunzo hayo huaendeshwa na Kanisa la (KKKT), kushoto ni Askofu wa Kanisa hilo Dr, Emmanuel Makala.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MABINTI wenye Ualbino wapatao 11, wamefurahia kuhitimu mafunzo ya ushonaji nguo na ujasiriamali, ambayo wameeleza yatawasaidia kujipatia kipato na kuendesha maisha yao bila ya kuwa tegemezi tena.


Mafunzo hayo ni moja ya program ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini Mashariki ya Ziwa Victoria mkoani Shinyanga, ya kuwainua kiuchumi Mabinti hao wenye Ualbino, pamoja na kutokomeza imani potofu dhidi yao.

Magdalena Mashauri ni mmoja wa wahimitu wa mafunzo hayo, anasema yatawasaidia sana kufanya shughuli zao mbalimbalu za kiuchumi, na kuacha tena kuishi maisha ya shida sababu watakuwa na vyanzo vya kuwaingizia kipato na kuinuka kiuchumi.

“Tunalishukuru Kanisa hili la KKKT kwa kutupatia mafunzo haya ya Ujasiriamali wa kutengeneza bidhaa mbalimbali, na mafunzo ya ushonaji nguo, ambayo yatakuwa mkombozi wa maisha yetu,”alisema Mashauri.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa hilo la KKKT Dr, Emmanuel Makala, alisema Mahafali hayo ni ya Tisa, na walianzisha Programu hiyo mwaka 2016 ya kusomesha mabinti wenye Ualbino mafunzo ya ushonaji nguo na ujasiriamali, na mpaka sasa wamesha wezesha Mabinti 108.

“Ndani ya Program hii hua tunatoa pia elimu ya kutokomeza Imani Potofu dhidi ya watu wenye ualbino, ambapo tumeshatoa elimu kwa wagaga wa Jadi 2,000, viongozi wa dini 5,000, pamoja na kutoa elimu ya kujitambua kwa mabinti hawa wenye ualbino,”alisema Askofu Makala.

Naye Mwenyekiti wa chama cha watu wenye Ualbino Tanzania mkoani Shinyanga (TAS) Unice Zabroni, amelishukuru Kanisa hilo la KKKT kwa kuona thamani ya mabinti hao, na kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatakuwa mkombozi wa maisha yao.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dr, Emmanuel Makala, akielezea Program ya kusomesha Mabinti wenye Ualbino.

Mwenyekiti wa Chama Cha watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) mkoani Shinyanga Unice Zabroni akizungumza kwenye Mahafali hayo.

Binti mwenye Ualbino Magdalena Mashauri akielezea namna mafunzo hayo ya ushonaji nguo na ujasiriamali yatakavyo kuwa mkombozi kwao kimaisha.

Viongozi kutoka Madhehebu Mbalimbali ya kidini wakiwa kwenye Mahafali hayo.

Mahafali yakiendelea.

Mahafali yakiendelea.

Mahafali yakiendelea.

Mahafali yakiendelea.

Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali yao.

Wahitimu wakisoma shairi.

Mgeni Rasmi Beda Chamatata, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akigawa vyeti kwa wahitimu wa Mafunzo ya Ushonaji nguo na Ujasiriamali kwa Mabinti wenye Ualbino ambapo mafunzo hayo huaendeshwa na Kanisa la (KKKT), kushoto ni Askofu wa Kanisa hilo Dr, Emmanuel Makala.

Zoezi la utoaji vyeti likiendelea kwa wahitimu.

Zoezi la utoaji vyeti likiendelea kwa wahitimu.

Zoezi la utoaji vyeti likiendelea kwa wahitimu.

Awali wahitimu wakiingia ukumbini.

Wahitimu wakipiga picha ya pamoja na viongozi dini.

Wahitimu wakipiga picha ya pamoja na viongozi dini kutoka Madhehebu mbalimbali.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.


















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464