Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza kwenye kikao cha Taasisi za Serikali.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ameendesha kikao cha kusikiliza Taarifa za utendaji kazi za Taasisi Mbalimbali za Serikali jimboni kwake, na kuzitaka kila moja itekeleze majukumu yake ipasavyo, na siyo kufanya kazi kwa kusukumwa, ili kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassani kuwa hudumia wananchi na kuwaletea maendeleo.
Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, akizungumzia malengo ya kikao hicho, amesema ni kuona shughuli ambazo zimefanywa na Taasisi hizo za Serikali ndani ya mwaka mmoja, na kufanya Tathimini ya utendaji kazi katika kuwatumikia wananchi.
“Lengo letu kubwa katika kikao hiki, ni kuona nini kimefanyika katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM na ahadi za Mheshimiwa Rais na wagombea wenza wake, Mbunge, Madiwani, wenyeviti wa mitaa, vitongoji na vijiji zimetekelezwa kwa kiwango gani, kwa mujibu wa fedha zilizotengwa katika bajeti na kupelekwa kwenye Taasisi tujue zimefanya nini,”alisema Katambi.
“Tunataka kujua fedha hizi zimefanya nini na zimetumika vipi katika kuwahudumia wananchi na kubadilisha hali nzima ya maisha yao, na kujua wapi kuna tatizo na kulitafutia ufumbuzi, ambapo atazichukua changamoto zote na kuziwasilisha kwenye ngazi za mamlaka za juu na kufanyiwa kazi, ili kusiwe na vikwazo katika kuwahudumia wananchi,”aliongeza Katambi.
“Naziomba pia Taasisi za Serikali ziwajibike ipasavyo kuwatumikia wananchi, na siyo kusubili hadi msukumwe, sababu kazi yenu ni kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassani kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo,”alisisitiza.
Pia, alipongeza Taarifa ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) juu ya Mradi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano kutoka Mwanza hadi Isaka, namna walivyozingatia suala la utoaji ajira kwa wazazi, wa maeneo ambayo ujenzi wa mradi huo unapita na kuwataka pia wafuate masuala ya (Local Content) kwa kununua bidhaa na malighafi kutoka ndani ya nchi, ili kukuza uchumi wa wananchi.
“Kwenye suala la Ajira nimefurahishwa na Taarifa ya TRC kwenye mradi wa Reli ya kisasa, kwa kuajiri watu wa eneo ambalo mradi unafanyika na kuajiri Watanzania wengi kuliko wageni, kwenye miradi hii mikubwa ya maendeleo tunataka itusaidie watu wetu kuajirika pamoja na kununuliwa bidhaa zao ambazo wanazalisha ilikukuza uchumi wao,”alisema Katambi
“Pia Makampuni yazingatie suala la kuwajibika kwa jamii (CSR) ilikuwa na mahusiano mazuri na jamii, kwenye maeneo ambayo miradi inapita kwa kujenga hata barabara, darasa, kuboresha vyoo vya shule, kutoa vitabu, hali ambayo itasaidia miundombinu yenu kulinda na wananchi na kutohujumiwa,”aliongeza.
Aidha, aliipongeza pia Serikali ya Mkoa wa Shinyanga, kwa utoaji wa mikopo na kukuza ajira kwa vijana katika kuhakikisha wanawainua kiuchumi kupitia mikopo na kujiajiri wenyewe.
Naye Naibu Meneja Mradi wa Reli ya kisasa kipande cha Tano kutoka Mwanza hadi Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Mhandisi Alex Bunzu, akisoma taarifa ya mradi huo, alisema ulisainiwa januari mwaka huu kwa gharama ya Sh.Trilioni 3.06 na utakamilika Mei 2024.
Alisema kwa upande wa Ajira, mradi huo umeajiri vijana wa kitanzania 2,094 ambao ni wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu na ufundi , pamoja na vibarua 859 kutoka katika maeneo ambayo yanapitiwa na mradi huo.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary, akisoma taarifa ya mkoa huo kwa upande wa uwezeshaji vijana kiuchumi, alisema Mkoa huo unakadiriwa kuwa na vijana 697,556 wenye umri kuanzia miaka 18-35, sawa na asilimia 35 ya wakazi wote mkoani humo.
Alisema katika uwezeshaji vijana kiuchumi kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri, katika mwaka wa fedha (2020-2021) jumla ya vikundi 597 ya vijana yaliundwa, ambapo kati ya hivyo vikundi 103 vilipata mikopo Sh,milioni 601 kutoka Halmashauri zote sita za mkoa huo, na kuzalisha ajira kwa vijana 1,035.
Alisema katika mwaka wa fedha (2021-2022) mkoa umeendelea kutoa fedha za mikopo kwa vijana kupitia asilimia 10, kuwa kuanzia Julai hadi Novemba, vikundi 90 vimenufaika na mikopo hiyo, yenye thamani ya Sh.milioni 602 na kufanikiwa kuzalisha ajira kwa vijana 928.
Aidha, kwa upande wa Taasisi hizo za Serikali, kila moja iliwasilisha taarifa zake, na kueleza namna walivyowahudumia wananchi, na walivyojipanga mwakani kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwamo kuongeza Mtandao wa Maji,umeme, na ukabarati na miundombinu ya Barabara.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofis ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary, akizungumza kwenye kikao hicho.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rafael Nyandi, akimwakilisha pia Mwenyekiti wa CCM wilayani humo, akizungumza kwenye kikao hicho.
Naibu Meneja Mradi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano kutoka Mwanza hadi Isaka Mhandisi Alex Bunzu, akiwasilisha taarifa ya mradi huo kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola, akiwasilisha taarifa ya Taasisi hiyo kwenye kikao hicho.
Meneja wakala wa maji vijijini Wilaya ya Shinyanga (RUWASA)Mhandisi Emmael Nkopi, akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi kwenye kikao hicho.
Meneja wakala wa Barabara Mjini (TARURA) wilaya ya Shinyanga Mhandisi Samson Pamphil, akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi kwenye kikao hicho.
Meneja wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Grace Ntungi, akiwasilisha taarifa ya Taasisi hiyo kwenye kikao hicho.
Viongozi wakiwa meza kuu kwenye kikao hicho.
Wajumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga, wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga, wakiwa kwenye kikao hicho.
Kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA