KATAMBI AMPONGEZA RAIS SAMIA UTAFUTAJI FEDHA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule Shukizi ya Negezi Kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MBUNGE wa jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassani, kwa utafutaji fedha na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
 
Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, amebainisha hayo leo Decemba 28, 2021, wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili jimboni kwake, ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, miundombinu ya barabara, madaraja, na kituo cha afya.

Alisema anampongeza Rais Samia Suluhu Hassani, kwa kazi kubwa ambayo ameifanya, ya utafutaji fedha na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa, miundombinu ya barabara, madaraja, na kituo cha afya.

"Miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, miundombinu ya barabara,madarajana kituo cha afya, hii ni kazi kubwa ambayo imefanywa na Rais Samia Suluhu Hassani, kwa kutafuta fedha na kuzitoa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, na kuboresha mazingira rafiki ya wanafunzi kusoma," alisema Katambi.

"Kutokana na kazi kubwa ambayo anaifanya Rais Samia Suluhu Hassani, tunapaswa kumpongeza na kumuunga mkono, ili azidi kuwaletea maendeleo Watanzania," aliongeza.

Aidha, alitoa wito kwa wanafunzi wasome kwa bidii na kutimiza ndoto zao, sababu Rais Samia ameshawajengea mazingira rafiki ya kusoma, kwa kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu.

Katika hatua nyingine, Katambi amemuagiza Mkandarasa ambaye anatekeleza ujenzi wa madaraja na miundombinu ya barabara Manispaa ya Shinyanga, kukamirisha jenzi hizo kwa wakati na ubora unaotakiwa.

Nao baadhi ya wakuu wa shule za Sekondari Manispaa ya Shinyanga, walisema ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa, umemaliza changamoto ya upungufu wa madarasa, ambapo wanafunzi watasoma bila msongamano na kufanya vizuri masomo yao.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Manispaa ya Shinyanga Chibugu Mugini, alisema walipokea fedha Sh.milioni 800. kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 44, 35 kwa shule za Sekondari na Shikizi vyumba Tisa.

Ziara hiyo ya Mbunge Katambi, ameifanya siku mbili kwa Kata zote 17 za Manispaa ya Shinyanga, kwa kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, miundombinu ya barabara na madaraja, ambapo kesho atafanya mkutano mkubwa wa hadhara, katika viwanja vya miti mirefu Majengo kwa honda
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kumpongeza Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili utekelezaji wa miradi hiyo.
Katambi, akiendelea kuzungumza na kutoa maelekezo juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza kwenye ziara hiyo.
Diwani wa Chibe John Kisandu, akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassani na wasaidizi wake juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa vyumba vya Madarasa.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Ndala, (kulia) ni Diwani wa Kata ya Ndala Zamda Shabani.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ubora wa Ubao katika ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Ndala, (kulia) ni Diwani wa Kata ya Ndala Zamda Shabani.
Muonekano ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa na Ofisi katika Shule ya Sekondari Ndala.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ujenzi wa chumba kimoja cha darasa katika Shule ya Sekondari Mwawaza.

Muonekano ujenzi chumba kimoja cha darasa Shule ya Sekondari Mwawaza.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, (kulia) akikagua ubora wa Ubao katika Shule ya Sekondari Mwangulumbi iliyopo Chibe.
Ukaguzi ujenzi vyumba vya Madarasa Shule ya Sekondari Mwangulumbi- Chibe ukiendelea.

Muonekano ujenzi vyumba vya Madarasa Masekelo.

Muonekano ujenzi chumba kimoja cha darasa Mwamalili.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira,(katikati) akikagua ujenzi kituo cha Afya Ihapa- Oldshinyanga.

Muonekano ujenzi kituo cha Afya Ihapa- Oldshinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, (kushoto) akikagua ujenzi wa kivuko cha watembea kwa miguu katika Daraja la Upongoji- Ndala Manispaa ya Shinyanga.

Muonekano wa kivuko hicho.

Awali kabla ya ziara yake Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, (kushoto) akiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, wakimtembelea Diwani wa Mwamalili Paul Machela ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga akipatiwa matibabu.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, (kushoto) akibadilisha mawazo na Madaktari pamoja na ndugu wa diwani wa Mwamalili Paul Machela namna ya kumhudumia ili apone na kurudi kwenye majukumu yake ya kutumikia wananchi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.






































































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464