KATAMBI AMPONGEZA RAIS SAMIA UJENZI VYUMBA MADARASA

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Kolandoto, (kushoto) ni Kaimu Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Chibugu Mugini.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassani, kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa nchi nzima.

Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira ametoa pongezi hizo leo Decemba 27, 2021 alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za Sekondari na Shikizi Manispaa ya Shinyanga, akiwa ameambatana na wataalam, pamoja na kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Shinyanga mjini.

Alisema amekagua ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa, na kupokea taarifa kutoka kwa wakuu wa shule, kuwa yamemaliza changamoto ya upungufu wa vyumba hivyo kwa baadhi ya shule, ambapo wanafunzi watasoma katika mazingira mazuri bila ya mrundikano darasani na kufanya vizuri kitaaluma, na kumpongeza Rais Samia kwa ujenzi huo wa madarasa.

“Wananchi wa jimbo la Shinyanga tumpongeze Rais wetu Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha za ujenzi wa vyumba hivi vya madarasa, ambapo watoto wetu wanaoingia kidato cha kwanza mwakani, watasoma katika mazingira mazuri sababu vyumba vya madarasa vipo vya kutosha,”alisema Katambi.

"Nimekagua pia ujenzi wa vyumba hivi vya madarasa kwa kweli nimeona thamani yake ya fedha, mmejenga kwa ubora unaotakiwa, ambapo licha ya kujenga vyumba viwili vya madarasa kwa Sh.milioni 40, lakini mmejiongeza na kujenga Ofisi moja ya walimu,"aliongeza Katambi.

Aidha, Katambi aliwapongeza Wananchi wa Shinyanga kwa kumuunga mkono Rais Samia kwenye ujenzi wa vyumba hivyo vya Madarasa, na kutoa nguvu kazi ikiwamo kushiriki kwenye shughuli za uchimbaji msingi.

Katika hatua nyingine, akikagua ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja, aliwataka wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA), kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu hiyo, pamoja na kuzingatia ubora unaotakiwa na kuikamilisha kwa wakati.

Nao Wakuu wa shule Deus Maganga wa Kolandoto na Cosmas Nkoko wa Uzogole, kwa nyakati tofauti, walisema ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa, utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya msongamano wa wanafunzi madarasani.

Ziara ya Mbunge Katambi itaendelea kesho kwa kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na pamoja na miundombinu ya barabara na Madaraja.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira,akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, miundombinu ya barabara na madaraja.
 
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza kwenye ziara hiyo.
Katibu wa umoja wa vijana UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rafael Nyandi, akizungumza kwa niaba ya Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Agnes Bashemu, kwenye ziara ya Mbunge Katambi.

Katibu wa Itikadi siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Saidi Bwanga, akizungumza kwenye ziara hiyo.
Diwani wa Vitimaalumu Manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri, akizungumza kwenye ziara hiyo.

Diwani wa Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Ruben Kitinya akizunguma kwenye ziara hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Kolandoto, (kushoto) ni Kaimu Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Chibugu Mugini.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Kolandoto.
Muonekano ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Kolandoto.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ubora wa Ubao katika Shule ya Sekondari Kolandoto.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ubora wa Ubao katika Shule ya Sekondari Kolandoto, (kushoto) ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Uzogole.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ubora ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Uzogole, akiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ubora ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Town.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Town.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ubora ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Town, (kulia) ni Diwani wa Kata ya Mjini Gulamhafeez Mukadam.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akiangalia ujenzi wa kutunzia nyaraka za Mkuu wa Shule katika Shule ya Sekondari Town iliyobuniwa katika ujenzi wa vyumba vya Madarasa shuleni hapo.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Kizumbi.
Muonekano ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na Ofisi katika shule ya Sekondari Ibinzamata.

Muonekano wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Ngokolo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ujenzi wa miundombinu ya barabara na daraja katika barabara ya Uzogole- Bugwandege.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ujenzi wa Daraja la Ndembezi Mwanoni.
ukaguzi ujenzi Daraja wa Ndembezi Mwanoni ukiendelea.
ukaguzi ujenzi Daraja la Mwagala-Itilima ukiendelea.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akisaidiana na mafundi wa ujenzi wa Daraja la Mwagala-Itilima.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, (wapili kushoto) akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa jimboni kwake.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.























































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464